Sunday, May 31, 2020

Awamu ya Pili ya Watanzania warejea nchini kutoka India kutokana na ugonjwa wa COVID-19

Baadhi ya watanzania waliokuwa wamekwama India kutokana na ugonjwa wa COVID-19 wakiwa ndani ya ndege maalum ya Air Tanzania wakisubiri kuondoka kurejea Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chhatrapati Shivaji Jijini Mumbai tarehe 30 Mei 2020. Serikali ya India ilisitisha huduma ya kuingia na kutoka kwa ndege za kimataifa ikiwa ni moja ya mkakati wa kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa COVID-19.
Sehemu nyingine ya watanzania waliokuwa wamekwama nchini India wakiwa ndani ya ndege maalum ya Air Tanzania wakisubiri kuondoka kurejea Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chhatrapati Shivaji Jijini Mumbai tarehe 30 Mei 2020.

Baadhi ya watanzania waliokuwa wamekwama India wakisubiri kuingia katika ndege maalum ya Air Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chhatrapati Shivaji Jijini Mumbai tarehe 30 Mei 2020.

Ndege  aina ya Boeng 787-8 ya Dreamliner ya Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) ikipakia watanzania 119 waliokuwa wamekwama nchini India katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chhatrapati Shivaji Jijini Mumbai tarehe 30 Mei 2020.
================================================
Serikali yarejesha kwa awamu ya pili Watanzania 192 waliokuwa wamekwama nchini India kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19
Ubalozi wa Tanzania nchini India kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Tanzania [ATCL] pamoja na Diaspora wa Tanzania nchini India kwa mara nyingine wamefanikisha safari ya pili ya kuwarejesha nchini Watanzania 192 waliokuwa wamekwama katika miji mbalimbali nchini India. Watanzania hao walikwama kutokana na zuio la kuingia na kutoka kwa ndege za Kimataifa lililowekwa na Serikali ya India kama hatua mojawapo ya kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19.
Ndege maalum ya aina ya Boeng 787-8 ya Dreamliner ya Shirika la Ndege la Tanzania ilitumwa tena na Serikali Jijini Mumbai kuja kuwachukua Watanzania hao waliokwama nchini India tangu tarehe 22 Machi 2020 lilipowekwa zuio hilo na Serikali ya India. Ndege hiyo iliondoka tarehe 30 Mei 2020 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chhatrapati Shivaji,  Mumbai ikiwa imebeba jumla ya raia wa Tanzania 192, miongoni mwao ni waliokuwa wamekwenda India kwa ajili ya matibabu; wahitimu kutoka vyuo mbali mbali na wanafunzi ambao wanalazimika kurudi nyumbani kwa kuwa vyuo vimefungwa hadi mwezi Agosti/Septemba 2020.
Tofauti na awamu ya kwanza, safari hii pia ilihusisha kuwarejesha nchini India raia wa nchi hiyo wapatao 202 ambao walikuwa wamekwama nchini Tanzania. Hatua hii ya Serikali ya Tanzania itasaidia sana katika kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo kati ya India na Tanzania.
Mpaka sasa jumla ya Watanzania 438 wamerejeshwa Tanzania kutoka India kwa utaratibu huu maalum. 

Friday, May 29, 2020

PROF. KABUDI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ITALIA NCHINI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, ambapo walijadili masuala mbalimbali yanayohusu mahusiano baina ya Tanzania na Italia.

Aidha, walitumia mazungumzo hayo kujadili hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania pamoja na Serikali ya Italia katika kupambana na ugonjwa wa COVID-19. Mhe. Waziri alifahamisha kuwa hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ya Tanzania kwenye mapambano ya ugonjwa huo zimezingatia mazingiria na hali halisi ya Tanzania pamoja na nchi jirani zinazozunguka Tanzania.

