Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, kesho tarehe 15 Desemba
2019, anatarajiwa kufungua rasmi Kongamano la sita la Diaspora Tanzania mjini
Zanzibar.
Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi -Zanzibar wamekuwa wakiandaa makongamano ya Disapora kwa kuwakutanisha
kila mwaka Watanzania waishio ughaibuni kujadili mambo mbalimbali ikiwemo
masuala ya uwekezaji, Utalii, Kilimo na mengine ya maendeleo.
Kongamano hili ni
muendelezo wa makongamano mengine matano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam,
Unguja na Pemba katika miaka ya kuanzia 2014 hadi 2018.
Lengo la kongamano hili la
sita ni kuhamasisha na kushirikisha Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini.
Dhamira ya kongamano hili kuendeleza
ushirikiano uliopangwa na Diaspora na wawekezaji kama wadau wa maendeleo nchini
chini ya kauli mbiu ya "mtu kwao
ndio ngao".
Kongamano hili linatarajiwa
kuwa na washiriki zaidi ya 350 wakiwemo Diaspora, Viongozi wa Kitaifa, Wadau
mbalimbali kutoka Serikalini na Sekta Binafsi ambapo pamoja na mambo mengine,
watajadili mazingira ya uwekezaji na fursa za uwekezaji na utalii ziliopo
nchini.
Leo tarehe 14 Desemba 2019
Diaspora na wadau wengine waliowasili wanafanya ziara ya kutembelea vivutio
mbalimbali vya utalii ikiwa ni pamoja na Zanzibar Village Icon na mashamba ya
viungo mbalimbali vya chakula.
Mwezi Augusti, 2018 watanzania
waishio ughaibuni (Diaspora) walikutana Chake Chake, kisiwani Pemba katika kongamano
la tano la Diaspora kufuatia utaratibu
uliowekwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kuwakutanisha kila mwaka Watanzania waishio
ughaibuni.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.