Friday, December 27, 2019

Mhe. Waziri Kabudi akutana na kupokea nakala za Hati za Utambulisho za Mabalozi Wateule wa Algeria na Ujerumani


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana, kufanya mazungumzo na kupokea nakala za Hati ya Utambulisho ya Balozi Mteule wa Algeria Mhe.  Ahmed Djellal pamoja na Balozi Mteule wa Ujerumani Mhe. Balozi Regine Hess.

Prof. Kabudi amekutana na mabalozi hao wateule leo jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, kabla ya kukabidhiwa nakala za hati za utambulisho kukoka kwa mabalozi hao, Prof. Kabudi amefanyaa mazungumzo na Mabalozi wateule ambapo mazungumzo hayo yaliyolenga kuimarisha uhusiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria pamoja Shirikisho la Ujerumani.

Waziri Kabudi alimweleza Balozi mteule wa Algeria nchini Tanzania kuwa Tanzania na Algeria zimeendelea kuwa na uhusiano mzuri na wa kihistoria tangu miaka ya 1960 wakati wa harakati za ukombozi wa bara la Afrika dhidi ya ukoloni…"Misingi ya uhusiano wa Tanzania na Algeria ulijengwa na Waasisi wa Mataifa haya mawili, Hayati Mwl. Julius Nyerere na Hayati Ahmed Ben Bella wa Algeria," Amesema Prof. Kabudi

Waziri Kabudi ameongeza kuwa, Algeria imeendelea kuwa na Ubalozi wake hapa nchini Tanzania tangu mwaka 1964 ikiwa ni miongoni mwa nchi za mwanzo kabisa kufungua ubalozi hapa nchini. Mwaka 1981 nchi hizi mbili zilianzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) ambayo imechangia kuimarisha na kukuza ushirikiano katika masuala mbalimbali ikiwemo diplomasia, ulinzi, elimu, madini, nishati na michezo.

 Kwa upande wake Balozi mteule wa Algeria Mhe. Balozi Ahmed Djellal ameahidi kuwa Serikali ya Algeria itaendeleza ushirikiano mzuri uliopo kati yake na Tanzania hususani diplomasia, kukuza na kuimarisha biashara, uwekezaji na utalii.
"Mimi Balozi Mteule nitashughulikia na kuhakikisha kwamba uwekezaji na biashara unaofanywa kati ya Algeria na Tanzania unakuwa wa manufaa kwa pande zote mbili lengo likiwa ni kukuza sekta ya biashara hapa Tanzania" Amesema Mhe. Balozi Djellal

Katika tukio jingine, Prof. Kabudi amepokea nakala za Hati ya Utambulisho za Balozi Mteule wa Shirikisho la Ujerumani hapa nchini, Mhe. Balozi Regine Hess ambaye amemweleza Waziri Kabudi kuwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Ujerumani ni mzuri na kuongeza kuwa jukumu lake kubwa kwa sasa ni kuendeleza uhusiano huo.

Balozi Regine Hess ameyasema hayo wakati akikabidhi nakala za Hati ya Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb).

Balozi Regine Hess amesema kuwa mbali na uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Ujerumani, ushirikiano mzuri uliopo wa uwekejzaji, biashara, utalii na elimu utaendelea kuimarika na kutoa zaidi fursa za maendeleo kwa Tanzania.

"Kuna baadhi ya wawekezaji kutoka Ujerumaani ambao wameshaonesha nia ya kutaka kuwekeza Tanzania, hivyo nitawasiliana nao na kuweza kujua wamefikia wapi kwani Tanzania ina sifa nzuri. Jukumu langu nikiwa Balozi hapa ni kukuza na kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya Ujerumani na Tanzania, hivyo nitajitahidhi niwezavyo kufanikisha jukumu hilo," Amesema Balozi Hess.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisoma nakala ya Hati ya Utambulisho mara baada ya kukabidhiwa na Balozi Mteule wa Shirikisho la Ujerumani hapa nchini katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisoma nakala ya Hati ya Utambulisho mara baada ya kukabidhiwa na Balozi Mteule wa Shirikisho la Ujerumani hapa nchini Mhe. Balozi Regine Hess katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Balozi Mteule wa Shirikisho la Ujerumani Mhe. Balozi Regine Hess akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) kabla ya kuwasilisha nakala ya Hati ya Utambulisho. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkaribisha Balozi Mteule wa Shirikisho la Ujerumani Mhe. Balozi Regine Hess alipowasili katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kuwasilisha nakala ya Hati ya Utambulisho kwa mhe. waziri 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na Balozi mteule wa Algeria nchini Tanzania Mhe. Balozi Ahmed Djellal kabla ya kuwasilisha nakala ya Hati ya Utambulisho. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.




