Thursday, November 5, 2015

Magufuli Aapishwa kuwa Rais wa awamu ya Tano wa Tanzania Leo Jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akila  kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mh. Mohamed Chande Othman, katika  Sherehe za kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo.Kushoto ni Rais aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Makamu wake, Mh. Dkt. Mohamed Gharib  Bilal. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

Rais aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davies Mwamunyange, wakati  akiwaaga wananchi mara tu alipowasili kwenye Uwanja wa Taifa, katika Sherehe za kuapishwa Rais Mpya wa awamu ya tano, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, zilizofanyika leo jijini Dar es salaam. 

Rais aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salamu ya heshima ya kijeshi kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais Mpya wa awamu ya tano, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais Mpya wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akionyesha Mkuki na Ngao aliokabidhiwa na Wazee wa kimila ikiwa ni ishara ya Uongozi wa Kitaifa, katika Sherehe za kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride maalum la Jeshi la Ulinzi lenye Umbo la Alfa, ikiwa ni ishara ya kuanza kwa Serikali mpya ya awamu ya tano, katika Sherehe za kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo. Sherehe hizo zimehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (wa sita kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Marais kutoka nchi mbalimbali walioudhuria katika Sherehe za Kumwapisha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (wa pili kutoka kushoto), Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kutoka kulia), Mke wa Rais Magufuli Mama Janeth Magufuli (wa kwanza kulia) na Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.