Tuesday, August 31, 2021

UYOGA WA TANZANIA KUPATA SOKO NCHINI UHOLANZI

Balozi Irene Kasyanju (katikati) akiwa katika mazungumzo na uongozi wa LIMAX Group ulioongozwa na Mkurugenzi na Mmiliki wa Kampuni hiyo, Bw. Tom van WALSEM (wa pili kushoto) kuhusu soko la uyoga wa Tanzania nchini Uholanzi kwenye Ofisi za Kampuni hiyo zilizopo katika Mji wa Horst, Uholanzi. LIMAX Group inazalisha faida/pato kwa mwaka (annual turnover) la takriban Euro milioni 25. 

Balozi Irene Kasyanju (kulia) akiangalia namna uyoga unavyofungashwa kwenye makasha (packaging) tayari kwa kupelekwa sokoni huku akipatiwa maelezo ya mchakato mzima wa ufungaji kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa LIMAX Group, Bw. Rob Menheere (kushoto). Katikati ni Bw. Petro Mahuwi “intern” Mtanzania aliyeongozana na Balozi Kasyanju kwenye ziara hiyo.


Namna kitalu kimoja wapo cha uyoga uliopandwa na ambao unakaribia kuvunwa kinavyoonekana katika moja ya mashamba makubwa 4 ya LIMAX Group iliyoko Horst, Uholanzi.

Balozi Kasyanju (kushoto) akiwa na Mkurugenzi na Mmiliki wa LIMAX Group, Bw. Tom van WALSEM (wa kwanza kushoto); Mkurugenzi Mwendeshaji, Bw. Rob Menheere (wa pili kushoto); na Meneja Biashara, Bw. Mark Duppen (wa tatu kushoto) wakikamilisha mazungumzo yao baada ya zoezi la kutembelea mashamba ya uyoga mjini Horst, Uholanzi kukamilika.


----------------------------

UYOGA WA TANZANIA KUPATA SOKO NCHINI UHOLANZI

Kampuni maarufu ya Uholanzi, LIMAX B.V. (LimaxGroup) imedhamiria kuwekeza kwenye Sekta ya Uyoga nchini Tanzania kwa kujenga kiwanda cha kusindika na kukausha uyoga Mkoani Iringa kwa thamani ya Euro milioni 2.1 ambazo ni sawa na Shilingi Bilioni 5.5 za Tanzania. Hayo yameelezwa kufuatia Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju kutembelea kampuni hiyo tarehe 26 Agosti 2021 na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi na Mmiliki wa kampuni hiyo, Bw. Tom VanWalsem.

Balozi Kasyanju alieleza kuwa uwekezaji huo utakapokamilika, Tanzania itafaidika kwa kiasi kikubwa kutokana na mtiririko wa biashara ya uyoga kukua kwa kasi duniani ambapo kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), biashara hiyo inakadiriwa kuongezeka hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 62.2 ifikapo mwaka 2023 kutoka Dola za Marekani bilioni 42.4 mwaka 2018.

Balozi Kasyanju aliendelea kueleza kuwa Kilimo cha uyoga ni sekta inayostawi nchini Tanzania na thamani yake ya kila mwaka inakadiriwa kuwa Tsh. Bilioni 4. Hivyo, ni dhahiri kuwa uwekezaji wa LimaxGroup utakuwa na tija kubwa na wazalishaji wa uyoga nchini watafaidika na soko kubwa lililopo katika Jumuiya ya Ulaya likiongozwa na Uholanzi ikifuatiwa na Ujerumani na baadaye Poland.

Balozi Kasyanju akiwa katika kampuni hiyo alipata fursa ya kujionea mashamba ya kisasa ya uyoga unaozalishwa (sio wa asili) na namna zao hilo lenye faida kubwa kwa binadamu linavyosindikwa na kufungashwa (processed and packed) na kuelezea matumaini yake kuwa Tanzania itafaidika na uwezo, uzoefu na utaalam mkubwa wa biashara wa Kampuni  hiyo.

“Tanzania ni nchi yenye maeneo makubwa ya misitu yenye aina anuwai ya uyoga wa porini kwa ajili ya kula, na jamii zimekuwa zinategemea maarifa asilia kukusanya uyoga huo kwa matumizi na kuuza katika masoko ya ndani tu. Ni wakati muafaka sasa kufanya kazi pamoja kukuza ukuaji wa sekta hii kibiashara”., Balozi Kasyanju alisema.

LIMAXGroup itatoa mafunzo ya kuhifadhi na kuvuna uyoga wa porini kwa madhumuni ya biashara na kulinda mazingira pia. Aidha, ujenzi wa kiwanda hicho mkoani Iringa kutawawezesha wakulima kuuza uyoga wanaozalisha moja kwa moja kiwandani, kuongeza ajira kwa Watanzania na kukuza mnyororo wa thamani wa kilimo cha uyoga nchini. 


