Monday, June 28, 2021

MAKONSELI WAKUU WA MSUMBIJI NA OMAN WAWASILISHA BARUA ZA UTAMBULISHO

 Na mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula apokea nakala ya barua za utambulisho za Makonseli Wakuu wawili kutoka Msumbiji na Oman wenye makazi Zanzibar.

Makonseli hao ni Mhe. Agustinho Abacar Trinta Konseli Mkuu wa Msumbiji pamoja na Mhe. Said Salim Al Sinawi Konseli Mkuu wa Oman

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamedajiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia na Kiuchumi baina ya nchi zao na Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala ya barua za utambulisho kutoka kwa Konseli Mkuu wa Msumbiji mwenye makazi Zanzibar Mhe. Agostinho Abacar Trinta katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Konseli Mkuu wa Msumbiji mwenye makazi Zanzibar Mhe. Agostinho Abacar Trinta katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasilisha nakala ya hati za utambulisho   


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala ya barua za utambulisho kutoka kwa Konseli Mkuu wa Oman mwenye makazi Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi. Uwasilishwaji wa hati hizo umefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam 


Konseli Mkuu wa Oman mwenye makazi Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasilisha nakala ya hati za utambulisho      TANZANIA KUNUFAIKA SOKO ENEO HURU LA BIASHARA AFRIKA

Na Mwandishi wetu, Dar

Serikali ya Tanzania inategemea kunufaika na soko la bidhaa zake katika masoko ya nje baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa ushiriki katika Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA).

Akiongea na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCTA) Mhe. Wamkele Mene, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema kwa sasa Serikali ipo katika hatua za mwisho kusaini Mkataba wa AfCTA.

“Lengo la ziara ya Mhe. Mene hapa nchini pamoja na mambo mengine ni kukutana na viongozi na wadau wengine muhimu kujadiliana na masuala mbalimbali yanayohusu Mkataba wa AfCTA ikiwa ni pamoja na umuhimu wa Tanzania kuridhia Mkataba huo,” Amesema Balozi Mulamula

Balozi Mulamula ameongeza kuwa, uanzishwaji wa AfCTA ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa ambapo pamoja na mambo mengine, utekelezaji wake unatarajiwa kuongeza wigo wa fursa nafuu za biashara nchini kwa kuwavutia wawekezaji na kuongeza mauzo hasa ya bidhaa za kilimo.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Sekretariati ya Eneuo Huru la Biashara Afrika (AfCTA) Mhe. Wamkele Mene ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano ambao imempatia tangu wakati wa uchaguzi hadi sasa na kuahidi kuwa utekelezaji wa Mkataba huo utanufaisha kila Nchi Mwanachama.

“……….Naipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwani tangu ilipoingia Madarakani imetumia muda mfupi katika kushiriki kwa ukamilifu katika majadiliano ya kusaini mkataba huu na Tanzania imeshiriki vizuri sana kwenye majadiliano haya muhimu,” Amesema Mhe. Wene

Ameongeza kuwa kwa sasa Eneo Huru la Biashara Afrika lina Nchi wanachama 38 ambazo zimekubaliana na Mkataba huo na kwamba kwa sasa Sekretariati hiyo inaendelea kuimarika katika kukuza biashara na sekta binafsi katika nchi wanachama wa AfCTA.

Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika umesainiwa na Nchi 54 kati ya nchi 55 za Umoja wa Afrika ikiwemo Tanzania. mkataba huo ulipata nguvu ya Kisheria Julai, 2019 baada ya nchi 28 kuridhia Mkataba huo. Mkataba wa AfCTA unahusisha maeneno ya ushirikiano katika bishara ya bidhaa, biashara ya huduma, uwekezaji, hakimiliki na ubunifu pamoja na Sera za ushindani.

Katika tukio jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameshiriki uzinduzi wa Kongamano la Usawa wa Kijinsia ambapo pamoja na mambo mengine, Balozi Mulamula kongamano hili litakuwa mahsusi kuangalia masuala ya uswa wa jinsia kwa kizazi hiki na kizazi kijacho na kwamba wakuu wa Nchi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa watakuatana Ufaransa katika kongamano hilo kuanzia tarehe 30 Juni hadi 2 Julai 2021.

