Thursday, November 12, 2015

WANAFUNZI WA ISS WAMTEMBELEA BALOZI MPYA WA TANZANIA, UHOLANZI


 Kutoka kushoto ni Ndg. Shamy Chamicha,  Ndg. Jackosn Bulili, Mhe. Balozi Kasyanju, Ndg. Florence Chakina na Ndg. Hofman Sanga.



Mhe. Irene F. M. Kasyanju, Balozi wa Tanzania, Uholanzi amekutana na wanafunzi wanne (4) kati ya watano (5) wa Kitanzania wanaosoma shahada tofauti katika Taasisi iitwayo “International Institute of Social Studies (ISS)”,ya Chuo Kikuu cha Erasmus, Rotterdam ambao walifika Ubalozini kwa lengo la kumsalimu na kufahamiana.



Pamoja na mambo mengine wanafunzi hao wamewasilisha ombi lao kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Mhe. Balozi wa kuiomba isaidie kuhakikisha kuwa idadi ya “Scholarships” kwa Tanzania kwenye Chuo hicho inaongezeka.  Hii ni kutokana na idadi ya Watanzania wanojiunga na ISS kupungua sana ukilinganisha na nchi zingine za Afrika hususan za Afrika Mashariki, tofauti na ilivyokuwa zamani.



Balozi kwa upande wake alipokea ombi lao na kuahidi kulifanyia kazi ipasavyo. Aliwashukuru wanafunzi hao kwa kufika Ubalozini kujitambulisha na akawaahidi ushirikiano wakati wote watakaokuwepo Uholanzi.










No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.