Wednesday, October 30, 2019

NAIBU WAZIRI AONGOZA UJUMBE WA WIZARA KWENYE KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisoma taarifa kwenye kikao kati ya Wizara na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara  Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe

Naibu Waziri Mhe. Dkt. Ndumbaro leo ameongoza ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye kikao kati ya Wizara na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje , Ulinzi na Usalama kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Bunge jijini Dodoma. 
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Musa Azzan Zungu (MB), kwa pamoja wameipongeza Wizara kwa  kutekeleza vyema mapendekezo yaliyotolewa na kamati hiyo katika vikao vilivyopita, sambamba na utekelezaji mzuri wa vipaumbele na malengo ya Wizara.
 
Kikao hicho kilitoa fursa kwa Wizara kuwasilisha kwa kamati taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu yake. Aidha, kikao hicho hutoa fursa kwa kamati kupokea na kujadili taarifa za Wizara pamoja na kutoa mapendekezo yake kuhusu masuala mbalimbali.


Kikao cha Wizara na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kikiendelea.
Sehemu ya Waheshimiwa Wabunge (Wajumbe wa Kamati) wakifuatilia taarifa ya Wizara iliyokuwa ikiwasilishwa wakati wa kikao. 
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Wabunge (Wajumbe wa Kamati) wakifuatilia taarifa ya Wizara iliyokuwa ikiwasilishwa wakati wa kikao. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Musa Azzan Zungu (MB), akichangia jambo wakati wa kikao.
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Wabunge (Wajumbe wa Kamati) wakifuatilia kikao.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB) KUIPATIA TANZANIA ZAIDI YA SHILINGI TRILIONI MOJA KWA AJILI YA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA MSALATO WA JIJINI DODOMA PAMOJA NA BARABARA ZA MZUNGUKO JIJINI HUMO.

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli wa kuhamia Dodoma na kuahidi kuidhinisha kiasi cha dola za kimarekani milioni 455 sawa na zaidi ya shilingi za Kitanzania trilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Msalato sambamba na ujenzi wa barabara za mzunguko Jijini  humo.

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina ameyasema hayo katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo yaliyopo Abijdan Nchini Ivory Coast wakati wa Mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na kuongeza kuwa benki hiyo itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kipindi chake cha Uenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) lakini pia kwa Tanzania.

Amesema Benki hiyo tayari imeshaidhinisha kiasi cha dola za marekani milioni 180 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko jijini  Dodoma na kwamba kiasi kingine cha dola za marekani milioni 275 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato kinatarajiwa kuidhinishwa na mapema mwezi Novemba 2019.

Dkt. Adesina ameongeza kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika ina imani na mageuzi ya kiuchumi yanayotekelezwa chini ya Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma za kijamii ikiwemo elimu bila malipo,afya na maji pamoja na mapambano dhidi ya rushwa na kuleta uwajibikaji katika taaisisi za uma na kwamba iko tayari kuunga jitihada hizo za serikali kwa kuwekeza katika sekta ya miundombinu..

Aidha Dkt. Adesina ameelezea nia yake ya kutaka kushudia bara la Afrika likipiga hatua kubwa za kimaendeleo sasa na kwa haraka na sio kusubiri baadae na kwamba katika kipindi chake cha uongozi katika Benki ya Maendeleo ya Afrika atapambana kuhakikisha azma hiyo inatekelezeka.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa ushirikiano inayoutoa kwa Tanzania hususani katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na rais Dkt. John Pombe Magufuli ambayo kimsingi yalikuwa ni maono ya Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere kwa nia ya kuiwezesha Tanzania kujitegemea kiuchumi na hatimae Bara zima la Afrika.

Prof. Kabudi ameongeza kuwa tayari Benki ya Maendeleo ya Afrika iko tayari kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa yaani standard gauge railway ya kipande cha kutoka Isaka hadi Kigali nchini Rwanda na kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mara baada ya kukamilika mchakato wa utoaji wa fedha hizo ambapo mazungumzo ya awali kuhusu ufadhili huo yameanza.

Pia Prof. Kabudi amemtaka Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt. Akinwumi Adesina kuimarisha ofisi za kanda za benki hiyo ili ziweze kutoa huduma zote za kibenki ili kusogeza huduma karibu na wanufaika wa benki hiyo sambamba na kuunga mkono miradi yote ya kimkakati inayounganisha nchi na nchi katika bara la Afrika ili kuboresha nakurahisisha huduma ya usafiri katika Bara la Afrika na hivyo kuwezesha biashara miongoni mwa nchi za Kiafrika na kujiletea maendeleo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi yuko Abijdan Nchini Ivory Coast kushiriki mkutano wa siku mbili wa dharura wa Mawaziri wa fedha uliondaliwa na Benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB).