Balozi Mulamula ameongeza kuwa, Tanzania itashiriki katika kongamano hilo ambapo Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan atawakilishwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango

Uzinduzi wa Kongamano la Usawa wa Kijinsia uliofanyika leo jijini Dar es Salaam umehudhuriwa na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Fredric Clavie pamoja na Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Bibi Hodan Addou.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiongea na waandishi wa Habari wakati alipokutana na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) Mhe. Wamkele Mene leo Jijini Dar es Salaam


Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) Mhe. Wamkele Mene akiongea na waandishi wa Habari wakati wa Mkutano baina yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb)uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam


Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) Mhe. Wamkele Mene akiongea na waandishi wa Habari wakati wa Mkutano baina yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb)uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam


Mkutano ukiendelea


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akihutubia wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Usawa wa Kijinsia ulifanyika Jijini Dar es Salaam  


Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Fredric Clavie akihutubia wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Usawa wa Kijinsia ulifanyika Jijini Dar es Salaam  


Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Bibi Hodan Addou akihutubia wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Usawa wa Kijinsia Jijini Dar es Salaam 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb), Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Fredric Clavie pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Bibi Hodan Addou wakiwa katika picha ya pamoja   Sunday, June 27, 2021

KATIBU MTENDAJI AfCFTA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) Mhe. Wamkele Mene awasili nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku nne kuanzia tarehe 27 – 30 Juni, 2021.


Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) Mhe. Wamkele Mene akipokelewa akipokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya  Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) Mhe. Wamkele Mene akipokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya  Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz. Kushoto mwa Mhe. Mene ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Biashara,Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji, kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Benard Haule.


Mkurugenzi wa Idara ya Afrika - Wizara ya Mambo ya  Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) Mhe. Wamkele Mene mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam 


Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) Mhe. Wamkele Mene akipokelewa Saturday, June 26, 2021

TANZANIA NA PAKISTAN ZA ADHIMISHA SIKU YA URAFIKI


Tanzania na Pakistan zimefanya madhimisho ya siku ya urafiki wa kihistoria uliodumu kwa muda mrefu baina ya Mataifa haya mawili rafiki, yaliyochazwa na hafla fupi iliyofanyika tarehe 25 Juni 2021 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. 

Madhimisho haya ambayo yamefanyika kwa mara ya kwanza, yalihudhuriwa na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali katika jamii kama vile, Wafanyabiashara, Wanadiplomasia, Watendaji na Viongozi kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali, Watendaji wa Jumuiya za Kikanda, Wanasiasa na baadhi ya Viongozi Wastaafu wa Serikali. 

Pamoja na masuala mengine maadhimisho haya yanalenga kukuza zaidi mahusinao ya kibiashara baina ya Tanzania na Pakistan kwa kuwakutanisha wafanyabisha wa pande zote mbili ili waweze kubadilishana uzoefu na kujenga urafiki ambao utawazesha kwa pamoja kutumia na kuibua fursa za kibiashara zinazopatika katika nchi hizi mbili (Tanzania na Pakistan).

Akizungumza katika maadhimisho hayo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameeleza kuwa Tanzania itaendelea kuendeleza na kuboresha mahausiano mazuri yaliyodumu kwa muda mrefu na Pakistan. Ameongeza kusema kuwa Serikali ya Tanzania imejipanga kutumia muhusionao haya mazuri kuibua fursa za kibiashara ambazo zitanufaisha Serikali na raia wa pande zote mbili. “Takwimu za hivi karibuni zinaeleza, kuna zaidi ya kampuni 100 kutoka Pakistan ambazo zimewekeza nchini Tanzania. Ni lengo la Serikali ya awamu ya 6 kuhakikisha kunakuwepo na muafaka mzuri wa kisheria na kitaasisi na mazingira kwa wawekezaji hawa kufanya biashara nchini Tanzania bila bugudha.”

Akizungumza katika maadhimisho hayo Balozi wa Pakistan nchini Tanzania Mhe. Mohammad Saleem amepongeza Serikali ya Jumhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi Mahiri Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendele kuchukua hatua za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini. “Tunaendelea kushuhudia juhudi na mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya usimamizi mahiri wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha mazingira ya biashara nchini, hakika jitihada hizi zinatoa matumaini na faraja kubwa kwa wawekezaji waliopo nchini na wale ambao wanania ya kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini”. 

Mahusiano ya Kidiplomasia kati ya Pakistan na Tanzania yamedumu kwa tariban miaka 54 tokea yalipoanzishwa mwaka 1967 ambapo nchi ya Pakistani ilifungua Ofisi zake za Ubalozi hapa nchini Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwasili katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam kushiriki maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akihutubia hadhara iliyojitokeza kwenye maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania yaliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akihutubia hadhara iliyojitokeza kwenye maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania yaliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akikabithiwa picha yenye maudhui ya utamaduni wa Pakistani na Mhe. Mohammad Saleem (kulia) Balozi wa Pakistani nchini, kwenye maadhimisho ya maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania.