Kwa upande wake Balozi Mengoni alipongeza juhudi hizo za Serikali ambapo alifahamisha kuwa Serikali yake ya Italia inaziunga mkono na kwamba ipo tayari kutoa ushirikiano pale itakapohitajika kufanya hivyo.

Viongozi hao walikubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kihistoria baina ya Mataifa hayo mawili ambao umejikita katika sekta za elimu, afya, utalii pamoja na biashara na uwekezaji.


Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akimuelezea jambo Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akimuelezea jambo Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge




PROF. KABUDI ATAKA NCHI ZA SADC KUIMARISHA USHIRIKIANO




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof Palamagamba kabudi (Mb) (wa kwanza kushoto) akiongea na wajumbe wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam 


Baadhi ya Mawaziri pamoja na maafisa waandamizi/ makatibu wakuu wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam 


Baadhi ya maafisa waandamizi/ makatibu wakuu wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam 
Baadhi ya mawaziri wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mkutano huo


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof Palamagamba Kabudi amezitaka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuimarisha ushirikiano na umoja wakati huu wa kuenea kwa janga la  Virusi vya Corona huku bidhaa na huduma muhimu zinazovuka mipaka baina ya nchi na zikiendelea kutolewa.

Prof. Kabudi amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa njia ya Video katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Nawaomba Nchi zote Wanachama wa SADC tuimarishe umoja na mshikamano wetu wakati huu wa kuenea kwa janga la Virusi vya Corona, huku bidhaa na huduma muhimu zinazovuka mipaka baina ya nchi nan chi zikiendelea kutolewa, huu ni wakati wa kuepuka vitendo vya kujitenga na kuongeza mashauriano baina ya nchi,” amesema.

Aidh Mhe Waziri ameziomba Nchi za SADC kuwapa heshima na kuthamini utu wa madereva wanaosafirisha bidhaa na huduma muhimu kuvuka mipaka ya nchi kwa wakati huu ambao ugonjwa wa corona umeenea katika nchi wanachama.

Amesema Nchi wanachama zinapaswa kuchukua hatua za kukabiliana na ueneaji wa virusi vya Corona bila ya kuwanyanyapaa madereva na kuwachukulia kama watu wanaosambaza virusi hivyo na kuongeza kuwa madereva hao wanapaswa kupewa heshima stahiki kama binadamu wengine na kuwashukuru kutokana na hatari wanayochukua ya kusafirisha mizigo na huduma wakati huu wa kuenea kwa janga hilo.

“Madereva wetu wamevunjika moyo kwa sababu wanaonekana kama wao ndio wanaosambaza virusi vya Corona na sio askari wazuri ambao wanatoa huduma ya kusafirisha huduma na biidhaa muhimu wakati huu wa mlipuko, katika nchi za jumuiya,”

Ameziomba nchi za SADC kuwapa heshima na kuthamini utu wa madereva hao huku zikiendelea kuchukua tahadhari za kupambana na janga la virusi vya corona na kuongeza kuwa umoja wetu ni muhimu sana kwa wakati huu.

“Naziomba nchi zetu tuwape heshima na kuthamini utu wa madereva hao na kuwapa heshima wanayostahili huku tukiendelea kuchukua tahadhari zinazotolewa na wataalamu wa afya katika kukabiliana na janga hilo,” alisema.

Prof. Kabudi amesema janga la COVID 19 linaonekana kama halitoisha ndani ya muda mfupi na nchi za ukanda wa SADC lazima ziishi  kwa kufuata mifumo salama katika biashara na usafirishaji wa huduma na bidhaa ili kupata ukuaji wa uchumi na kuondoa umasikini huku tukiwa bado tunakabiliana na janga hili la ueneaji wa virusi vya corona.

Amesema wakati hatua za kukabiliana na janga la Corona zikiendelea kuchukuliwa nchi za SADC lazima zikumbuke dhumuni la utangamano miongoni mwa nchi wanachama ambalo ni kuboresha ufanyaji biashara baina ya nchi na nchi na hivyo kutowaangusha waanzilishi wa Jumuiya ya SADC.