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Abidjan - Ivory Coast.
30 OCTOBER 2019



BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB) KUIPATIA TANZANIA ZAIDI YA SHILINGI TRILIONI MOJA KWA AJILI YA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA MSALATO NA BARABARA MZUNGUKO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba  John Kabudi (Mb) akisalimiana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina Makao Makuu ya Benki hiyo yaliyopo Abidjan Nchini Ivory Coast.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba  John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina. Mazungumzo hayo yamefanyika Makao Makuu ya Benki hiyo yaliyopo Abidjan Nchini Ivory Coast.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba  John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina,mara baada mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo yaliyopo Abidjan Nchini Ivory Coast.Wengine katika picha ni viongozi wa AfDB na Afisa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania.


Monday, October 28, 2019

Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC Wafanyika JIANGSU

Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC kutoka Jimbo la Jiangsu umefunguliwa leo jijini Nanjing na Naibu Gavana wa Jimbo hilo Ndugu Ma Qiulin. Mkutano huo umehudhuriwa na Mabalozi 11 wa nchi za SADC na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa SADC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Miundombinu wa Sekretariat ya SADC Bi Mapolao Mokolena.

Katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo Balozi wa Tanzania Mhe. Mbelwa Kairuki alitoa hotuba kwa niaba ya Jumuiya ya Mabalozi wa Nchi za SADC nchini China ambapo pamoja na mambo mengine aliyakaribisha makampuni ya SADC kuchangamkia fursa za uwekezaji katika nchi za SADC kutokana  na fursa za soko kubwa la SADC lenye idadi ya watu wanaokadiliwa kuwa milioni 345 na uchumi wa GDP 600 Billioni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miundombinu wa SADC Bi Makolane alipokuwa akitoa mada alielezea mazingira mazuri  yaliyopo ya biashara na uwekezaji katika nchi za SADC. Aidha, Mabalozi wa nchi za SADC walielezea fursa zilizopo katika nchi za SADC katika sekta za miundombinu, kilimo, viwanda; madini; utalii nk.  

Jiangsu ni jimbo la pili kwa ukubwa wa uchumi nchini China likiwa na GDP ya USD 1.2 Trillion na idadi ya watu milioni 80.  Jimbo hilo linaongoza nchini China katika sekta ya viwanda. Makampuni kutoka Jimbo la Jiangsu yamefanya uwekezaji nchini Tanzania katika sekta ya viwanda.

Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Afrika na wenyeji China mara baada kuhitimisha mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC uliofanyika jimbo la Jiangsu nchini China
Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki akitoa hutuba kwenye ufunguzi wa Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC ulifanyika Jiangsu, China
Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki (mstari wa mbele katikati) akifuatilia Mkutano wa kuvutia uwekezaji uliokuwa ukiendelea 
Wajumbe kutoka chi za SADC na Wenyeji tao China wakifutilia Mkutano uliokuwa ukiendelea

Friday, October 25, 2019

TANZANIA YATAKA ZIMBABWE KUONDOLEWA VIKWAZO VYA KIUCHUMI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akihutubia katika kongamano maalumu la kujadili vikwazo vya kiuchumi na hatma ya Afrika: Uzoefu kutoka Zimbabwe.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza katika kongamano la kujadili vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa Zimbabwe

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango (Mb) akitoa hotuba ya majumuisho na kufunga kongamano maalumu la kujadili vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa Zimbabwe

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. John Jingu, akihutubia hadhara wakati alipowasilisha mada iliyolenga hali ya utawala na diplomasia ya uchumi Afrika katika kongamano maalumu la kujadili vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa Zimbabwe.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika kongamano maalumu lililojadili vikwazo vya kiuchumi na hatma ya Afrika: Uzoefu kutoka zimbabwe.

Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Mstaafu Joseph Warioba (wa pili kutoka kulia) pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali, vyama vya siasa wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika kongamano maalumu

Baadhi ya mabalozi wateule pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika kongamano la kujadili vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa Zimbabwe.

Vingozi, Mabalozi na wananchi wakifuatilia mdahalo wa kujadili jinsi ya kuiwezesha Zimbabwe kuondolewa vikwazo vya kiuchumi.

Wageni wa Meza kuu wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango (Mb) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye pamoja na watoa mada wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wateule katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimishwa kwa kongamano

Mabalozi wa SADC, Qatar watoa wito kuiondolea vikwazo Zimbabwe.

Waheshimiwa Mabalozi wakiwa wanaendelea kutekeleza jukumu lao.
Baada ya kumaliza kazi wanapongezena kwa kushikana mikono ikiwa ni kiashiria cha mshikamamo hadi Zimbabwe inaondolewa vikwazo.


Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma Rajab akiongea na Waheshimiwa Mabalozi wa Nchi za Eswatini na Afrika Kusini ambao wanaunda kundi la Mabalozi wa nchi za SADC nchini Qatar. Waheshimiwa Mabalozi walikuwa wanakamilisha mpango mkakati wa kutumia siku ya tarehe 25 Oktoba kama ilivyoamuliwa na Viongozi wa Nchi za SADC kupaza sauti kwa njia mbalimbali kutoa wito kwa nchi za Magharibi kuiondolea vikwazo vya uchumi ilivyowekewa Zimbabwe. Mabalozi hao wamepanga kupeleka Waraka wa Kidiplomasia Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, Balozi za EU na Ubalozi wa Marekani pamoja na kutoa makala kwenye vyombo vya habari kuelezea athari za vikwazo katika uchumi wa Zimbabwe. 

WAZIRI KABUDI ASHIRIKI MAADHIMISHO YA 74 YA SIKU UMOJA WA MATAIFA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Bw. Michael Dunford Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini alipowasili katika uwanja wa Nyerere Square jijini Dodoma kushiriki maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa amesimama sehemu maalumu wakati wimbo wa Taifa ulipokuwa unapigwa kwenye sherehe za maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa mbele ya parede maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya sherehe za maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akikagua parede maalumu liliondaliwa kwa ajili ya sherehe za maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja Mataifa 
Sehemu ya hadhara iliyojitokeza katika uwanja wa Nyerere Square kushuhudia sherehe za maadhimisho 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (katikati) akifuatalia matukio yaliyokuwa yakiendelea wakati wa maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, akipokea zawadi kutoka Ofisi za Umoja wa Mataifa nchini iliyowasilishwa na Bw. Michael Dunford Kaimu Mratibu Mkazi, kwenye sherehe za maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika jijini Dodoma 
Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi Wafanyakazi wa Ofisi za Umoja wa Mataifa nchini
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akihutubia  hadhira iliojitokeza kwenye maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Taifa iliyofanyika jijini Dodoma katika uwanja wa Nyerere Square

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akihutubia  hadhira iliojitokeza (hawapo pichani) kwenye amaadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Taifa iliyofanyika jijini Dodoma katika uwanja wa Nyerere Square


WAKATI HUO HUO MHE. PROF. KABUDI AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA  BW. MICHAEL DUNFORD KAIMU MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, akiwa na Bw.Michael Dunford Kaimu Katibu Makazi wa Umoja wa
Mataifa nchini, walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma. Wengine ni Bw. Deusdedit Kaganda Kaimu Mkurugenzi wa Ushikiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Bi.Glory Ngaiza Afisa Mambo ya Nje.
Waziri Mhe. Prof. Kabudi akilelezea jambo wakati wa mazungumzo na Bw. Michael Dunford Kaimu Katibu Makazi wa Umoja wa Mataifa nchini. Wawili hao wamejadili masuala mbalimbali ya kuendelea kudumisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Umoja wa Mataifa


VILEVILE WAZIRI MHE. PROF. PALAMAGAMBA JOHN KABUDI AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akisisitiza jambo alipokutana wakati wa mazunguzo na Mkuu wa Shirika la Wahamiaji nchini Dr. Qasim Sufi walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Wawili hao wamejadili masuala mbalimbali ya kuendelea kudumisha ushiririkiano kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kutoa huduma.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akimsikiliza Mkuu wa Shirika la Wahamiaji nchini Dr. Qasim Sufi walipokutana kwa mazungumzo jijini Dodoma

Wednesday, October 23, 2019

MAADHIMISHO YA SIKU YA UMOJA WA MATAIFA KUFANYIKA KESHO, DODOMA

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizungumza na wanahabari  (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma.

Katika mkutano huo Dkt. Mnyepe amewajulisha waandishi wa habari kuhusu kufanyika kwa maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa tarehe 24 Oktoba, 2019
jijini Dodoma kwenye uwanja wa Nyerere square.  

Dkt. Mnyepe amebainisha kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho hayo, yatakayofanyika kuanzia saa 2.30 asubuhi hadi 5.00 asubuhi.

Maadhimisho ya mwaka huu yataongozwa na kauli mbiu isemayo "Wanawake na Wasichana kuwa Kipaumbele katika kufikia Malengo ya Dunia. Kauli mbiu hii inalenga kusisitiza uwajibikaji na ushirikishwaji wa Wanawake katika kufikia malengo ya dunia.

Aidha, Katibu Mkuu Dkt. Mnyepe amebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuheshimu na kusimamia misingi ya kulinda na kutetea maslahi ya Wanawake na Wasichana ikiwemo kuwashirikisha katika mipango ya maendeleo ya kijamii na uchumi.

Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa hufanyika kila mwaka tarehe 24 Oktoba. Maadhimisho ya mwaka huu ambayo yatapambwa na shamrashamra kutoka vikundi mbalimbali vya sanaa, yanatarajiwa kuhudhuriwa na Viongozi na Watendaji Wakuu wa Serikali, Wawakilishi kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa nchini, vijana, asasi za kiraia na wadau wengine mbalimbali.
Bw. Michael Dunford Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika ofisi za Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma.   
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (katikati) Bw. Deusdedit Kaganda Kaimu Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Bw. Michael Dunford Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini wakisikiliza maswali kutoka kwa Wanahabari (hawapo pichani).
Picha ya pamoja baada ya mkutano na waandishi wa habari

Saturday, October 19, 2019

PROF. KABUDI AKUTANA NA BALOZI MTEULE WA EU

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazugumzo na Balozi  Mteule wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Manfredo Fanti katika ofisi ndogo za Wizarajijini Dar es Salaam.

Balozi Mteule wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Manfredo Fantiakifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na Balozi Mteule wa Rwanda nchini, Meja Jenerali Karamba Charles jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Itifiki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Wilbert Ibuge akimkaribisha Balozi Mteule wa Rwanda nchini, Meja Jenerali Karamba Charles katika ofisi ndogo za Wizarajijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akipokea nakala ya hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Manfredo Fanti. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akipokea nakala ya hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Rwanda nchini, Meja Jenerali Karamba Charles. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Wilbert Ibuge.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika picha ya pamoja na Balozi mteule wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Manfredo Fanti na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Wilbert Ibuge, pamoja Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Mona Mahecha katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika picha ya pamoja na Balozi mteule wa Rwanda nchini, Meja Jenerali Karamba Charles. Kulia ni Mkuu wa Itifiki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Wilbert Ibuge.

Prof. Kabudi akutana, kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Manfredo Fanti.
Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Kabudi amemueleza Balozi Fanti kuwa Uhusiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya ni wa Muda mrefu tangu mwaka 1975 ambao hadi sasa Tanzania imekuwa na mahusiano imara na umoja huo.
"Ushirikiano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya umelenga kupunguza umasikini, kukuza maendeleo endelevu, na kusaidia ujumuishaji wa Tanzania katika uchumi wa dunia, mpango kazi wa ushirikiano huu unaundwa na nguzo kuu tatu ambazo ni maendeleo ya uchumi, biashara na uwekezaji pamoja na mazungumzo ya kisiasa. Msaada wa Umoja wa Ulaya umeweza kushughulikia changamoto mbalimbali katika ajenda za maendeleo ya kitaifa" Alisema Prof. Kabudi
 Waziri Kabudi ameongeza kuwa, kulingana na takwimu za mwaka 2017, Umoja wa Ulaya unaonekana ndiye mshirika mkubwa zaidi wa biashara ya bidhaa kwa Tanzania baada ya India, kwa asilimia 13.1. Bidhaa zinazoingizwa kutoka Umoja wa Ulaya ni pamoja na mashine, vifaa, bidhaa za kemikali na vifaa vya usafirishaji.  
 Prof. Kabudi amegusia pia mazungumzo ya kisiasa na kueleza kuwa ni nguzo muhimu ya uhusiano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya. Mazungumzo ya kisiasa yanalenga kuongeza uwazi na umoja ili kukuza uelewa wa pamoja katika vyama vya siasa.
 Balozi mteule wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Manfredo Fanti amesema kuwa Umoja huo upo tayari kusaidia Tanzania na kuhakikisha kuwa sera za nchi zinasonga mbele ili kuiwezesha Tanzania kuwa na  maendeleo endelevu na kusaidia malengo ya nchi. 
"Pia tupo tayari kuhakikisha kuwa uwekezaji na biashara unaofanywa kati ya Umoja wa Ulaya pamoja na Tanzania unakuwa wa manufaa kwa pande zote lengo likiwa ni kukuza sekta ya biashara hapa Tanzania" Balozi Fanti
Katika tukio jingine Waziri wa Mamno ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mteule  wa Rwanda hapa nchini, Meja Jenerali Karamba Charles ambaye ameelezea uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Rwanda ni wa kiwango cha juu na kuongeza kuwa jukumu lake kubwa kwa sasa ni kuongeza kiwango cha biashara na uswekezaji kati ya Nchi hizo mbili.
Meja Jenerali Karamba Charles ameyasema hayo wakati akikabidhi nakala za hati ya utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) kuchukua nafasi ya  aliyekuwa Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Balozi Eugene Kayihura ambaye amemaliza muda wake.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar Es Salaam,Tanzania