Monday, October 28, 2019

Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC Wafanyika JIANGSU

Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC kutoka Jimbo la Jiangsu umefunguliwa leo jijini Nanjing na Naibu Gavana wa Jimbo hilo Ndugu Ma Qiulin. Mkutano huo umehudhuriwa na Mabalozi 11 wa nchi za SADC na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa SADC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Miundombinu wa Sekretariat ya SADC Bi Mapolao Mokolena.

Katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo Balozi wa Tanzania Mhe. Mbelwa Kairuki alitoa hotuba kwa niaba ya Jumuiya ya Mabalozi wa Nchi za SADC nchini China ambapo pamoja na mambo mengine aliyakaribisha makampuni ya SADC kuchangamkia fursa za uwekezaji katika nchi za SADC kutokana  na fursa za soko kubwa la SADC lenye idadi ya watu wanaokadiliwa kuwa milioni 345 na uchumi wa GDP 600 Billioni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miundombinu wa SADC Bi Makolane alipokuwa akitoa mada alielezea mazingira mazuri  yaliyopo ya biashara na uwekezaji katika nchi za SADC. Aidha, Mabalozi wa nchi za SADC walielezea fursa zilizopo katika nchi za SADC katika sekta za miundombinu, kilimo, viwanda; madini; utalii nk.  

Jiangsu ni jimbo la pili kwa ukubwa wa uchumi nchini China likiwa na GDP ya USD 1.2 Trillion na idadi ya watu milioni 80.  Jimbo hilo linaongoza nchini China katika sekta ya viwanda. Makampuni kutoka Jimbo la Jiangsu yamefanya uwekezaji nchini Tanzania katika sekta ya viwanda.

Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Afrika na wenyeji China mara baada kuhitimisha mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC uliofanyika jimbo la Jiangsu nchini China
Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki akitoa hutuba kwenye ufunguzi wa Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC ulifanyika Jiangsu, China
Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki (mstari wa mbele katikati) akifuatilia Mkutano wa kuvutia uwekezaji uliokuwa ukiendelea 
Wajumbe kutoka chi za SADC na Wenyeji tao China wakifutilia Mkutano uliokuwa ukiendelea

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.