Monday, June 28, 2021

MAKONSELI WAKUU WA MSUMBIJI NA OMAN WAWASILISHA BARUA ZA UTAMBULISHO

 Na mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula apokea nakala ya barua za utambulisho za Makonseli Wakuu wawili kutoka Msumbiji na Oman wenye makazi Zanzibar.

Makonseli hao ni Mhe. Agustinho Abacar Trinta Konseli Mkuu wa Msumbiji pamoja na Mhe. Said Salim Al Sinawi Konseli Mkuu wa Oman

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamedajiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia na Kiuchumi baina ya nchi zao na Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala ya barua za utambulisho kutoka kwa Konseli Mkuu wa Msumbiji mwenye makazi Zanzibar Mhe. Agostinho Abacar Trinta katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Konseli Mkuu wa Msumbiji mwenye makazi Zanzibar Mhe. Agostinho Abacar Trinta katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasilisha nakala ya hati za utambulisho   


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala ya barua za utambulisho kutoka kwa Konseli Mkuu wa Oman mwenye makazi Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi. Uwasilishwaji wa hati hizo umefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam 


Konseli Mkuu wa Oman mwenye makazi Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasilisha nakala ya hati za utambulisho      



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.