Amesema ufanyaji wa biashara baina ya nchi na nchi ndani ya SADC uko chini ya asilimia 20 hali ambayo inazuia nchi wanachama kuona ukuaji wa uchumi wake na kuongeza kuwa janga la corona lichukuliwe kama chachu ya kuongeza juhudi za kuinua kiwango cha ufanyaji biashara baina ya nchi na nchi kupitia utekelezajia wa Protokali ya SADC katika biashara ya 2005 na uanzishwaji wa eneo huru la biashara la SADC.

Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la SADC Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Isack Kamwele na Waziri wa Maliasilia na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala. 


Thursday, May 28, 2020

PROF. KABUDI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MABALOZI WA UFARANSA, UTURUKI NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Pamalagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Frederic Clavier ambapo pamoja na mambo mengine, Balozi Clavier ameipongeza Tanzania kwa hatua ilizochukua kupambana na janga a virusi vya corona nchini.

Balozi Clavier pia amemhakikishia Mhe. Waziri kuwa Ufaransa inaiunga mkono Tanzania kwa asilimia 100 kwa hatua ilizochukua kupambana na janga la virusi vya corona na kusema Ufaransa itaipatia Tanzania Euro milioni 30 ikiwa ni mkopo wenye masharti nafuu na riba ndogo kwa ajili ya kupambana na janga la virusi vya Corona pamoja na kusaidia kuinua uchumi.

Katika mazungumzo yao, Mhe. Waziri Kabudi amemuelezea Balozi wa Ufaransa jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kupambana na Janga la Corona nchini na kumhakikishia utayari wa Tanzania katika kupambana na janga hilo na kuongeza kuwa Serikali ya Tanzania ilichukua hatua hizo kulingana na hali halisi ya maisha ya watanzania.

Prof. Kabudi amesema hatua zilizochukuliwa na Tanzania zililenga kuwafanya watanzania kuendelea na maisha yao bila ya kuathiriwa kiuchumi huku wakijilinda na kuchukua tahadhari ambazo zilikuwa zikitolewa na wataalamu wa afya nchini na duniani.

Balozi Clavier amemuambia Mhe. Waziri Kabudi kuwa Ufaransa pia imetoa msaada wa Dola 500,000 ambazo watapewa wakulima wadogowadogo 6,000 nchini kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha kilimo chao na maghala ya kuhifadhia mazao yao.

Ameongeza kuwa Rais wa Ufaransa ameziandikia nchi za G20 na Paris Club kuzishawishi kuahirisha ulipaji wa madeni na riba zake na pia kufuta kabisa madeni hayo ili kuimarisha uchumi ambao umeathiriwa na janga la corona katika nchi zinazoendelea.

Katika hatua nyingine, Waziri Kabudi amekutana na kuagana na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Ali Davutaglu ambaye amemaliza muda wake wa utumishi na amemtakia maisha mema na kumwambia kuwa ni matarajio yake kuwa atakuwa Balozi wa hiari wa Tanzania nchini uturuki na kwingineko duniani.

Naye balozi Davotaglu ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano ambao imekuwa ikimpatia alipokuwa akitekeleza majukumu yake nchini na kuahidi kuwa ushirikiano uliopo utaendelezwa hasa ikizingatiwa kuwa. 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akipokea zawadi ya kitabu cha Mwl. Nyerere kutoka kwa Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimuelezea jambo Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Frederic Clavier wakati alipokutana na balozi huyo leo katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam


Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Frederic Clavier akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati balozi huyo alipokutana na Mhe. Waziri leo katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na Balozi wa Uturuki nchini ambaye amemaliza muda wake wa utumishi, Mhe. Balozi Ali Davutaglu wakati walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Balozi Ali Davutaglu akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) pamoja na Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Balozi Ali Davutaglu wakiangalia picha ya kazi zilizofanywa na Ubalozi wa Uturuki wakati walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya picha Balozi wa Uturuki nchini aliyemaliza muda wake wa utumishi, Mhe. Balozi Ali Davutaglu 


Wednesday, May 27, 2020

SADC: NGAZI YA MAKATIBU WAKUU WAPENDEKEZA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA MIPAKANI


Makatibu Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wamependekeza kuruhusu Biashara za bidhaa zote kuendelea kusafirishwa katika Nchi zao kama ilivyokuwa kabla ya janga la Virusi vya Corona.

