Serikali ya Tanzania
imeahidi kuendeleza ushirikiano wake na Falme za Kiarabu (UAE) katika sekta za
biashara, miradi ya maendeleo, utalii, utamaduni, usafirishaji, kilimo na afya.
Akiongea katika
maadhimisho ya 48 ya Falme za Kiarabu (UAE) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
jana Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.
Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa ili kukuza na kuendeleza ushirikiano
baina ya nchi hizo mbili ni muhimu pia kupanua maeneo ya ushirikiano kati ya
nchi zetu mbili hyaakiwemo ya utalii, kilimo na miradi mbalimbali ya maendeleo.
"Tayari tumeanza
maandalizi ya mkutano wa pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC)
kati ya Tanzania na Falme za Kiarabu (UAE) ambao utafanyika hapa nchini
Tanzania mwaka 2020, baada ya mkutano wa kwanza wa JPC ambao ulifanyika Desemba
2016 Abu Dhabi wakati ambao, makubaliano hayo yalipo sainiwa," Amesema
Prof. Kabudi
Prof. Kabudi aliongeza
kuwa, makubaliano hayo yaliyosainiwa Abu Dhabi ni pamoja na Mkataba wa Ushirikiano kwenye Huduma za Usafiri wa Anga (BASA) na Mkataba wa ushirikiano katika sekta ya Utalii.
Tunatarajia kupanua wigo wa ushirikiano wetu katika mkutano ujao wa JPC.
Kama moja ya Makati wa
uwekezaji, tuko tayari kuhakikisha kuwa wawekezaji wanawekeza Tanzania. Aidha,
mbali na maboresho ya mfumo wa udhibiti wa biashara Tanzania 'Blue Print' yaliyoanza
Julai, 2019, tunafanya mashauriano ya ndani mkataba wa kuepusha na na tozo za
ushuru mara mbili; na makubaliano ya mkataba wa pamoja juu ya kukuza na
kuendeleza ulinzi wa uwekezaji aambapo kwa makubaliano haya ni chanzo cha Falme
za Kiarabu (UAE) kuwekeza Tanzania.
"UAE imekuwa
ikisaidia katika ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kusaidia
juhudi za Tanzania kufikia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kama vile ufadhili
wa ujenzi wa barabara kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi (ADFD). Ni matumaini
yangu kuwa Mfuko utaendeleza usaidizi na kuelekeza miradi mingine ya maendeleo,"
Amesema Prof. Kabudi.
Kwa upande wake, Kwa
upande wake, Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Balozi, Khalifa
Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi amesema kuwa Falme za Kiarabu zitaendeleza
ushirikiano baina yake na Tanzania kindugu, kidiplomasia, kiuchumi na kuhakikisha
kuwa ni wa kudumu.
"Napenda kuwafahamisha
kuwa Falme za Kiarabu (UAE) utaendelea kuwekeza hapa nchini Tanzania ikiwa ni
ishara ya kukuza uchumi. Tutaendelea kuwaeleza wawekezaji fursa zilizopo
Tanzania ili waendelee kuja kuwekeza" Amesema Balozi, Mohamed Al-Marzooqi.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiimba nyimbo za taifa za Tanzania pamoja na ya Falme za Kiarabu (UAE) kabla ya kuanza rasmi kwa maadhimisho |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.