Saturday, October 28, 2017

Waziri Mahiga azitaka taasisi kutoa fursa za ajira kwa vijana

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga leo ameongea na vijana kupitia kongamano la Ubalozi Youth Forum lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. Waziri Mahiga katika hotuba yake amewataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na Taasisi mbalimbali za Kimataifa na za ndani na makampuni binafsi. Waziri Mahiga amezitaja baadhi ya fursa hizo kuwa ni nafasi za ufadhili wa masomo ya elimu ya juu (scholarship) na mafunzo mbalimbali kama vile ujasiriamali, teknolojia, ajira na biashara.

Kongamano hilo lililenga kuwaelimisha vijana kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye Taasisi za Kimataifa zilizopo nchini na Makampuni binafsi na kuwahamasisha kuchangamkia fursa hizo. Vilevile kongamano hilo lilihudhuriwa na Wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi mbalimbali nchini Tanzania ambapo, vijana walipata fursa ya kuzungumza nao na kujifunza masuala mbalimbali kutoka kwa Wanadiplomasia hao.

Aidha katika Kongamano hilo vijana walipata fursa ya kuonesha bidhaa na huduma mbalimbali walizo zibuni, pia kuonesha bidhaa walizozalisha kutokana na miradi mbalimbali inayofadhili na Mashirika ya kimataifa. Miongoni mwa bidhaa zilizooneshwa ni mazao ya kilimo yaliyofadhiliwa na Umoja wa Mataifa (UN) chini ya mradi wa"ajira stahiki kwa vijana vijijini" (decent rural employment) ambapo hadi sasa jumla ya vijana 480 wamenufaika na mradi huo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifuatilia kongamano la Ubalozi Youth Forum
Sehemu ya Wanadiplomasia kutoa nchi mbalimbali Duniani wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wakifuatila Kongamano


Waziri Mhe.Mahiga akihutubia hadhira ya Ubalozi Youth Forum

Waziri Mhe.Mhiga akiangalia moja ya bidhaa iliyobuniwa na kutengenezwa na kijana kwenye maonesho ya kongamano la Ubalozo Youth Forum yaliyofanyika katika viwanja vya  Leaders Club Jijini Dar es Salaam

Friday, October 27, 2017

Program ya Uendelezaji wa Sekta ya Uchukuzi kwa njia ya Barabara kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya Utatu wa COMESA-EAC-SADC yazinduliwa.

Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbalawa akihutubia katika Mkutano wa Mawaziri wa Uchukuzi na Ujenzi wakati wa uzinduzi rasmi wa Program ya Uendelezaji wa Sekta ya Uchukuzi kwa njia ya Barabara kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC. Mkutano huo ulifanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Oktoba 2017.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Liberat Mfumukeko akihutubia ambapo pamoja na mambo mengine alieleza faida zitakazopatikana kutokana na uzinduzi wa program hiyo na namna Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivyojidhatiti kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa kwa uhakika.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leornard Chamuriho (kulia) pamoja na wajumbe kutoka nchi wanachama wakifuatilia mkutano, wa kwanza kushoto ni Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura
Sehemu ya wajumbe wa Tanzania wakifuatilia mkutano, wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko.
Sehemu ya wajumbe kutoka nchi wanachama wakifuatilia mkutano.
Meza kuu wakiongoza Mkutano.
Mkutano ukiendelea.

Thursday, October 26, 2017

Waziri Mahiga afungua Mkutano wa Mawaziri wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC (TRIPARTITE)

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifungua Mkutano wa kwanza wa Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Miundombinu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC (TRIPARTITE) uliofanyika katika Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Oktober 2017.
Viongozi na wajumbe kutoka Nchi Wanachama wakifuatilia Mkutano, wa tatu kutoka kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbalawa na wa nne kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima.

Sehemu nyingine ya Wajumbe kutoka nchi Wanachama wakifuatilia Mkutano.
Mkutano ukiendelea.

Picha ya pamoja.
============================================================


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MHE. WAZIRI MAHIGA AFUNGUA RASMI MKUTANO WA KWANZA WA MAWAZIRI WENYE DHAMANA YA MASUALA YA MIUNDOMBINU WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA UTATU WA COMESA-EAC-SADC (TRIPARTITE) UNAOFANYIKA HAPA DAR ES SALAAM LEO TAREHE 26 OKTOBA 2017

Mkutano wa Kwanza wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC umefanyika hapa Dar es Salaam, Serena Hoteli leo tarehe 26 Oktoba 2017. Mkutano huo unahusisha jumla ya nchi 26 Wanachama wa Umoja huo. Mkutano huu unafanyika hapa Tanzania kwa kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ndiyo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC.