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa ngazi ya Mkatibu Wakuu uliofanyika kwa njia ya Mtandao (video conference) leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Makatibu Wakuu amesema mkutano huo umejadili na kutoa mapendekezo ya kuondoa vikwazo vyote vya kibiashara ili kuweza kuendeleza uchumi ndani ya Jumuiya.

Balozi Ibuge amesema kuwa uamuzi huo utawawezesha wananchi kuendelea na maisha yao ya kawaida na biashara zao kwa kuwa janga la COVID 19 litaendelea kuwepo kwa muda ambao ukomo wake haujulikani japo juhudi za kuukabili ugonjwa huo zinaendelea.

“Kikao cha makatibu cha makatibu wakuu cha leo, kimependekeza  kuondoa kikwazo cha bidhaa mahususi tu kupita katika mipaka yetu badala yake bidhaa zote zinazowezesha wananchi wetu kuendelea na maisha ni lazima ziruhusiwe kupita katika mipaka ya nchi wanachama wa SADC” Amesema Balozi Ibuge.

Aidha, Katibu Mkuu ameongeza kuwa ni muhimu wa wanaSADC kujumuika katika wakati huu na kuona ni jinsi gani wanaweza kushirikiana na kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi wanachama wa SADC unakua kwa kuongeza juhudi katika sekta ya biashara. 
  
Balozi Ibuge ameongeza kuwa “kwa mfano halisi sisi kama Tanzania hatukufunga mipaka yetu, na katika kutokufunga mipaka yetu bado tunatambua kwamba tunaendelea kuwategemea wenzetu kama wanavyotutegemea sisi............tuna badari inayohudumia nchi nane za SADC na zisizokuwa za SADC na ambazo ndizo hasa tunapozungumzia utengamano na mazingiara ya kufanya biashara na kuzingataia tahadhari mbalimbali za uonjwa wa COVID 19 ambazo nchi hizo zimekuwa zikichukua,"

Aidha, Mkutano huu pia umejadili hali ya kifedha ndani ya Jumuiya, Utekelezaji wa Maazimio yaliyotokana na kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC ambayo ni Menejimenti ya Maafa, utekelezaji wa kaulimbiu ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC isemayo "Mazingira Wezeshi kwa ajili ya Maendeleo Endelevu na Jumuishi ya Viwanda, Kukuza Biashara na Ajira ndani ya SADC" na mapitio ya hali halisi ya biashara baina ya nchi, maendeleo ya viwanda ndani ya Jumuiya na taarifa ya utekelezaji wa Mkakati wa Maendeleo ya Viwanda wa Jumuiya na Mpango kazi wake.

Mkutano huo umahusisha wataalamu kutoka nchi wanachama 12 wa SADC kutoka sekta za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Fedha na Mipango, Uchukuzi na Mawasiliano, Viwanda na Biashara, Maliasili na Utalii pamoja na Afya. Mkutano huo pia utatoka na maazimio ambayo nchi wanachama watatakiwa kuyatekeleza ndani ya muda utakaokubaliwa.

