Tuesday, December 24, 2019

SERIKALI YALITAKA SHIRIKA LA MSALABA MWEKUNDU TANZANIA (TRCS) KUENDELEA KUTOA HUDUMA ZA MATIBABU KATIKA KAMBI ZA WAKIMBIZI MKOANI KIGOMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji K. Mnyepe ametoa msimamo huo wa Serikali alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bw. George Kuchio katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Aidha, Dkt. Mnyepe ameitaka UNHCR kuzingatia na kuheshimu makubaliano baina yake na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1991 hususani Ibara ya Pili na ya Tatu (Articles II & III). Ibara hizo zinaelekeza kwamba UNHCR ni lazima ishirikiane na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutekeleza majukumu yake hapa Nchini.

Hivi karibuni UNHCR ililitaka Shirika la Msalaba mwekendu Tanzania (TRCS) kukabidhi majukumu yao bila kuihusisha serikali. Hatua hiyo ya UNHCR inavunja makubaliano ya 1991.

Hivyo amewaeleza UNHCR kwamba Shirika la Msalaba mwekundu Tanzania kuendelea na majukumu yake kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo mpaka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na UNHCR watakapokubaliana vinginevyo.




Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe (kulia) akimsisitiza Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bw. George Kuchio, kuzingatia na kuheshimu makubaliano baina UNHCR na Serikali ya Tanzania ya mwaka 1991. Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe (kulia) akimueleza jambo Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bw. George Kuchio. Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.


Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bw. George Kuchio (kushoto) akimueleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe wakati wa mazungumzo katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.