Mkutano huu umefunguliwa na Mhe. Dkt. Augustine Phillip Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo unaongozwa na Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb), Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Kufanyika kwa Mkutano wa Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Miundombinu kunatokana na maazimio ya Mkutano wa Pili wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa COMESA, EAC na SADC uliofanyika Johannesburg, Afrika Kusini tarehe 14 Juni, 2011 ambao ulipitisha maeneo matatu ya kutekelezwa kwenye ushirikiano wa Utatu wa COMESA – EAC – SADC. Maeneo hayo ni: 1) Kuunganisha Soko; 2) Kuendeleza Miundombinu ili kuunganisha Nchi Wanachama kwa miundombinu iliyo bora; na 3) Kukuza Viwanda.
Kwa upande wa Sekta za Miundombinu, huu ni Mkutano wa Kwanza wa Mawaziri  wa Nchi Wanachama wa Utatu wa COMESA, EAC na SADC. Mkutano huu katika Ngazi ya Wataalam ulijadili hatua zilizofikiwa na Nchi Wanachama katika uendelezaji wa miundombinu na kupendekeza maamuzi ya kisera kwenye sekta za miundombinu ya uchukuzi (barabara, reli, bandari, anga); teknolojia ya habari na mawasiliano; na nishati.

Kwa ujumla Mkutano wa Mawaziri umepita na kujadili programu kuu zifuatazo:
           i.          Programu ya Uendelezaji wa Sekta za Uchukuzi kwa njia ya Barabara kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC (Tripartite Transport and Transit Facilitation Programme (TTTFP);

          ii.          Taarifa za utekelezaji wa miradi na programu kuhusiana na Sekta ya Miundombinu ya Uchukuzi (Anga, Barabara, Reli na Bandari); Sekta ya Mawasiliano na Sekta ya Nishati;

         iii.          Maendeleo ya Kanda za Uchukuzi (Corridor Development) za Jumuiya ya Utatu wa COMESA, EAC na SADC, ambapo hatua mbalimbali za Utekelezaji wa Vituo vya Kutoa Huduma kwa Pamoja Mipakani (OSBPs) kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya hizo zimejadiliwa;

        iv.          Utekelezaji wa Programu ya Kikanda wa Uendelezaji wa Miundombinu katika Ukanda wa Afrika Mashariki, Ukanda wa Afrika Kusini na Ukanda wa Bahari ya Hindi (Regional Indicative Programme for Eastern Africa, Southern Africa and the Indian Ocean (2014 – 2020); na

         v.          Utekelezaji wa Miradi ya NEPAD Presidential Infrastructure Championship Initiative (PICI);
        vi.          Rasimu ya Mpangokazi wa shughuli za utatu wa COMESA- EAC- SADC hususan uratibu wa mikutano ya miundombinu;
       vii.          Utafutaji raslimali fedha za kuwezesha shughuli za utatu wa COMESA- EAC- SADC; na

     viii.          Uzinduzi rasmi wa Programu ya Uendelezaji wa Sekta za Uchukuzi kwa njia ya Barabara kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC (Tripartite Transport and Transit Facilitation Programme (TTTFP).

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Waziri Mahiga, pamoja na kuwakaribisha Mawaziri nchini Tanzania na jijini Dar es Salaam, amesisitiza umuhimu wa kuwa na miradi ya pamoja ya kuendeleza sekta ya miundombinu baina ya Jumuiya za kikanda kama njia madhubuti ya kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi. Mhe. Mahiga pia amesisitiza kwamba Tanzania inathamini ushirikiano wa kanda na hivyo itaendelea kushiriki kikamilifu katika juhudi za maendeleo za kikanda ikiwemo zile za Jumuiya ya Utatu (Tripartite) kama njia mojawapo wa utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda. Mwisho, Mhe. Mahiga amewatakia mkutano mzuri Mawaziri wa Miundombinu akiwaomba kuibua mikakati na mapendekezo madhubuti katika kuendeleza miundombinu katika eneo lote la UTATU.

Aidha, Mawaziri kwa pamoja, wakiongozwa na Mhe. Aggrey Henry Bagiire, Waziri wa Uchukuzi na Ujenzi wa Jamhuri ya Uganda na ambaye atakuwa ni Mwenyekiti wa Mkutano huo kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, watazindua rasmi Programu ya Uendelezaji wa Sekta za Uchukuzi kwa njia ya Barabara kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC (Tripartite Transport and Transit Facilitation Programme (TTTFP).