Nchi zilizoshiriki Mkutano huo ni pamoja na Angola, Afrika Kusini, Comoro, Eswatini, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia, Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Zimbabwe na Mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa ngazi ya Mkatibu Wakuu uliofanyika kwa njia ya Mtandao (video conference) leo jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge (wa kwanza meza kuu kushoto) akiongea na wajumbe wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa ngazi ya Mkatibu Wakuu uliofanyika kwa njia ya Mtandao (video conference) leo jijini Dar es Salaam





MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA SADC NGAZI YA MAKATIBU WAKUU WAANZA


 Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umefanyika leo jijini Dar es Salaam kwa njia ya Mtandao (Video Conferencing) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) 
Mkutano huo umefunguliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Maafisa Waandamizi/ Makatibu Wakuu, Balozi Kanali Wilbert Ibuge Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Wajumbe wengine ni waliohudhuria ni Katibu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Prof. Abel Makubi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utaii Dkt. Aloyce Nzuki pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipago, Bi Amina K. Shaaban.
Mkutano wa Baraza la Mawaziri utafanyika Mei 29, 2020 baada ya kukamilika kwa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Maafisa Waandamizi/Makatibu Wakuu ambapo pamoja na mambo menine, Kikao cha Maafisa waandamizi kimejadili masuala mbalimbali ndani ya Jumuiya ikiwemo Mlipuko wa Virusi vya Corona ndani ya SADC.
Mkutano huo utaangalia utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri kilichofanyika mwezi Aprili 2020 kuhusu COVID 19 na athari zake katika utekelezaji wa programu za SADC, athari za kijamii na kiuchumi za COVID -19 na madhara yake ndani ya Jumuiya.
Aidha, Mkutano huu pia umejadili Hali ya kifedha ndani ya Jumuiya, Utekelezaji wa Maazimio yaliyotokana na kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC ambayo ni Menejimenti ya Maafa, utekelezaji wa kaulimbiu ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC isemayo "Mazingira Wezeshi kwa ajili ya Maendeleo Endelevu na Jumuishi ya Viwanda, Kukuza Biashara na Ajira ndani ya SADC" na mapitio ya hali halisi ya biashara baina ya nchi, maendeleo ya viwanda ndani ya Jumuiya na taarifa ya utekelezaji wa Mkakati wa Maendeleo ya Viwanda wa Jumuiya na Mpango kazi wake.
Mkutano huo umehusisha wataalamu kutoka nchi  wanachama 12 wa SADC kutoka sekta za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Fedha na Mipango, Uchukuzi na Mawasiliano, Viwanda na Biashara, Maliasili na Utalii pamoja na Afya.
Nchi zilizoshiriki Mkutano huo ni Angola, Afrika Kusini, Comoro, Eswatini, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia, Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Zimbabwe na Mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge (kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bi. Agnes Kayola wakati akifungua mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam  

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge (aliyevaa koti jeusi) akiongea na wajumbe wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa ngazi ya Makatibu Wakuu kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam  

Baadhi ya Makatibu Wakuu wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya Maafisa waandamizi wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam  

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge akisisitiza jambo kwa wajumbe wa mkutano (hawapo pichani). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bi. Agnes Kayola    

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge (wa kwanza meza kuu kushoto) akiongea na wajumbe wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam  




Tuesday, May 26, 2020

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



KAIMU BALOZI WA MAREKANI DKT. IMNI PATTERSON AITWA WIZARANI KWA UFAFANUZI

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akisalimiana na Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt mni Patterson. Kaimu Balozi huyo ameitwa Wizarani kwa lengo la kutoa ufafanuzi masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho.Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiwa katika mazungumzo na Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt mni Patterson. Kaimu Balozi huyo ameitwa Wizarani kwa lengo la kutoa ufafanuzi masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho. Mazungumzo haYo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt Imni Patterson akizungumza wakati alipokutana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge. Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akimsikiliza Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt Imni Patterson. Kaimu Balozi huyo ameitwa Wizarani kwa lengo la kutoa ufafanuzi masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho. Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam

Sunday, May 24, 2020

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akitoa salam za shukrani kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Albano,Dayosisi ya Dar es Salaam ikiwa ni kilele cha siku tatu ya shukrani kwa Mungu baada ya maambukizi ya virus vya Corona kupungua nchini.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akitoa salam za shukrani kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Albano,Dayosisi ya Dar es Salaam ikiwa ni kilele cha siku tatu ya shukrani kwa Mungu baada ya maambukizi ya virus vya Corona kupungua nchini.

