Monday, June 13, 2016

KATIBU MKUU AKIWA KWENYE SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO MAALUM YA JKT

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Aziz P. Mlima akikagua gwaride liliondaliwa wakati wa sherehe za kufunga mafunzo maalum ya JKT kwaajili ya watumishi 30 walioajiriwa hivi karibuni.
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo maalum ya JKT akitoa salaam maalum ya kijeshi kwa Katibu Mkuu Dkt. Aziz P. Mlima
Katibu Mkuu  Dkt Aziz P. Mlima akimpongeza mmoja wa wahitimu waliofanya vizuri zaidi wakati wa mafunzo maalum ya JKT
Katibu Mkuu Dkt.  Mlima (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Jeshi  mara baada ya kuwasili viunga vya Kikosi namba 832 KJ Ruvu tayari kwa ufunguzi wa sherehe za  kufunga mafunzo maalum ya JKT, wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi Rasrimali watu Bibi Mary Fidelis 
Katibu Mkuu Dkt Azizi P. Mlima (kushoto) akitembelea mradi wa shamba la migomba la Kikosi namba 832 KJ Ruvu kabla ya kuanza kwa  sherehe za kufunga  mafunzo maaalum ya JKT, wakawanza kulia Mkuu wa Kikosi hicho Luteni Kanali Charles Mbuge.
Katibu Mkuu Dkt Aziz P. Mlima (wa kwanza kushoto) akipewa maelezo na Mkuu wa Kikosi namba 832 KJ  Ruvu, Luteni Kanali Charles Mbuge (wapili kulia) alipotembelea mradi wa kufuga kuku unaosimamiwa na kikosi kabla ya kuanza kwa sherehe za kufunga mafunzo maalum ya JKT (operasheni kikwete) yalifanyika katika viwanja vya JKT Ruvu. Mafunzo haya ya wiki sita (6) yalihusisha watumishi 30 wa Wizara ( 13 kati yao wakiwa ni wasichana na 17 ni Wavulana)

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.