Balozi wa Pakistan nchini Tanzania Mhe. Mohammad Saleem akihutubia hadhara iliyojitokeza kwenye maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania yaliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote akihutubia hadhara iliyojitokeza kwenye maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania yaliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Hafla ya maadhimisho ikiendelea.
Hafla ya maadhimisho ikiendelea.
Hafla ya maadhimisho ikiendelea.

BALOZI MULAMULA AKUTANA NA WAWAKILISHI WA St. EGIDIO

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akionesha zawadi iliyotolewa na wawakilishi wa Jumuiya ya St. Egidio ya nchini Italia walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 25/06/2021.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiangalia zawadi iliyotolewa na wawakilishi wa Jumuiya ya St. Egidio ya nchini Italia walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 25/06/2021.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na wawakilishi wa Jumuiya ya St. Egidio ya nchini Italia walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 25/06/2021.

mazungumzo yakiendelea

Mmoja wa wawakilishi wa Jumuiya ya St. Egidio ya nchini Italia Bw. Andrea Bartoli akizungumza wakati wawakilishi hao walipomtembelea Balozi Mulamula ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 25/06/2021


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ya nchini Italia.

Katika mazungumzo hayo wawakilishi wa Jumuiya hiyo wakiongozwa na Bw. Andrea Bartoli wamemuhakikishia Mhe. Waziri Mulamula kuwa Jumuiya yao itaendelea na kazi ya kuhakikisha amani inatamalaki katika nchi mbalimbali barani Afrika ikiwemo Tanzania.

Akizungumza nao Mhe. Waziri amewahakikishia wawakilishi hao kwamba Tanzania itaendelea kuwaunga mkono katika harakati zao za kuwa na jamii salama kwani kufanya hivyo kunasaidia dunia kuwa salama.

Amewaomba kuendelea na kazi ya kuifahamisha jamii juu ya kazi zinazofanywa na Jumuiya hiyo katika sehemu mbalimbali nchini na barani Afrika kwa ujumla.

Jumuiya hiyo inajihusisha na masuala ya utafutaji wa amani kwa njia ya midahalo na mazungumzo ikiwa ni pamoja na kutoa misaada ya kijamii katika jumuiya mbalimbali nchini na katika Bara la Afrika.


BALOZI MULAMULA AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA WIZARA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (katikati) akiwa na viongozi wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakiimba wimbo wa mshikamano daima alipowasili ukumbini kwa ajili ya kuzindua Baraza jipya la Wafanyakazi wa wizara jijini Dodoma tarehe 25/06/2021

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiimba wimbo wa mshikamano daima baada ya mgeno rasmi kuwasili ukumbini kwa ajili ya kuzindua rasmi Baraza hilo jijini Dodoma 

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiimba wimbo wa mshikamano daima baada ya mgeni rasmi kuwasili ukumbini kwa ajili ya kuzindua Baraza hilo jijini Dodoma 

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Liberata Mulamula mara baada ya kuzindua Baraza hilo jijini Dodoma tarehe 25/06/2021.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Liberata Mulamula mara baada ya kuzindua Baraza hilo jijini Dodoma tarehe 25/06/2021.


wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja na Mhe. Waziri Mulamula

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Liberata Mulamula mara baada ya kuzindua Baraza hilo jijini Dodoma tarehe 25/06/2021.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amezindua Baraza jipya la Wizara na kuwataka wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara kuwa mabalozi wazuri wa watumishi wa Wizara wanaowawakilisha.

Mhe. Waziri Mulamula ametoa rai hiyo jijini Dodoma alipokuwa akizindua Baraza hilo jijini Dodoma baada ya baraza la awali kumaliza muda wake.

Amesema kwamba uongozi wake kwa kushirikiana na watendaji wengine wa Wizara wako tayari kuyasikiliza na kuyafanyia kazi mapendekezo watakayoyapeleka kwa uongozi wa Wizara na kuwataka kuyafanyia kazi mapendekezo yanayotolewa na wafanyakazi ili yaweze kushughulikiwa.

