Friday, June 3, 2016

Tanzania kuendelea kuimarisha ushirikiano na nchi za Ghuba

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akimkaribisha leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam, Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Saud Ali Mohamed Al-ruqaishi alipokuja kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kuhudumu hapa nchini.

 Katika mazungumzo yao Waziri Mahiga alimshukuru Balozi kwa kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Oman, vilevile aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano hata kwa Balozi atakaye teuliwa kuja kuiwakilisha nchi ya Oman. kwa upande wa Balozi Al-raqaishi alitumia fursa hiyo kumshukuru Waziri Mahiga na uongozi wote wa Wizara kwa ujumla kwa ushirikiano aliokuwa akipewa kwa kipindi chote cha uwakilishi wa Taifa lake hapa nchini. 
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga pamoja na Afisa Mambo ya Nje Bw. Tahir Bakari, kwa pamoja wakifuatilia mazungumzo kati ya Dkt. Mahiga na Balozi Al-ruqaishi.
Waziri Mahiga na Balozi Al-ruqaishi wakiwa katika picha ya pamoja.
       ===Wakati huo huo Waziri Mahiga alizungumza na Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu===

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Kulia) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Falme za Kiarabu (U.A.E) nchini Mhe. Abdulla Ibrahim Ghanim Al suwaidi alipokuja kumtembelea wizarani, na kufanya naye mazungumzo  yaliyojikita katika kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Falme za Kiarabu katika nyanja mbalimbali zikiwemo:  Afya, Elimu, Biashara na Uchumi, pia Balozi wa Al suwaidi alimpongeza Waziri Mahiga kwa Hotuba ya Bajeti ya 2016/2017 iliyopitishwa na Bunge. 
Waziri Mahiga na Balozi Al suwaidi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mazungumzo
                      === Pia Dkt. Mahiga alikutana kwa mazungumzo na Balozi wa Kuwait  ====

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akisaliamiana na Balozi wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al Najem alipomtembelea Wizarani mapema leo asubuhi na kufanya naye mazungumzo yaliyojikita katika kuboresha na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Kuwait.
Dkt. Mahiga akimweleza jambo Balozi Al Najem
Balozi Al Najem akimwelezea jambo Waziri Mahiga mara baada ya kuzindua Tovuti ya Ubalozi wao, huku Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya kati Balozi Abdallah Kilima (wa Tatu kutoka kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga pamoja na Afisa Mambo ya Nje wakishuhudia.  
Waziri Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Al Najem mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

==== Vilevile Balozi  Mahiga alikutana kwa mazungumzo na  Balozi wa Qatar ====
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Kulia) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar Mhe. Abdulla Jassim Al Maadad alipokuja kumtembelea Wizarani, mazungumzo hayo yaliyojikita katika kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Qatar katika nyanja mbalimbali zikiwemo za Elimu, Biashara na Uchumi.
Balozi Al Maadadi naye pia alimweleza Waziri Mahiga atahakikisha kuwa anaendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na nchi yake, sambamba na kuhakikisha Serikali nchini Qatar inaisaidia Tanzania hasa katika sekta ya elimu, biashara na uchumi ambazo Qatar imekuwa ikifanya vizuri.
Mazungumzo yakiendelea
Waziri Mahiga akiagana na Balozi Al maadadi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. 

==== Mwisho Mhe. Waziri alikutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia  ====

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Mhe. Wajih Alotaabi alipokuja kumtembelea katika ofisi za Wizara  na kufanya naye  mazungumzo, ambapo katika mazungumzo yao Dkt. Mahiga ameshukuru Taifa la Saudi Arabia kwa kuwa na Mahusiano Mazuri na nchi ya Tanzania, pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Mhe. Alotaabi, kwa kufanikisha ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Ade Al Jubair alipokuja kwa ziara ya kikazi nchini na kuweka saini ya Mkataba wa Ushirikiano wa Uchumi na Uwekezaji.  
Mhe. Wajih Alotaabi naye alitoa shukrani kwa ushirikiano ambao amekuwa akipewa na Wizara na Serikali kwa ujumla katika utekelezaji wa majukumu yake.
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga pamoja na Afisa Mambo ya Nje Bw. Tahiri Bakari, kwa pamoja wakifuatilia mazungumzo kati ya Dkt. Mahiga na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia Mhe. Wajih Alotaabi
Waziri Mahiga akifurahia jambo na Mhe. Wajih Alotaabi mara baada ya kumaliza mazungumzo 
Waziri mahiga katika Picha ya pamoja na Mhe. Alotaabi
Picha ya Pamoja


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.