Wednesday, November 25, 2015

Balozi Mushy amuaga Mwakilishi wa UNICEF nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akimkabidhi zawadi Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini Dkt. Jama Gulaid aliyemaliza muda wake wa Uwakilishi nchini.
Moja ya zawadi alizopokea kutoka kwa Balozi Mushy ni Kitabu kinachoelezea Vivutio mbalimbali vya Utalii vinavyo patikana hapa nchin.

Pia katika mazungumzo yao, Balozi Mushy alimpongeza Dkt. Gulaid kwa kuiwakilisha vyema   UNICEF hapa nchini. kwa Upande wa Dkt. Gulaid naye alitumia fursa ya kumshukuru Balozi Mushy kwa niaba ya Wizara  na Serikali kwa ujumla kwa Ushirikiano mkubwa alioupata katika kipindi chote cha uwakilishi wa UNICEF hapa nchini.   
Balozi Mushy akizungumza na Dkt. Gulaid
Dkt. Gulaid naye akizungumza huku Balozi Mushy akimsikiliza.


Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.