Makatibu Wakuu wa Nchi wanachama wa
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wamependekeza kuruhusu
Biashara za bidhaa zote kuendelea kusafirishwa katika Nchi zao kama ilivyokuwa
kabla ya janga la Virusi vya Corona.
Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua
mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa ngazi ya Mkatibu Wakuu uliofanyika
kwa njia ya Mtandao (video conference) leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali
Wilbert Ibuge ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Makatibu Wakuu amesema
mkutano huo umejadili na kutoa mapendekezo ya kuondoa vikwazo vyote vya kibiashara
ili kuweza kuendeleza uchumi ndani ya Jumuiya.
Balozi Ibuge amesema kuwa uamuzi huo utawawezesha
wananchi kuendelea na maisha yao ya kawaida na biashara zao kwa kuwa janga la
COVID 19 litaendelea kuwepo kwa muda ambao ukomo wake haujulikani japo juhudi
za kuukabili ugonjwa huo zinaendelea.
“Kikao cha makatibu cha makatibu wakuu cha leo, kimependekeza
kuondoa kikwazo cha bidhaa mahususi tu
kupita katika mipaka yetu badala yake bidhaa zote zinazowezesha wananchi wetu
kuendelea na maisha ni lazima ziruhusiwe kupita katika mipaka ya nchi wanachama
wa SADC” Amesema Balozi Ibuge.
Aidha, Katibu Mkuu ameongeza kuwa ni muhimu wa wanaSADC
kujumuika katika wakati huu na kuona ni jinsi gani wanaweza kushirikiana na
kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi wanachama wa SADC unakua kwa kuongeza juhudi katika
sekta ya biashara.
Balozi Ibuge ameongeza kuwa “kwa mfano halisi sisi kama
Tanzania hatukufunga mipaka yetu, na katika kutokufunga mipaka yetu bado
tunatambua kwamba tunaendelea kuwategemea wenzetu kama wanavyotutegemea sisi............tuna
badari inayohudumia nchi nane za SADC na zisizokuwa za SADC na ambazo ndizo
hasa tunapozungumzia utengamano na mazingiara ya kufanya biashara na
kuzingataia tahadhari mbalimbali za uonjwa wa COVID 19 ambazo nchi hizo zimekuwa
zikichukua,"
Aidha, Mkutano huu pia umejadili hali ya kifedha ndani
ya Jumuiya, Utekelezaji wa Maazimio yaliyotokana na kikao cha Baraza la
Mawaziri wa SADC ambayo ni Menejimenti ya Maafa, utekelezaji wa kaulimbiu ya
Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC isemayo "Mazingira Wezeshi kwa ajili ya Maendeleo Endelevu na Jumuishi ya
Viwanda, Kukuza Biashara na Ajira ndani ya SADC" na mapitio ya hali
halisi ya biashara baina ya nchi, maendeleo ya viwanda ndani ya Jumuiya na
taarifa ya utekelezaji wa Mkakati wa Maendeleo ya Viwanda wa Jumuiya na Mpango
kazi wake.
Mkutano huo umahusisha wataalamu kutoka nchi wanachama 12
wa SADC kutoka sekta za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Fedha
na Mipango, Uchukuzi na Mawasiliano, Viwanda na Biashara, Maliasili na Utalii
pamoja na Afya. Mkutano huo pia utatoka na maazimio ambayo nchi wanachama
watatakiwa kuyatekeleza ndani ya muda utakaokubaliwa.
Nchi zilizoshiriki Mkutano huo ni pamoja na Angola,
Afrika Kusini, Comoro, Eswatini, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia,
Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Zimbabwe na Mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali
Wilbert Ibuge waandishi wa habari
mara baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa ngazi ya
Mkatibu Wakuu uliofanyika kwa njia ya Mtandao (video conference) leo jijini Dar
es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.