Balozi mteule wa Algeria nchini Tanzania Mhe. Balozi Ahmed Djellal akimkabidhi nakala ya Hati ya Utambulisho Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Wednesday, December 25, 2019

WATALII ZAIDI YA 450 KUTOKA ISRAEL WAKO NCHNI KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII




Watalii kutoka nchini Israel walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) watalii hao wako nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii nchini wakati huu wa Siku Kuu za Krismasi na Mwaka mpya.
Watalii kutoka nchini Israel wakiingia ndani ya uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii wakati wa mapumziko ya mwisho wa mwaka na Siku Kuu za Krismasi na Mwaka mpya

Watalii kutoka nchini Israel wakielekea sehemu maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya mapokezi yao baada ya kuwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) watalii hao wako nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii nchini wakati wa mapumziko ya mwisho wa Mwaka na Siku Kuu za Krismasi na Mwaka mpya wa 2020.

Watalii kutoka nchini Israel wakiwa ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) baada ya kuwasili nchini  kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii wakati wa Siku Kuu za Krismasi na Mwaka mpya wa 2020.


Kikundi cha ngoma cha Kimasai kikiwa ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kutumbuiza wakati wa hafla ya kuwapokea  Watalii kutoka nchini Israel waliowasili nchini  kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Jaji Mst. Mhe. Thomas Mihayo (wa pili kulia) akiwa na Mkurugrenzi Mtendaji wa TTB Bi Devota Mdachi wa (kwanza kushoto) wakiwa na baadhi ya watalii kutoka nchini Israel mara baada ya kuwapokea katika Uwanja wa KIA walipowasili nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii.


Watalii zaidi ya 450 kutoka Israel wamewasili nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio vya kitalii vilivyoko kaskazini mwa Tanzania. Watalii hao wamekuja nchini kwa kutumia ndege binafsi na za kawaida.
 
Kundi la kwanza la watalii 150 liliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) tarehe 21 Desemba 2019 na kupokelewa na Bodi ya Utalii nchini (TTB) na baadaye kuelekea katika vivutio vya utalii vilivyoko mkoani Arusha.

Kundi la pili na la tatu lililokuwa na watalii 313 limewasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege KIA  tarehe 24 Desemba 2019.

Watalii hao wako nchini kwa ajili ya kusherehekea sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya wanatembelea Hifadhi za Taifa za Serengeti, Tarangire, Ziwa Manyara, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorogoro na Bonde la Eyasi.

Ubalozi wa Tanzania nchini Israel umetoa viza zaidi ya 500 kwa Waisrael ambao wamepanga kuwasili nchini kwa kutumia Mashirika ya Ndege ya Ethiopia, Uturuki na Uswisi katika kipindi hiki cha siku kuu za mwisho wa mwaka  huku ukiendelea kuratibu ziara nyingine ya watalii zaidi ya 800 ambao mchakato wa safari yao upo katika hatua za mwisho.

Ujio wa watalii hao unatokana na jitihada za kuvutia watalii zinazofanywa na Ofisi ya Ubalozi nchini Israel kwa kushirikiana na makampuni ya wakala wa utalii ya ndani na nje ya nchi ili kuunga mkono harakati za Serikali za kukuza pato la taifa kupitia utalii na hivyo kuiletea nchi maendeleo.

       

Tuesday, December 24, 2019

PROF. KABUDI AKUTANA, KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UTURUKI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Balozi Ali Davutaglu katika ofisi ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri Kabudi amemweleza Balozi Davutaglu kuwa Uhusiano kati ya Tanzania na Uturuki ni wa muda mrefu na mahusiano hayo ni imara hadi sasa. 