Baadhi ya waumini wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Albano Dayosisi ya Dar es Salaam,wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati akitoa salam za shukrani kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Albano,Dayosisi ya Dar es Salaam ikiwa ni kilele cha siku tatu ya shukrani kwa Mungu baada ya maambukizi ya virus vya Corona kupungua nchini

Thursday, May 21, 2020

WATANZANIA 119 KUTOKA DUBAI WAREJEA NCHINI, KUISHUKURU SERIKALI


Serikali ya Tanzania imewarejesha nchini watanzania 119 ambao walikuwa wamekwama Abu Dhabi (Dubai) kufuatia kuzuiwa kwa safari za ndege kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosabishwa na virus vya corona (COVID-19).

Ndege ya fly Dubai imewarejesha watanzania hao waliokuwa wamekwama Abu Dhabi (Dubai) tangu 25 Machi 2020 Serikali ya Falme za Kiarabu ilipotoa zuio la kuingia na kutoka kwa ndege.

Ndege hiyo imewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8 mchana leo Alhamisi tarehe 21 Mei 2020 ikiwa na watanzania 119.

Kabla ya ndee hiyo kuwasili katika uwanja wa ndee wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wa watanzania hao walionekana wakiwa na nyuso za furaha na shauku ya kuonana na ndugu zao.

"Tunashukuru Serikali yetu ya Tanzania kwa kuweza kuturejesha nyumbani….binafsi namshukuru sana sana Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi za kuturejesha, pia naushukuru ubalozi wa Tanzania katika Falme za Kiarabu kwa msaada wa hali na mali pamoja na nchi ya Falme za Kiarabu na watanzania kwa umoja na upendo kwani wengine tulikuwa hatuna fedha ya tiketi lakini kwa umoja tumeweza kuchangiwa na kurejea tena nchini kwetu," Amesema Mohhamed Juma Omary.

Kwa Upande wake, Bi. Christina Magige ambaye alikuwa amekwama Dubai kwa miezi mitatu ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Falme za Kiarabu kwa kuweza kutoa ndege ambayo imeweza kuwarejesha nyumbani.

"Nampongeza sana Serikali yanu ya Tanzania kwa kuweza kufungua viwanja vya ndege ambapo kwa kufanya hivyo imetusaidia sisi watanzania tuliokuwa nje ya nchi kuweza kurejea nchini leo tunamshukuru sana, amesema bi. Magige.

Tarehe 15 Mei, 2020 jumla ya watanzania 246 waliokuwa wamekwama katika miji mbalimbali nchini India kutokana na zuio la kuingia na kutoka ndege za Kimataifa lililowekwa na Serikali ya India kama hatua mojawapo ya kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 walirejea nchini.

Ndege ya flydubai iliyowarejesha watanzania 119 nchini kutoka Abu Dhabi (Dubai) ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo jijini Dar es Salaam

Baadhi ya watanzania waliokuwa wamekwama Dubai wakishuka kwenye ndege ya flydubai mara baada ya ndee iyo kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo jijini Dar es Salaam

Baadhi ya watanzania waliokuwa wamekwama Dubai wakishuka kwenye ndege ya flydubai mara baada ya ndee iyo kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo jijini Dar es Salaam

Baadhi ya watanzania waliokuwa wamekwama Dubai wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo jijini Dar es Salaam

Baadhi ya watanzania waliokuwa wamekwama Dubai wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo jijini Dar es Salaam

Baadhi ya watanzania waliokuwa wamekwama Dubai wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo jijini Dar es Salaam