Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma Rajab akiwa na wakimbiaji wa Tanzania walioshiriki mbio za marathon jijini Doha, Qatar. wakimbiaji hao walienda Ubalozini kuaga kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani.
Wakimbiaji wa
Tanzania walimaliza rasmi mashindano ya mbio za Marathon na kwa bahati mbaya
wanariadha wawili hawakuweza kumaliza mbio hizo kutokana na maumivu ya goti na
misuli. Mwanariadha Alphonce Simbu ambaye alikuwa anatetea medali yake ya shaba
alishika nafasi ya 16 na alikuwa miongoni mwa wakimbiaji 20 bora ambao wamefuzu
moja kwa moja kushiriki mashindano ya mwakani.
Wakimbiaji wa
Ethiopia walishinda medali za dhahabu na fedha na Mkenya alishinda medali ya
shaba.
Kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini Qatar,
Mhe. Fatma Rajab, Mwanariadha Simbu anaonekana ana uwezo mkubwa wa kuweza
kushinda na amewasihi wakimbiaji hao waendelee kuwasiliana na ofisi ya Ubalozi
ili kuwasaidia kupata ufadhili wa kuwajengea uwezo ikiwemo kupatiwa msaada wa
mafunzo na vifaa. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.