"Ushirikiano wa Tanzania na Uturuki ni wa muda mrefu na ni imara kwa kweli, pamoja na mambo mengine uhusiano huu umekuwa ukijikita katika kuendeleza uwekezaji wa viwanda, elimu na utalii hasa katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania katika shirika la ndege la Uturuki," Amesema Prof. Kabudi.

Waziri Kabudi ameongeza kuwa, uhusiano wa Tanzania na Uturuki ni imara hivyo kwa sasa ni kuendelea kuimarisha uhusiano huo kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali mfano kuwekeza katika sekta ya biashara na uwekezaji. “…naamini tukiwekeza katika viwanda hasa vya nguo hapa nchini ni fursa ambayo italiwezesha taifa la Tanzania kupata bidhaa nzuri na imara,". Amesema Prof. Kabudi

Kwa upande wake Balozi wa Uturiki nchini Tanzania, Mhe. Balozi Ali Davutaglu amesema kuwa Uturuki ni nchi ambayo imekuwa ikiheshimu taratibu za nchi ya Tanzania na ni marafiki wazuri na wa siku nyingi hivyo ataendelea kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali yanasonga mbele ili kuiwezesha Tanzania kuwa na  maendeleo endelevu.

"Uwekezaji ni muhimu sana kwa nchi zetu hizi mbili na tayari nimeshawasiliana na Umoja wa Wasafirishaji na ule wa Mawakala wa Utalii Uturuki  ili waweze kutembelea Tanzania pamoja na kuangalia fursa za uwekezaji kwa lengo la kuwekeza na hatimaye kukuza sekta hizi na  uchumi wa mataifa haya mawili," Amesema Balozi Davutaglu.

Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Balozi Ali Davutaglu akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akifafanua jambo kwa Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Balozi Ali Davutaglu wakati walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Balozi Ali Davutaglu wakati walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


SERIKALI YALITAKA SHIRIKA LA MSALABA MWEKUNDU TANZANIA (TRCS) KUENDELEA KUTOA HUDUMA ZA MATIBABU KATIKA KAMBI ZA WAKIMBIZI MKOANI KIGOMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji K. Mnyepe ametoa msimamo huo wa Serikali alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bw. George Kuchio katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Aidha, Dkt. Mnyepe ameitaka UNHCR kuzingatia na kuheshimu makubaliano baina yake na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1991 hususani Ibara ya Pili na ya Tatu (Articles II & III). Ibara hizo zinaelekeza kwamba UNHCR ni lazima ishirikiane na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutekeleza majukumu yake hapa Nchini.

Hivi karibuni UNHCR ililitaka Shirika la Msalaba mwekendu Tanzania (TRCS) kukabidhi majukumu yao bila kuihusisha serikali. Hatua hiyo ya UNHCR inavunja makubaliano ya 1991.

Hivyo amewaeleza UNHCR kwamba Shirika la Msalaba mwekundu Tanzania kuendelea na majukumu yake kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo mpaka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na UNHCR watakapokubaliana vinginevyo.




Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe (kulia) akimsisitiza Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bw. George Kuchio, kuzingatia na kuheshimu makubaliano baina UNHCR na Serikali ya Tanzania ya mwaka 1991. Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe (kulia) akimueleza jambo Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bw. George Kuchio. Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.


Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bw. George Kuchio (kushoto) akimueleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe wakati wa mazungumzo katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam



Monday, December 23, 2019

Wizara Yapanda Miti kufuatia Mvua Zinazonyesha Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji K. Mnyepe akipanda mti katika ofisi za Wizara zilizopo Mtumba, Ddodoma. Katibu Mkuu aliongoza Wakuu wa Idara/Vitengo na watumishi kupanda miti kwa awamu ya pili kufuatia mvua kubwa zinazonyesha mjini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji K. Mnyepe akiendelea na shughuli ya kupanda mti

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji K. Mnyepe akifukia mchanga katika shimo alilopanda mti

Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen P. Mbundi akipanda mti

Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Bw. Japhary Kachenje akipanda Mti

Afisa kutoka Idara ya Asia na Australasia skipanda mti.

