Friday, June 11, 2021

MKUTANO WA 31 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC WANAOSHUGHULIKIA MASUALA YA AFRIKA MASHARIKI NA MIPANGO WAFANYIKA ARUSHA

Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango umefanyika jijini Arusha leo tarehe 11 Juni 2021 huku Mawaziri wakipitisha agenda mbalimbali zilizowasilishwa kwao.

 

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kikanda wa Kenya, Mhe. Aden Mohammed amepongeza kazi kubwa iliyofanywa na vikao vilivyotangulia vya Wataalam na Makatibu Wakuu ya kukamilisha agenda mbalimbali muhimu na kwamba anayo furaha kwa mikutano mbalimbali kuanza kufanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na Wajumbe kutoka Nchi Wanachama baada ya vikao hivyo kufanyika kwa muda mrefu kwa njia ya mtandao kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona.

 

Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Peter Muthuki aliwakaribisha Mawaziri kwenye Makao Makuu ya[H1]  Jumuiya hiyo na alitumia fursa hiyo kuzipongeza Tanzania na Uganda kwa kuendesha zoezi la uchaguzi kwenye nchi zao kwa amani na utulivu. Kadhalika, alitoa shukrani kwa Nchi Wanachama kwa kuendelea kushirikiana kikamilifu na Sekretarieti ya Jumuiya hiyo na kuiwezesha kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa ufanisi.


Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula ambaye alishiriki mkutano huo kwa mara ya kwanza kwa njia ya mtandao akiwa jijini Dar es Salaam, alitumia fursa hiyo kumpongeza Mwenyekiti wa mkutano huo pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuteuliwa kuiongoza Jumuiya hiyo na kuwahakikishia ushirikiano kutoka kwake binafsi na kwa  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mkutano wa Mawaziri ulitanguliwa na Mkutano kwa Ngazi ya Wataalam uliofanyika tarehe 7 hadi 9 Juni 2021 na kufuatiwa na Mkutano wa Makatibu tarehe 10 Juni 2021.


Pamoja na mambo mengine Mkutano huo umepokea na kupitisha agenda mbalimbali zilizowasilishwa ikiwa ni pamoja Taarifa ya Utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa kwenye vikao vilivyopita; Taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki; Taarifa kuhusu ombi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo la kujiunga na EAC; Taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa ya utatu wa Jumuiya za EAC-COMESA-SADC katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika na Taarifa ya Uchangiaji wa Bajeti ya EAC kutoka Nchi Wanachama.


Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Ngazi ya Mawaziri umeongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohammed Mchengerwa aliyemwakilisha Mhe. Balozi Mulamula ambaye alishiriki kwa njia ya mtandao.

 

Viongozi wengine walioshiriki Mkutano huo ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kilangi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji, Uchumi na Ajira Zanzibar, Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Godwin Mollel, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Bw. Mussa Haji Ali na   Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Mohammed Mchengerwa akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliofanyika jijini Arusha tarehe 11 Juni 2021. Kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardius Kilangi.

Mhe. Mchengerwa akichangia hoja wakati wa Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliofanyika jijini Arusha tarehe 11 Juni 2021

Mhe. Prof. Kilangi naye akichangia jambo wakati wa Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliofanyika jijini Arusha tarehe 11 Juni 2021

Mwenyekiti wa Mkutano wa Mawaziri ambaye ni Waziri Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kikanda wa Kenya, Mhe. Adan Mohammed akifungua rasmi Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliofanyika jijini Arusha tarehe 11 Juni 2021

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Mhe. Dkt. Peter Mathuki akizungumza wakati wa Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliofanyika jijini Arusha tarehe 11 Juni 2021

Ujumbe wa Burundi ukiongozwa na Mhe. Balozi Ezechiel Nabigira (kushoto), Waziri anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Vijana, Michezo na Utamaduni

Ujumbe wa Rwanda ukiongozwa na Mhe. Prof. Manasseh Nshuti (kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa


Ujumbe wa Kenya ukiwa kwenye Mkutano wa 31 Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliofanyika jijini Arusha tarehe 11 Juni 2021

Ujumbe wa Uganda ukishiriki Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliofanyika jijini Arusha tarehe 11 Juni 2021


Ujumbe wa Sudan Kusini ukishiriki Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliofanyika jijini Arusha tarehe 11 Juni 2021

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji, Uchumi na Ajira Zanzibar, Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga (kulia) akiwa  na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Godwin Mollel kwenye Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliofanyika jijini Arusha tarehe 11 Juni 2021. 

Mhe. Soraga na Mhe. Mollel wakiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome wakati wa Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliofanyika jijini Arusha tarehe 11 Juni 2021

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) kwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Bw. Mussa Haji Ali na Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi wakiwa kwenye Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliofanyika jijini Arusha tarehe 11 Juni 2021

Ujumbe wa Tanzania ukishiriki Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliofanyika jijini Arusha tarehe 11 Juni 2021


Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.