|
Watalii kutoka nchini Israel walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) watalii hao wako nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii nchini wakati huu wa Siku Kuu za Krismasi na Mwaka mpya. |
|
Watalii
kutoka nchini Israel wakiingia ndani ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Kilimanjaro (KIA) baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya kutembelea
vivutio vya utalii wakati wa mapumziko ya mwisho wa mwaka na Siku Kuu za Krismasi na Mwaka
mpya
|
|
Watalii
kutoka nchini Israel wakielekea sehemu maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya mapokezi yao baada ya kuwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Kilimanjaro (KIA) watalii hao wako nchini kwa ajili ya kutembelea
vivutio vya utalii nchini wakati wa mapumziko ya mwisho wa Mwaka na Siku Kuu za Krismasi na Mwaka
mpya wa 2020.
|
|
Watalii
kutoka nchini Israel wakiwa ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Kilimanjaro (KIA) baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya kutembelea
vivutio vya utalii wakati wa Siku Kuu za Krismasi na Mwaka
mpya wa 2020.
|
|
Kikundi cha ngoma cha Kimasai kikiwa ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kutumbuiza wakati wa hafla ya kuwapokea Watalii
kutoka nchini Israel waliowasili nchini kwa ajili ya kutembelea
vivutio vya utali. |
|
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Jaji Mst. Mhe. Thomas Mihayo (wa pili kulia) akiwa na Mkurugrenzi Mtendaji wa TTB Bi Devota Mdachi wa (kwanza kushoto) wakiwa na baadhi ya watalii kutoka nchini Israel mara baada ya kuwapokea katika Uwanja wa KIA walipowasili nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii. |
Watalii zaidi ya 450 kutoka
Israel wamewasili nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio vya kitalii
vilivyoko kaskazini mwa Tanzania. Watalii hao wamekuja nchini kwa kutumia ndege
binafsi na za kawaida.
Kundi la kwanza la
watalii 150 liliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) tarehe 21
Desemba 2019 na kupokelewa na Bodi ya Utalii nchini (TTB) na baadaye kuelekea
katika vivutio vya utalii vilivyoko mkoani Arusha.
Kundi la pili na la tatu
lililokuwa na watalii 313 limewasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege KIA tarehe 24 Desemba 2019.
Watalii hao wako nchini
kwa ajili ya kusherehekea sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya wanatembelea
Hifadhi za Taifa za Serengeti, Tarangire, Ziwa Manyara, Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorogoro na Bonde la Eyasi.
Ubalozi wa Tanzania
nchini Israel umetoa viza zaidi ya 500 kwa Waisrael ambao wamepanga kuwasili
nchini kwa kutumia Mashirika ya Ndege ya Ethiopia, Uturuki na Uswisi katika
kipindi hiki cha siku kuu za mwisho wa mwaka
huku ukiendelea kuratibu ziara nyingine ya watalii zaidi ya 800 ambao
mchakato wa safari yao upo katika hatua za mwisho.
Ujio wa watalii hao
unatokana na jitihada za kuvutia watalii zinazofanywa na Ofisi ya Ubalozi nchini
Israel kwa kushirikiana na makampuni ya wakala wa utalii ya ndani na nje ya
nchi ili kuunga mkono harakati za Serikali za kukuza pato la taifa kupitia
utalii na hivyo kuiletea nchi maendeleo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.