Bi. Ellen Maduhu kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa akipanda mti wake.

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Bibi. Caroline Chipeta akipanda mti

Bw. Ali Ubwa kutoka Idara ya Afrika naye akipanda mti

Thursday, December 19, 2019

WAZIRI KABUDI AKUTANA, KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UFARANSA NCHINI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Kabudi amemueleza Mhe. Balozi Clavier kuwa, uhusiano baina ya Tanzania na Ufaransa ni wa muda mrefu ambapo hadi sasa Tanzania imekuwa na mahusiano imara na taifa hilo.

Aidha, pamoja na mambo mengine, mazungumzo yao yalijikita katika kuongeza ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa, kuongeza ushirikino wa maendeleo, kuimarisha uwekezaji, biashara pamoja na kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama.



Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati balozi huyo alipokutana na Mhe. Waziri leo katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimuelezea jambo Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier wakati alipokutana na balozi huyo leo katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimsisitiza jambo Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier wakati alipokutana na balozi huyo leo katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati balozi huyo alipokutana na Mhe. Waziri leo katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier






TAARIFA KWA UMMA KUHUSU FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO


INDIA KUFANYA UWEKEZAJI MKUBWA TANZANIA

Ujumbe wa Tanzania na India ukiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mazungumzo kuhusu uwekezaji.

Sunday, December 15, 2019

SMZ YAAHIDI KUKAMILISHA SHERIA YA DIASPORA KABLA YA MEI 2020


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia hadhara ya Diaspora Tanzania (haipo pichani) katika kongamano la sita la diaspora
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Issa Haji Ussi Gavu, akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein kuhutubia kongamano la sita la Diaspora
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akipokea moja ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wadogo Zanzibar wakati alipotembelea banda la wajasiriamali, kabla ya kufungua rasmi kongamano la sita la Diaspora Tanzania. Kulia kwake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akifuatiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, George Simbachawene pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Issa Haji Ussi Gavu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akipokea moja ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wadogo Zanzibar wakati alipotembelea banda la wajasiriamali, kabla ya kufungua rasmi kongamano la sita la Diaspora Tanzania. Kulia kwake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akifuatiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, George Simbachawene. 


Baadhi ya ujumbe wa Diaspora ukiwa umesimama wakati wa kuimba wimbo wa taifa wa Tanzania katika kongamano la sita la Diaspora lililofanyika Zanzibar


Na Nelson Kessy, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, amewahakikishia wanadiaspora kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itasimamia na kuhakikisha kuwa sheria ya Diaspora inakamilika kabla ya mwezi Mei, 2020.

Rais Dkt. Shein ametoa kauli hiyo leo mjini Zanzibar wakati alipokuwa akifungua rasmi kongamano la sita la Diaspora ambalo limeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi-Zanzibar. Dhamira ya kongamano hili kuendeleza ushirikiano uliopangwa na Diaspora na wawekezaji kama wadau wa maendeleo nchini chini ya kauli mbiu ya "mtu kwao ndio ngao".

Ndugu wanadiaspora mwaka jana nilieleza jitihada za kuanziasha ofisi za Diaspora hapa Zanzibar kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati ule kwa kuanziasha Diaspora.

"Kutokana na kutambua umuhimu wa watanzania waishio nje ya nchi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliunda idara maalumu ya kushughulikia masuala ya Diaspora katika wizara ya Mambo ya nje mwaka 2010 ili kuvitekeleza kwa vitendo azma yetu ya kuwashirikisha wanadiaspora Tanzania katika kuendeleza nchi yetu," Amesema Dkt. Shein

Ameongeza kuwa kwa umuhimu huohuo, na kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya ccm ya mwaka 2010 na kuyapa nguvu masuala ya Diaspora tulianzisha kitengo cha Diapora na baadae idara ya Diaspora ilinzishwa hapa Zanzibar.  Tulitengeneza sera maalumu ya wanadiaspora, na sasa tupo mbioni kuanzisha sheria ya Diaspora, nimefurahi kuwa rasimu ya sheria hiyo imefikia katika hatua nzuri.

