Thursday, June 17, 2021

NAIBU WAZIRI AFANYA MAZUNGUMZO NA WAANDAAJI MASHINDANO YA UREMBO AFRIKA MASHARIKI

 

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na waandaaji wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki (Miss East Africa beauty Pegeant) ofisini kwake jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota akizungumza wakati Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk wakati walipokutana na akizungumza na waandaaji wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki (Miss East Africa beauty Pegeant) ofisini kwa Naibu Waziri jijini Dodoma

Makamu Rais wa Kamati ya Waandaaji wa Mashindano ya Urembo Afrika Mashariki bi Jolly Mutesi wa Rwanda (katikati) akizungumza akiwa na bi Mariam Ikoa kutoka Tanzania wakia na naibu Waziri Ofisini kwake jiini Dodoma.

mazungumzo yakiendelea

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika picha ya pamoja na waandaaji wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki (walioko Kulia kwake) walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodom


Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amekutana na kufanya mazungumzo na waandaaji wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki (Miss East Africa beauty Pegeant) ofisini kwake jijini Dodoma.

Waandaaji hao ni  bi Jolly Mutesi ambaye ni makamu wa Rais anayetokea nchini Rwanda na bi Mariam Ikoa ambaye ni muandaaji wa kimataifa anayetokea Tanzania.

Katika mazungumzo hayo  na waandaaji hao wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk amewapongeza waandaaji hao  kwa kuja na wazo  hilo pamoja na kutaka kufahamu miongozo na itifaki za kufuatilia ili kufanikisha mashindano hayo.

Akizungumza  katika kikao hicho Mratibu wa mashindanoo hayo Bi Mariam Ikoa amemuelezea Mhe. Naibu Waziri Mbarouk kwamba ujio wao Wizarani una lengo la kujitambulisha pamoja na kupata miongozo na itifaki za jinsi ya kuendelea na taratibu za mashindano hayo ya urembo kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Amesema mashindano hayo yamepangwa  kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 26 Oktoba hadi Novemba 20 2021

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.