Thursday, June 30, 2016

Waziri Mahiga akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Rwanda


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharikii, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe.Loiuse Mushikiwabo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha na kuboresha mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizi mbili pamoja na Ziara ya ya Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mhe. Paul Kagame anayetarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ziara ya siku mbili. 

Kaimu Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. James Bwana alipokuwa akimkaribisha Mhe. Waziri Mushikiwabo mara baada ya kuwasili Wizarani.

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Samuel Shelukindo akiwa na Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. James Bwana na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Medard Ngaiza wakifuatilia mazungumzo.
Balozi wa Jamhuri ya Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura (kulia) pamoja na Afisa aliyeambatana na Mhe. Waziri Mushikiwabo wakifuatilia mazungumzo.

Wakati mazungumzo yakiendelea
Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo

Diaspora wahimizwa kutii Sheria bila Shuruti


TANGAZO KWA WATANZANIA WOTE NA WALE WANAOISHI NJE YA NCHI (DIASPORA)

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, inaendelea na jitihada zake za kuhamasisha Watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) katika kuchangia maendeleo ya nchi yao.  Ili kufanikisha hilo, Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo imekuwa ikizishawishi taasisi mbalimbali hapa nchini kutoa huduma na fursa za biashara na uwekezaji, ambazo zitasaidia Diaspora kuwekeza kiurahisi hapa nchini.  Juhudi hizi ambazo zilianza tokea Serikali ya Awamu ya Nne zimeanza kutoa matunda makubwa ambapo thamani ya uwekezaji kutoka kwa Diaspora inaongezeka kila kukicha.

Thursday, June 23, 2016

Rais Magufuli apokea taarifa ya Uchaguzi Mkuu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Ikulu, kwa ajili ya makabidhiano ya taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wageni waalikwa (hawapo pichani) katika hafla ya Makabidhiano ya taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015.
Taarifa hiyo imekabidhiwa leo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Damian Lubuva kwa Mhe. Rais Magufuli, katika hafla iliyofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi Wakuu wastaafu wa Serikali, Viongozi wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Bara na Zanzibar, Waheshimiwa Mawaziri na Viongozi Waandamizi wa Serikali, wengine ni  Viongozi Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Waheshimiwa Mabalozi na  Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaowakilisha nchini.

Mhe. Rais akionyesha taarifa aliyokabidhiwa na Mhe.Lubuva kwa wageni  waalikwa 
Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akijadili jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi(Katikati) mara baada ya kuwasili Ikulu kwaajili ya kushuhudia makabidhiano hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Aziz Mlima (wa kwanza kulia) akifuatilia hotuba iliyokuwa ikiwasilishwa na Mhe. Rais Magufuli
Mkuu wa Mabalozi, Mhe. Ambrosio Montecilo Balozi wa Angola nchini (wa kwanza kushoto) pamoja na Mabalozi wengine wanaowakilisha mataifa yao nchini wakishuhudia zoezi la makabidhiano ya taarifa ya NEC
Sehemu nyingine ya Mabalozi wakishudia makabidhiano
Kaimu Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. James Bwana (kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Gerson Msigwa wakiratibu hafla hiyo. 

Mhe. Rais akiwa katika picha ya pamoja na viongozi Wakuu wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Bara na Zanzibar, Viongozi wengine Wakuu wa Serikali na Marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 
Mhe. Rais na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mawaziri na Watendaji Wakuu wa Serikali

Mhe. Rais na meza kuu katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaowakilisha hapa nchini
Mhe. Rais na meza kuu  katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) 
Bw. James Bwana akiagana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo
Waziri Mahiga akijadili jambo na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Wizara ya Mambo ya Nje yaadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma

Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz P Mlima akizungumza na Wafanyakazi (hawapo pichani) wakati maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umama. Pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu alitumia fursa hiyo kusikiliza matatizo na kero mbalimbali zinazo wakabili watumishi wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Watumishi wakimsikiliza Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz P Mlima (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa
 Umma
Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz P Mlima akisisitiza jambo kwa watumishi wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. Pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu alitumia fursa hiyo kusikiliza matatizo na kero mbalimbali zinazo wakabili watumishi wakati wa kutekeleza majukumu yao. Pamojanaye ni Wakurugenzi wa Utawala na Usimamizi Raslimali Watu Niger Msangi (kushoto) na Bi. Mary Fidelis (Kulia)
Watumishi wakimsikiliza Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz P Mlima (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma
Waliosimama ni Watumishi wapya waliojiunga na Wizara hivi karibuni wakitambulishwa wakati wa Mkutano wa maadhimisho ya Wiki ya utumishi wa umma
Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria Balozi Baraka Luvanda (wapili kushoto) akichangia hoja wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC).
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wizara ya Mambo ya Nje yaadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima amewaasa watumishi wa Wizara hiyo kutekeleza wajibu wao ipasavyo kwa kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo haiwezi kufikiwa bila ya wao kutimiza wajibu wao kikamilifu.

 Dkt. Mlima alitoa kauli hiyo leo wakati wa kikao cha pamoja na watumishi kujadili mafanikio na changamoto zinazoikabili Wizara hiyo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo itahitimishwa tarehe 23 Juni 2016.

Aliwataka watumishi kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, ubunifu na kwa kushirikiana ili kuongeza kasi ya ufanisi wa Wizara.  “Nataka Wizara yetu iwe moja kati ya taasisi za Serikali zinazotoa huduma bora kabisa hapa nchini, hivyo tekelezeni wajibu wenu bila hofu kwa kuwa haki na maslahi ya kila mtumishi yatazingatiwa”.

Dkt. Mlima alipongeza uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wa kupunguza kodi ya mapato ya watumishi (payee) kutoka asilimia 11 hadi 09 na kubainisha kuwa hiyo ni ishara ya wazi kwamba ahadi ya Mhe. Rais ya kuboresha maslahi ya watumishi itatimizwa.

Katibu Mkuu alihitimisha nasaha zake kwa kuwaomba watumishi kuongeza saa moja ya ziada siku ya kilele cha maadhimisho ya Wiki ya utumishi wa umma ili itumike kutoa huduma kwa wananchi jambo ambalo liliungwa mkono na watumishi.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 23 Juni 2016.Katibu Mkuu wa AALCO, Prof. Gastorn afanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga )(Mb) kulia akifanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria katika Nchi za Asia na Afrika (Asian – African Legal Consultative Organization (AALCO), Prof. Kennedy Gastorn. Prof. Gastorn alichaguliwa kushika nafasi hiyo wakati wa Mkutano wa 55  uliofanyika mjini New Delhi, India mwezi Mei 2016. Prof. Gastorn alikuja kumuona Mhe. Waziri kwa lengo la kujitambulisha, kushukuru kwa kuungwa mkono na kubadilishana taarifa kuhusu Jumuiya hiyo.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria katika Nchi za Asia na Afrika (Asian – African Legal Consultative Organization (AALCO), Prof. Kennedy Gastorn akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo hayo. Alibainisha kwamba nafasi hiyo ni heshima kubwa kwake na nchi kwa ujumla kwa kuwa jukwaa hilo ni jukwaa muhimu kwa maendeleo ya sheria za Kimataifa nchini na Barani Afrika. Aliiomba Serikali ya Tanzania kuendelea kumuunga mkono kwenye utekelezaji wa majukumu yake kwa kuzisihi nchi za Afrika zijiunge na AALCO.
Mhe. Waziri akiendelea na mazungumzo yake ambapo alitoa pongezi kwa Prof. Gastorn na kumtakia kila la kheri kwenye utekelezaji wa majukumu yake mapya na kumuahidi ushirikiano wa Serikali ya Tanzania. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Baraka Luvanda (tai nyekundu) na Afisa wa Kitengo hicho, Bw. Abdallah Mtibora.