"Kwa matiki hiyo basi, namuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Issa Haji Ussi Gavu kuhakikisha anasimamia kwa karibu sana utayarishaji na kukamilika kwa rasimu ya sheria hiyo na iwasilishwe kwenye Baraza la wawakilishi kabla ya mwezi mei 2020," Amesema Dkt. Shein na kuongeza kuwa atahakikisha kuwa kabla ya kumaliza muda wangu wa Urais  hapa Zanzibar sheria hiyo itakuwa imekaa vizuri kimkakati, kisera pamoja na kisheria kwa upande wa Zanzibar.
Aidha, Rais Shein, aliwapongeza wanadiaspora kwa michango yao ambayo wamekuwa wakiitoa kwa kusaidia Serikali, pamoja na mambo mengine michango hiyo imekuwa ikisaidia kijamiii na kiuchumi.

Awali akitoa salamu za wanadiaspora, Mwenyekiti wa wanadiaspora, Norman Jasson alisema kuwa mchakato wa sera ya Diaspora umekuwa ni wa muda mrefu na kumekuwepo na ukimya takribani miaka mitatu na kumuomba Rais Dkt. Shein kuwasaidia kusimamia zoezi hilo.

"Sera ya Diaspora ina umuhimu wa kipekee kwani tunaamini kuwa sera hiyo itakapokamilika itatoa majibu ya maswali mengi ambayo yamekuwa yakitunyima usingizi. Tunaamini sera hii itasaidia sio tu masuala ya uraia wan chi mbili au hadhi maalum, bali pia masuala mengine kama umiliki wa ardhi, mirathi, ndoa kwa wenyeji na wageni, ruhusa ya makazi nchini kupitia vibali au visa na mengine mengi," amesema Bwn. Jasson  

Aliongeza kuwa, pia wanadiaspora wanaamini kuwa sera hiyo itarahisisha utungaji wa sheria itakayowatambua watanzania wote walio ughaibuni bila kujali kama tayari wameshachukua uraia wa nchi nyingine au kama tayari wana vibali vya makazi katika nchi wanazoishi na pia bila kujaliwaliingiaje ughaibuni katika kusaka maisha.

Bwana Jasson aliongeza kuwa, msingi wa wanadiaspora ni utanzania wao na utayari wa kushiriki katika jitihada za kusuma maendeleo ya kiuchumi na kijamii kama vile kuhamasisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini ambapo kwa sasa TDC-Global tayari imewaleta Tanzania watu wenye nia ya kuwekeza.
"Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa kushirikiana na Diaspora itafanikisha mambo mengi kwa kuanzisha mkakati wa wa kuhakikisha kuwa watanzania waishio nje ya nchi wanatayarishiwa mfumo ambao utasaidia kukusanya michango ya kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo," amesema Bwn. Jasson.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, George Simbachawene akitoa shukrani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Shein amesema kuwa sera ya Diaspora kwa upande wa Tanzania rasimu ya kwanza tayari imekamilika na hatua inayofuata ni kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wanadiaspora wenyewe kupitia balozi zetu ili na wao waweze kutoa mawazo yao.

"Mhe. Rais, kwa sasa sera ipo katika hatua nzuri, jitihada kubwa zinaendelea na jambo hili linahitaji kushughulikiwa kwa uangalifu mkubwa kwa sababu ya historia ya nchi yetu," Amesema Simbachawene.

Aidha, Waziri Simbachawene aliongeza kuwa ni muhimu kutumia wanadiaspora kama fursa, sekta muhimu katika ujenzi wa uchumi wa taifa letu na mataifa mengi dunini yanafanya hivyo.

Pamoja na mambo mengine, kongamano hili la sita la Diaspora limejadili mada saba ambazo ni urejeshaji wa taka za plastiki, Tanzania na uwekezaji, Diaspora na uwekezaji, Mradi wa nyumba za bei nafuu, kilimo cha kisasa, kubadili mfumo wa utalii wa Zanzibar pamoja na Mradi wa daraja la Zanzibar - Tanzania bara.

Mwezi Augusti, 2018 watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) walikutana Chake Chake, kisiwani Pemba katika kongamano la tano la Diaspora kufuatia  utaratibu uliowekwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar  kuwakutanisha kila mwaka Watanzania waishio ughaibuni.