Monday, June 6, 2016

Waziri Mahiga ampokea Naibu Waziri Mkuu wa Ubelgiji Mjini Dodoma

Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa na mgeni wake Mhe. 

Didier Reynders, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji mara baada ya kuwasili Mjini Dodoma kwa mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Serikali leo tarehe 6 Juni 2016.

Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akisalimiana na Mhe. Mahiga mara baada ya kumpokea na kumsalimu Mhe.

Didier Reynders, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji ofisini kwake mjini Dodoma ambapo alifanya mazungumzo kuhusu masuala ya biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Ubelgiji. 

Mazungumzo yakiendelea

Mhe. Kassim Majaliwa akiagana na Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania Mhe. Paul Cartier ambaye naye alikuwepo Mjini Dodoma na Naibu Waziri Mkuu wa nchi hiyo kwneye ziara ya kikazi ya siku tatu nchini Tanzania.

Mhe. Reynders na ujumbe wake wakiwa Mjini Dodoma walipata fursa ya kutembelea jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alisifu ukomavu wa demokrasia nchini Tanzania.

Ujumbe wa Naibu Waziri Mkuu (kutoka kulia-kushoto) Mhe. Didier Reynders, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga - Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Paul Cartier - Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Balozi Samuel Shelukindo - Mkurugenzi Idara ya
Afrika na mwisho ni Mjumbe Maalum wa Serikali ya
Ubelgiji wa Ukanda wa Maziwa Makuu.
Mhe. Didier Reynders, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji akiwa pichani na Mhe. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia alifanya naye mazungumzo kabla ya kuhitimisha ziara yake fupi mjini hapo.

Mhe. Didier Reynders, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji akiagana na mwenyeji wake Mhe. Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye uwanja wa ndege. Mwingine pichani (wa kwanza kulia) ni Mhe. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria. 




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.