Mhe. Waziri pia amewaambia wajumbe wa Baraza hio kwamba uongozi wake hautovumilia tabia au vitendo vya utovu wa nidhamu kama vile rushwa vitakavyolalamikiwa kufanywa na watumishi wa Wizara dhidi ya watu wanaowahudumia.

Amesema ni matarajio yake kwamba watumishi wa Wizara watakuwa waadilifu na wenye tabia njema wanapowahudumia wadau mbalimbali wa Wizara na hivyo kutekeleza majukumu yao kwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma na hivyo kutekeleza majukumu ya wizara ipasavyo.

Amesema kuwa Wizara imejipanga kuhakikisha inatoa vifaa na vitendea kazi kwa watumishi wake ili kuhakikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara unakamilika na kuwa na ufanisi.

Kikao hicho cha Baraza kiliwapitisha wajumbe wake katika mpango wa Bajeti wa mapato na matumizi ya wizara iliyopitishwa na Bunge mapema mwezi huu, kiliwachagua Bibi Judica Nagunwa kuwa Katibu na Bw. Hassan Mnondwa kuwa katibu Msaidizi wa Baraza hilo jipya ambalo litakaa madarakani kwa muda wa miaka mitatu.


Friday, June 25, 2021

MAWAZIRI WA EAC WAKUBALIANA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA UCHUKUZI, MAWASILIANO NA HALI YA HEWA


Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaosimamia Sekta ya Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa leo tarehe 25 Juni 2021 kwa pamoja wamekubaliana kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya sekta ya uchukuzi, mawasiliano na hali ya hewa. Makubaliano haya yamefikiwa katika Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa (TCM) la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Lengo la Mkutano huo wa 17 wa TCM pamoja na mambo mengine ilikuwa ni kupitia na kujadili utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sambamba na kupitia na kujadili utekelezaji wa sera, mikakati, miradi na program mbalimbali katika sekta ya Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa. 

Miongoni mwa maeneo ambayo Mawaziri hao wamekubaliana kushirikiana ni pamoja na mapendekezo ya Taasisi ya Afrika Mashariki kuratibu programu za maendeleo katika Sekta ya Mawasiliano; utekelezaji wa miradi na programu katika sekta ndogo ya barabara, reli, usafiri wa anga, usafiri wa njia ya maji, hali ya hewa na mawasiliano.

Akizungumza baada ya Mkutano huo, Mwenyekiti Mhe. Wavinya Ndeti ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Miundombinu wa nchini Kenya amesema kuwa makubaliano muhimu yaliyofikiwa yatafungua zaidi fursa zinazotokana na sekta ya uchukuzi na usafirishaji kupitia anga, bararaba, reli na maji. Aliongezea kusema hatua hii itachangia kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kuboresha hali ya maisha ya watu katika Jumuiya. 

Kwa upande wake Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo Mhe. Mhandisi Dkt. Leonard Madaraka Chamulio (Mb) Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ameeleza “tumekubaliana katika masuala yote tuliyojadiliana na hivyo tumeyapeleka katika Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, vilevile tumejadili na kupeleka mapendekezo kwa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya kuhusu uunganishaji wa huduma katika anga la Afrika Mashariki”.

Kwa upande wa Tanzania ushirikiano huu katika sekta ya anga unatarajiwa kuongeza mapato ya nchi kwa kuwa huduma za uongozaji ndege zitatozwa kutokana na ukubwa, uzito na muda utakaotumiwa na ndege kupita katika Anga la Tanzania.

Mkutano huo wa Mawaziri ambao awali ulitanguliwa na mikutano ya Wataalam na Makatibu Wakuu iliyofanyika kwa nyakati tofauti kuanzia ya tarehe 21 hadi 24 Juni 2021 jijini Dar, licha ya kupitia utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya wamepokea na kujadili agenda mbalimbali zilizowasilishwa kwao na Makatibu Wakuu ikiwemo, mapendekezo kuhusu Taasisi ya Afrika Mashariki kuratibu programu za maendeleo katika Sekta ya Mawasiliano.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mhandisi Dkt. Leonard Madaraka Chamulio akichangia jambo kwenye Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, Bw. Eliabi Chodota akifuatilia Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam.

Afisa Uchumi Bi. Edna Chuku kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifuatilia Mkutano uliokuwa ukiendelea.

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote akifafanua jambo kweye Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam

Mawaziri kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Masharikia wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini taaraifa ya Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa uliofanyika katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam

Wajumbe wakifuatilia majadala uliokuwa ukiendelea katika Mkutano.
 

Mkutano ukiendelea


                                          Mkutano ukiendelea