Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
inashiriki katika Maonesho ya Nne ya Viwanda yaliyoandaliwa na Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).
Kupitia Maonesho hayo, Wananchi wanaelimishwa kuhusu
majukumu ya Wizara na utekele zaji wake na namna wizara na balozi za Tanzania zinavyofanya
kazi ya kuvutia watalii na wawekezaji kuja nchini kutembelea vivutio vya
kitalii na kuwekeza nchini.
Maonesho hayo ni utekelezaji kwa vitendo kwa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya
kujenga Uchumi wa Viwanda ili kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa
2021.
Kauli mbiu ya maonesho hayo ya Tanzania sasa Tunajenga Viwanda
inalenga kujenga na kuimarisha utamaduni wa Watanzania kutambua, kununua na
kuthamini bidhaa zinazozalishwa nchini.
Maonyesho ya Nne ya Viwanda yanahusisha wadau wa Sekta ya
Viwanda na yataonesha fursa zilizopo katika katika sekta ya viwanda na yatatoa
fursa kwa wadau kuzungumza na kujadili
namna ya kujenga mahusiano endelevu ya biashara.
Maonyesho hayo pia yatawezesha kufanyika kwa mikutano ya wafanyabiashara ambayo
itawakutanisha wauzaji na wanunuzi .
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.