Saturday, August 28, 2021

BALOZI LIBERATA MULAMULA KATIKA KIKAO KAZI NA MAAFISA WA UBALOZI WA KUDUMU KATIKA UMOJA WA MATAIFA - NEW YORK, MAREKANI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika kikao kazi na watumishi wa Uwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa New York,Marekani(hawapo pichani)

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika kikao kazi na watumishi wa Uwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa New York,Marekani; kushoto kwa Balozi Mulamula ni Balozi wa Tanzania  katika umoja wa Mataifa Balozi Kennedy Gastorn.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika kikao kazi na watumishi wa Uwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa New York,Marekani

Baadhi ya Maafisa katika Ubalozi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa New York,Marekani wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb)

 

BALOZI MULAMULA AKIZUNGUMZA NA MHE. FLEMMING MOLLER MORTNSEN KWA NJIA YA MTANDAO KUHUSU UAMUZI WA KUFUNGA SHUGHULI ZA UBALOZI WA DENMARK

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza kwa nia ya mtandao (video conferencing) na Waziri Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Flemming Moller Mortensen kuhusu hamuzi wa Denmark kufunga shughuli za Ubalozi wake Nchini Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza kwa njia ya mtandao (video conferencing) na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Flemming Moller Mortensen kuhusu uamuzi wa Denmark kufunga shughuli za Ubalozi wake Nchini Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya Balozi Swahiba Mndeme (kushoto kwa Balozi Mulamula) pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bi. Jean Msabila wakati wa mazungumzo kwa njia ya mtandao na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Flemming Moller Mortensen kuhusu uamuzi wa Denmark kufunga shughuli za Ubalozi wake Nchini Tanzania

 

Friday, August 27, 2021

BALOZI SOKOINE AKUTANA NA BALOZI WA INDIA, ALGERIA NA SWEDEN

 Na Mwandishi wetu, Dar 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Balozi Sokoine amekutana kwa nyakati tofauti na mabalozi hao ambao ni Balozi wa India hapa nchini Mhe. Binaya Pradhan, Balozi wa Algeria hapa nchini Mhe. Ahmed Djellal pamoja na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Anders Sjöberg.

Pamoja na Mambo mengine viongozi hao wamejadili masuala ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia ulipo baina ya Tanzania na mataifa hayo ambapo awali Balozi wa India Mhe. Pradhan ameahidi kuendeleza na kudumisha uhusiano mzuri uliopo baina ya India na Tanzania.

“Nimemhakikishia Katibu Mkuu, Mheshimiwa Balozi Sokoine kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia uliopo baina ya mataifa yetu kwa maslahi ya pande zote mbili katika sekta mbalimbali ikiwemo Utalii, elimu, gesi, biashara na uwekezaji,” amesema Balozi Pradhan

Kwa upande wake, Balozi wa Algeria hapa nchini, Mhe. Djellal amesema kuwa mazungumzo yao yaligusia masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Algeria na Tanzania.

“Tumekubaliana kuendelea kuimarisha diplomasia baina ya mataifa yetu kwa maslahi mapana……….na kwa maendeleo ya wananchi wetu,” amesema Balozi Djellal     

Nae balozi wa Sweden hapa nchini Mhe. Sjöberg amesema katika jitihada za kuendeleza uhusiano wa Sweden na Tanzania, Sweden itaendelea kushirikiana na Tanzania kuendeleza sekta mbalimbali kwa manufaa ya pande zote mbili. 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Sokoine amewahakikishia mabalozi hao ushirikiano wa kutosha kutoka Tanzania.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiongea na Balozi wa India hapa nchini Mhe. Binaya Pradhan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Balozi wa Algeria hapa nchini Mhe. Ahmed Djellal akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Balozi wa Sweden nchini Mhe. Anders Sjöberg akimueleza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es SalaamThursday, August 26, 2021

MABALOZI WAWASILISHA HATI KWA RAIS SAMIA

 

Balozi wa Jamhuri ya Colombia mwenye makazi yake nchini Kenya Mhe. Monica Greiff Lindo akiwasilisha Hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam Agosti 26, 2021Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Colombia nchini nchini Mhe. Monica Greiff Lindo baada ya kupokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi huyo Ikulu Jijini Dar es Salaam Agosti 26,2021

Balozi wa Jamhuri ya Australia nchini mwenye makazi yake nchini Kenya Mhe. Luke Joseph Williams akiwasilisha Hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam Agosti 26, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Australia hapa nchini Mhe. Luke Joseph Williams baada ya kupokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi huyo Ikulu Jijini Dar es Salaam  Agosti 26,2021


Balozi wa Jamhuri ya Czech mwenye makazi yake nchini Kenya Mhe. Martin Kleptiko akiwasilisha Hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam Agosti 26, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Czech hapa nchini Mhe. Martin Kleptiko, mara baada ya kupokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi huyo Ikulu Jijini Dar es Salaam  Agosti 26,2021

 

Balozi wa Chile mwenye makazi yake nchini Kenya Mhe. Maria Alejendra Ferraz de Andrade akiwasilisha Hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam Agosti 26, 2021


Balozi wa Belarus mwenye makazi yake nchini Kenya Mhe. Pavel Vziatkin akiwasilisha Hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam Agosti 26, 2021