Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo
na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini
Dar es Salaam ambapo Waziri Kabudi amemueleza Mhe. Balozi Clavier kuwa,
uhusiano baina ya Tanzania na Ufaransa ni wa muda mrefu ambapo hadi sasa
Tanzania imekuwa na mahusiano imara na taifa hilo.
Aidha, pamoja na mambo mengine,
mazungumzo yao yalijikita katika kuongeza ushirikiano baina ya Tanzania na
Ufaransa, kuongeza ushirikino wa maendeleo, kuimarisha uwekezaji, biashara
pamoja na kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama.
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic
Clavier akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati balozi huyo alipokutana na
Mhe. Waziri leo katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimuelezea jambo Balozi wa
Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier wakati alipokutana na balozi
huyo leo katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam
|
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimsisitiza jambo Balozi wa
Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier wakati alipokutana na balozi
huyo leo katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam
|
|
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic
Clavier akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati balozi huyo alipokutana na
Mhe. Waziri leo katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akipokea zawadi kutoka kwa Balozi
wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.