Uzinduzi huu utafanyika leo tarehe 26 Oktoba, 2017 saa 9.00 Alasiri na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa Serikali na Sekta Binafsi.
I
Imetolewa na,
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI,
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI,
TAREHE 26/10/2017Wednesday, October 25, 2017

Wizara yamtunuku nishani Balozi Kapya

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.Aziz P Mlima (kushoto) akimkabidhi nishani Mhe.Balozi David Kapya kutokana na mchango wake wa kushiriki katika utatuzi wa migogoro  katika sehemu mbalimbali Barani Afrika. Mhe. Balozi Kapya amekabidhiwa nishani hiyo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es  Salaam.

Katibu Mkuu Balozi Dkt.Aziz P Mlima akimpongeza Balozi David Kapya mara baada yakumtunuku nishani kufuatia mchango wake mkubwa wa kushiriki katika utatuzi wa migogoro

Rais Magufuli apokea Hati za Utambulisho za Mabalozi wapya kutoka nchini Oman, Uholanzi na China

Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Oman nchini, Mhe. Ali bin Abdallah bin Salim Al-Mahrooqi mwenye makazi yake Jijini Dar es Salaam. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Mhe. Al-Mahrooqi.
Wakiwa katika mazungumzo ambapo maongezi yao yalijikita katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia sambamba na ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji ambao ndio msingi mkuu wa kuinua uchumi wa mataifa hayo.
Picha ya pamoja.  
Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Grace Martin akimtambulisha Mhe. Al-Mahrooqi kwa Mhe. Rais Magufuli kabla ya kukabidhi Hati za Utambulisho.
Mhe. Al-Mahrooqi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Balozi Al-Mahroooqi akipigiwa Wimbo wa Taifa wa Tanzania na Oman mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.                     
=========================================================

Wakati huohuo Mhe. Rais Magufuli alipokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Uholanzi.


Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Uholanzi nchini, Mhe. Jeroen Verheul mwenye makazi yake Jijini Dar es Salaam. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Itifaki, Balozi Grace Martin akimtambulisha Mhe. Verheul kwa Mhe. Rais Magufuli.    
Picha ya pamoja Viongozi na Maafisa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ubalozi wa Uholanzi nchini.     
Mhe. Waziri Mahiga akimtambulisha Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Mary Matari kwa Mhe. Verheul.
Mhe. Rais Magufuli akizungumza na Balozi wa Uholanzi nchini mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho. 
 
Mhe. Verheul akipigia wimbo wa Taifa wa Tanzania na Uholanzi na bendi ya polisi na baadae aliagana na kiongozi wa bendi hiyo.
====================================================================
Katika nafasi nyingine Mhe. Rais Magufuli alipokea Hati za Utambulisho za Balozi wa China nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho za Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke mwenye makazi yake Jijini Dar es Salaam. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Balozi Grace Martini akimtambulisha Mhe. Wang kwa Mhe. Rais Magufuli kabla ya kukabidhi Hati hizo.
Picha ya pamoja.
Mhe. Wang akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Wangi akiagana na kiongozi wa Bendi ya Polisi mara baada ya kukamilisha hafla ya makabidhiano.

Maadhimisho ya Miaka 72 ya Umoja wa Mataifa yafana

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga mara baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa. Maadhimisho hayo ambayo hufanyika tarehe 24 Oktoba kila mwaka yalibeba kaulimbiu isemayo "Maendeleo ya Viwanda na Utunzaji wa Mazingira kwa Maendeleo Endelevu".
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea heshima ya wimbo wa Taifa wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa.
Wageni waalikwa wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa kwa ajili maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez wakishuhudia upandishwaji wa Bendera ya Umoja wa Mataifa (Flag Raising) ikiwa ni ishara ya kilele cha maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza machache wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez naye akitoa salamu za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa.
Kikundi cha Burudani cha Wanafunzi kutoka Zanzibar kikitumbuiza wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa
Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru wakiimba wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa.
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez akimkabidhi tuzo maalum  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua ushirikiano na mchango wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa.
Mhe. Waziri Mahiga naye akipokea tuzo kutoka kwa Bw. Rodriguez. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Harrison Mwakyembe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.
Maafisa Mambo ya Nje ambao wameshiriki  Maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa wakiwa katika picha ya kumbukumbu
Sehemu nyingine ya Maafisa kutoka Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walioshiriki  maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa.
Watumishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakipata picha ya kumbukumbu wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa