Friday, January 29, 2021

PROF. KABUDI ATEMBELEA MAONESHO YA WIKI YA SHERIA DODOMA

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akisaini kitabu cha wagenii katika banda la Mahakama alipotembeea maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katka Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akiangalia picha za waliokuwa Majaji Wakuu wa Tanzania katika banda la Mahakama alipotembeea maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katka Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akiangalia moja ya nyaraaka zinazohusu uendeshaji wa mashauri mahakamani wakati alipotembelea   maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katka Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akisikiliza maelezo ya  jinsi  Mahakama inayotembea inavyoendesha shughuli zake alipotembelea  maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katka Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akisikiliza maelezo juu ya uendeshaji wa mashauri kwa njia ya mtandao unavyofanywa na Mahakama ya Tanzania alipotembelea maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akisikiliza maelezo juu ya ujenzi wa Mahakama unaofanywa na Mahakama ya Tanzania katika  maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akiangalia moja ya vitabu katika banda la Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki alipotembeea maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akisikiliza maelezo ya muoneshaji katika banda la Chuo cha Uongozi wa Mahakama - Lushoto (IJA) katika maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa waoneshaji katika Banda la Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) wanaoshiriki maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (MB) akiulizia kitu katika moja ya machapisho aliyoyakuta katika banda la Wizara ya Katiba na Sheria alipotembelea maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma


Tuesday, January 26, 2021

NAIBU WAZIRI OLE NASHA AKUTANA NA SPIKA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI JIJINI DODOMA

 


Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Martin Ngaga (wa pili kushoto) akizungumza katika kikao na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha walipokutana Ofisini kwa Naibu Waziri jijini Dodoma.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha akisisitiza jambo walipofanya mazungumzo na  Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Martin Ngaga aliyemtembelea  Naibu Waziri Ofisini kwake  jijini Dodoma.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha akisisitiza jambo walipofanya mazungumzo na  Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Martin Ngaga aliyemtembelea  Naibu Waziri Ofisini kwake  jijini Dodoma.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha (wa Pili Kulia)) akiwa na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Martin Ngaga (wa pili kushoto) walipokutana Ofisini kwa Naibu Waziri jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha akisisitiza jambo walipofanya mazungumzo na  Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Martin Ngaga aliyemtembelea  Naibu Waziri Ofisini kwake  jijini Dodoma.

Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Martin Ngaga  akisisitiza jambo alipokutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha Ofisini kwa Naibu Waziri jijini Dodoma.



 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Martin K. Ngoga ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 26 Januari, 2021.

Viongozi hao wamejadili namna watakavyoimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Bunge hilo la Afrika Mashariki na kuliwezesha Bunge hilo kutekeleza majukumu yake kikamilifu huku likizingatia sheria, kanuni , taratibu na uadilifu.

 Akizungumza katika kikao hicho Naibu Waziri Ole Nasha amemtaarifu Spika huyo wa Bunge la Afrika Mashariki kwamba Tanzania imekua ikifanya juhudi kubwa katika kuhakikisha nchi za Afrika ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki zinaimarisha mtangamano na kuongeza kwamba Bunge hilo la Afrika Mashariki ni moja kati ya vyombo muhimu sana katika Jumuiya ya Afrika Mashariki vinavyoimarisha mtangamano.

Amemuomba Mhe. Spika kuendelea kulisimamia Bunge hilo kwa kufuata Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki, Itifaki na Kanuni za Jumuiya ili kuzingatia utawala bora.

Mhe. Naibu Waziri amemkumbusha Spika huyo kwamba Bunge la Afrika Mashariki ni chombo kinachoziangalia taasisi za Jumuiya hivyo lazima kiwe chombo cha mfano kwa Serikali za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika uendeshaji wa shughuli zake na kuzingatia weledi.

Akizungumzia kuhusu bajeti ya Jumuiya kwa mwaka wa fedha 2020/2021, Mhe. Naibu Waziri alimtakia heri katika kupitisha Bajeti hiyo kwenye Mkutano wa Bunge hilo utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi Februari, 2021.

Naye Mhe. Spika Ngoga ameshukuru kwa maoni na msimamo wa Tanzania katika masuala mbalimbali ndani ya Jumuiya na kuelezea masikitiko yake baada ya Bunge kushindwa kupitisha Bajeti iliyowasilishwa na Baraza la Mawaziri la Jumuiya.

Ameahidi kuyafanyia kazi maoni ambayo ameyapokea kutoka kwa nchi wanachama ikiwamo Tanzania kwa ajili ya manufaa ya nchi hizo na wananchi wake na kuongeza kuwa atatumia uzoefu wake kuhakikisha Bajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inapitishwa na Bunge ili shughuli za Jumuiya ziendelee.

 

 

RAIS WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA SHIRIKISHO LA ETHIOPIA AHITIMISHA ZAIRA YAKE YA SIKU MOJA NCHINI


Mheshimiwa Sahle-Work Zewde, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia leo tarehe 25 Januari, 2021 amefanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini ambapo amepokelewa na mwenyeji wake, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uwanja wa ndege wa Chato, uliopo mkoani Geita. 
 
Baada ya mapokezi ya kitaifa Mhe. Zewde na mwenyeji wake Mheshimiwa Rais Mgufuli waliambatana kwenda kuendelea na ratiba ya mazungumzo baina yao, na baadaye wote kwa pamoja walijitokeza kuelezea umma wa Watanzania kupitia waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali yaliyojili na kukubaliana katika mazungumzo hayo.

Rais Magufuli kwa upande wake ameelezea mafanikio yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali kupitia ushirikiano na uhusiano mzuri uliodumu kwa muda mrefu  baina ya Nchi hizi mbili ikiwemo katika sekta ya biashara na uwekezaji. Mhe. Rais ameeleza kuwa kwa miaka ya hivi karibuni biashara kati ya Tanzania na Ethiopia imeendelea kuimarika madhalani, kwa mwaka 2016 biashara ilikuwa bilioni 3.07 na kufikia bilioni 13.55 kwa mwaka 2019/2020. Vilevile miradi 13 yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 14.57 kutoka nchini Ethiopia zimesajiliwa nchini kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania.

Aidha, Rais Magufuli amebainisha maeneo mengine ambayo Taifa litanufaika kutokana na ziara iliyofanywa na Rais Zewde wa Ethiopia nchini, kama vile;  fursa ya kufundisha kiswahili nchini Ethiopia, fursa ya mafunzo katika sekta ya usafiri wa anga ikiwemo urubani na ufundi wa ndege na fursa ya uwekezaji katika sekta ya viwanda vya kuzalisha bidhaa za ngozi nchini. Sambamba na hilo Rais Magufuli ameeleza kuwa amemweleza Rais Zewde kuhusu utayari wa Serikali wa kuwaachia huru wafungwa zaidi ya 1700 raia wa Ethiopia wanaotumikia vifungo gerezani kwa makosa ya kuingia nchini kinyume na taratibu.

Kwa upande wake Rais Zewde ameeleza kuwa Tanzania ni rafiki wa wakati wote wa Ethiopia na ni nchi muhimu Kijiografia ambayo ni lango la kuingilia kanda na nchi zingine za Afrika. "Ethiopia inatambua mchango na ushawishi wa Tanzania hasa katika kutetea masalahi ya Afrika kwenye majukwaa mbalimbali ya Kimataifa" amesema Rais Zewde.  Rais Zewde amesema pamoja na mambo mengine ziara yake ililenga kuja kutoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa kuchaguliwa na kuaminiwa kwa mara nyingine na Watanzania kuiongoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uchaguzi huru na wawazi. Aidha, Rais Zewde ameleeza utayari wake wa kukifanya kiswahili kuwa moja kati ya lugha nying zinazo zungumzwa nchini Ethiopia. 

Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na hadhira iliyojitokeza kwenye mapokezi ya Mheshimiwa Sahle-Work Zewde Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia mara baada ya kuhitimisha mazungumzo na Rais huyo. 

Mheshimiwa Sahle-Work Zewde Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia akizungumza na hadhira iliyojitokeza na kushiriki katika mapokezi yake wakati akiwasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja

Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Sahle-Work Zewde Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Serikali ya Tanzania na Ethiopia
Mheshimiwa Sahle-Work Zewde Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia akiwaaga Watanzania wakati anarejea nchini Ethiopia mara baada ya kuhitimisha ziara ya kikazi ya siku moja nchini.

Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifurahia jambo wakati wa kumhaga Rais Zewde baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini. 

Kwa Heri, Rais Zewde karibu tena wakati mwingine nchini Tanzania

Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Sahle-Work Zewde Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia wakikagua gwaride punde baada ya Rais Zewde kuwasili nchini.

Mheshimiwa Sahle-Work Zewde Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia akipiga ngoma kwenye hafla ya mapokezi ya kumkaribisha alipowasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja
 
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisalimiana na Mheshimiwa Sahle-Work Zewde Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia alipowasili njini kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Monday, January 25, 2021

MHE. SAHLE-WORK ZEWDE, RAIS WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA SHIRIKISHO LA ETHIOPIA KUFANYA ZIARA NCHINI

Mheshimiwa Sahle-Work Zewde, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Tanzania Jumatatu ya tarehe 25 Januari, 2021 kwa mwaliko wa mwenyeji wake, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Sahle-Work Zewde anatarajiwa kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato majira ya saa 4:00 asubuhi na kupokelewa na mwenyeji wake Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Baada ya mapokezi hayo ya Kitaifa, Mheshimiwa Zewde ataendelea na ratiba nyingine zitakazokuwa zimepangwa ikiwemo kufanya mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake.

Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili pamoja na kubadilishana mawazo juu ya masuala mbalimbali ya kikanda na kimataifa yenye maslahi kwa nchi zote mbili.

Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza na waandishi wa habari Chato, Mkoani Geita  ameeleza kuwa, Tanzania na Ethiopia zimeendelea kuwa na uhusiano na ushirikiano mzuri wa muda mrefu. Uhusiano huo unatokana na msingi mzuri uliowekwa na Waasisi wa nchi hizi, Hayati Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na Hayati Haile Sellasie wa Ethiopia ambao walishirikiana katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika na uanzishwaji wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika (Organization of African Unity -OAU) mwaka 1963. 

Profesa Kabudi aliendelea kueleza kuwa Tanzania na Ethiopia zimeendelea kushirikiana katika maeneo mbalimbali ikiwemo kukuza lugha ya Kishwahili,uwekezaji, biashara, utalii, ulinzi na usalama, na usafiri wa anga. "Mwaka 2017, nchi hizi zilisaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) ya kuanzisha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission of Cooperation-JPCC), Azimio la Pamoja la Mkakati wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Ethiopia (Joint Declaration on Strategic Partnership between Tanzania and Ethiopia); na Mkataba wa Ushirikiano katika Sekta ya Utalii (Cooperation in Tourism) ambayo utekelezaji wake unaendelea vizuri". alieleza Profesa Kabudi.

Mashirikiano mengine baina ya Nchi hizi mbili ni pamoja na sekta ya Utalii,uchukuzi,ulinzi na Usalama, utamaduni pamoja na viwanda.

Takwimu za biashara kati ya Tanzania na Ethiopia zinaonesha ongezeko la kiwango cha biashara (Trade Volume) kati ya nchi hizi mbili. Mathalan kiwango cha biashara kiliongezeka kutoka Bilioni 1.5 mwaka 2012 hadi Bilioni 9.3 mwaka 2014 na kufikia Bilioni 13.5 mwaka 2019. Urari wa Biashara (Balance of Trade) uliongezeka kutoka Milioni 946.8 mwaka 2012 hadi Bilioni 12 mwaka 2019. 


Aidha, taarifa ya Profesa Kabudi kwa waandishi wa habari   imeeleza kuwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili miradi 13 yenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 14. 57 kutoka nchini Ethiopia katika kipindi cha kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2020. Miradi hiyo imezalisha ajira 677 kwa Watanzania na ipo katika sekta za viwanda (manufacturing), ujenzi, uchukuzi na Utalii. 

Tanzania ilifungua Ubalozi wake nchini Ethiopia tangu mwaka 1963, Ubalozi huo pia unaiwakilisha Tanzania katika Umoja wa Afrika. Kwa kutambua umuhimu wa uhusiano wetu, Ethiopia nayo ilifungua Ubalozi wake hapa nchini mwezi Mei, 2018.

Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari wakati ambapo aliwajulisha kuhusha ziara ya Mhe.  Sahle-Work Zewde Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia. Kulia ni Balozi Brigadia Generali Wilbert Ibuge Katibu Mkuu Wizara ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki na Mheshimiwa Mhandisi Robert Gabrieli Luhumbi, Mkuu wa Mkoa wa Geita wakifuatalia mkutano.

Mkutano ukiendelea



Friday, January 22, 2021

DKT. MWINYI: MAZINGIRA YA KISIASA ZANZIBAR YANATOA FURSA YA KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO

 Na Mwandishi wetu, Zanzibar   

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar iko salama na mazingira ya kisiasa yanatoa fursa ya kuwaletea wananchi wa Zanzibar maendeleo kutokana na uwepo wa Serikali ya umoja wa kitaifa.

Rais Mwinyi ameyasema hayo Ikulu ya Zanzibar wakati alipokutana na ufanya mazungumzo na uongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi na kuongeza kuwa uongozi wake unajipanga kutimiza ahadi alizotoa kwa wananchi.

Pia Rais Mwinyi ameongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa kipaumbele katika kuimarisha Uchumi wa Bahari kuu hasa Uchumi wa bluu kama chanzo mbadala cha mapato kitakachosaidia kukuza uchumi na kupunguza mzigo wa kodi kwa wananchi.

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimetoa kipaumbele katika kuimarisha Uchumi wa Bahari kuu hasa Uchumi wa bluu kama chanzo mbadala cha mapato kitakachosaidia kukuza uchumi,” Amesema Dkt. Mwinyi  

Katika tukio jingine, Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje umekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ambaye amesisitiza kuwa uchumi wa bluu ni muhimu sana kwa maendeleo ya Zanzibar hivyo ni muhimu kwa Serikali zote mbili (Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) kulinda mipaka yake ya bahari ambapo pia ulinzi huo utasaidia kuzuia na kupambana na uingizwaji wa dawa za kulevya hapa nchini.

“Naamini kabisa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tukishirikiana katika kuimarisha ulinzi wa baharini itasaidia kupunguza uingizwaji wa dawa a kulevya hapa nchini,” Amesema Maalim Seif

Kwa upande wake Prof. Palamagamba John Kabudi ameupongeza uongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kwa hatua ulizozichukua katika kuhakikisha uwepo wa amani na utulivu visiwani humo na kwamba uwepo wa amani na utulivu utachangia kuleta maendeleo haraka kwa wananchi wa Zanzibar.

“Zanzibar imetulia na uchumi wake umezidi kuimarika sote ni mashahidi wa ongezeko la watalii hapa Zanzibar hii ni ishara ya kuwa na amani na utulivu, na jambo hili linachangia kukua kwa uchumi wa Zanzibar,” Amesema Prof. Kabudi

Mbali na kukutana na Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais, pia Uongozi huo umekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya maendeleo yanayohusu Tanzania Bara na Zanzibar hususan yanayohusu Muungano.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi katika ziara yake ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Olenasha pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiongea na uongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) Ikulu Zanzibar wakati wa ziara ya kikazi ya Prof. Kabudi Zanzibar. Prof. Kabudi ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Olenasha pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.  


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiongea na viongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, (hawapo pichani) katika Ikulu ya Zanzibar  


Kikao cha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na uongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikiendelea katika Ikulu ya Zanzibar  


Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi wakati alipokuwa akimuelezea jambo wakati uongozi wa Wizara ulipomtembelea Mhe. Seif kwa zaiara ya kikazi mjini Zanzibar


Kikao cha Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad na uongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kikiendelea katika Ikulu ya Zanzibar  



BALOZI IBUGE AKUTANA, KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR

 Na Nelson Kessy, Zanzibar

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akutana na kufanya mazungumzo na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji katika Afisi za Mwanasheria Mkuu mjini Zanzibar

Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya kazi baina Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Balozi Ibuge amesema kuwa jukumu kubwa la watendaji wa Serikali hizi mbili ni kuhakikisha wanatekeleza maono (vision) viongozi wakuu wa Serikali hasa kwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). “Ni jukumu letu sisi kama watendaji wa serikali kuwasaidia viongozi wetu kutekeleza maoni ya viongozi wetu kwa kuzingatia Ilani ya CCM ya 2020 – 2025,” Amesema Balozi Ibuge.

Kwa upande wake Dkt. Mwinyi Talib Haji amemuahidi Balozi Ibuge kuwa wataendelea kushirikiana katika kuhakikisha kuwa malengo ya serikali zote mbili yanatekelezwa kwa maslahi mapana ya pande zote mbili. 

“Nakuahidi kuwa sisi kama Afisi ya Mwanasheria Mkuu – Zanzibar tutashirikina na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikino wa Afrika Mashariki katika kuhakikisha tunatekeleza majukumu ya serikali,” Amesema Dkt. Haji.

Mwanansheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu Zanzibar leo


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge  akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu Zanzibar, kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi Talib Haji


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge  akiongea na Mwanansheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu Zanzibar


Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji akimkabidhi moja ya zawadi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge


Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mambo ya Nje – Zanzibar Bw. Masoud Balozi Masoud (kushoto) pamoja na Msaidizi wa Katibu Mkuu Bw. Hangi Mgaka (kulia). 


Thursday, January 21, 2021

KAIMU KATIBU MKUU AKUTANA NA BALOZI WA VITNAM


Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Vietnam nchini Mhe. Nguyen Nam Tien ofisini kwake jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamesisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia yaliyopo kati ya Tanzania na Vietnam na kuona jinsi Tanzania inavyoweza kujifunza na kunufaika na utaalam na uwekezaji kutoka Vietnam

Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Katibu Mkuu Balozi Mbundi ameelezea kuridhishwa na namna wawekezaji wa kutoka Vietnam wanavyoendesha shughuli zao nchini huku wakifuata sheria za nchi na kulipa kodi kwa wakati na hivyo kusaidia jitihada za Serikali ya Awamu Tano ya kukuza uchumi wa Nchi.

Pia ameelezea matarajio ya Tanzania katika kunufaika zaidi na mahusiano mazuri na Vietnam hususan katika maeneo ya matumizi ya teknolojia katika Kilimo na Uvuvi .

Naye Balozi Tien amesema Vietnam iko tayari kushirikiana na Tanzania katika maeneo hayo ili kuhakikisha maliasili zilizopo Tanzania zinainufaisha nchi na wananchi wake.

Amesema kwa sasa Ubalozi unafanya mazungumzo na wawekezaji wa nchini kwao ili kuona namna watakavyoshirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuanzisha mazungumzo na Jumuiya ya Wafanyabiashara na Viwanda Tanzania (TCCIA) ili kuwaita wawekezaji wa Vietnam kuja kuwekeza nchini katika viwanda vya kuzalisha korosho nchini hasa ikizingatiwa kuwa Vietnam ni nchi ya pili kwa ununuzi wa Korosho za Tanzania.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi akisalimiana na Balozi wa Viet Nam nchini Tanzania Mhe. Nguyen Nam Tien alipowasili katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma. Wawili hao wamezungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo biashara na uwekezaji baina ya Nchi hizi mbili.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi (kulia) akimsikiliza Balozi wa Viet Nam nchini Tanzania Mhe. Nguyen Nam Tien (kushoto) wakiwa katika mazungumzo yalifanyika katika Ofisi za Wazara jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi akielezea jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Viet Nam nchini Tanzania Mhe. Nguyen Nam Tien.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Viet Nam nchini Tanzania Mhe. Nguyen Nam Tien (hayupo pichani)

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi (kulia) na Balozi wa Viet Nam nchini Tanzania Mhe. Nguyen Nam Tien (kushoto) wakiwa katika mazungumzo yalifanyika katika Ofisi za Wazara jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi (kulia) na Balozi wa Viet Nam nchini Tanzania Mhe. Nguyen Nam Tien wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Ubalozi wa Viet Nam na Wizarani mara baada ya mazungumzo. 





ACTING PS MET WITH VIETNAM AMBASSADOR IN THE CAPITAL DODOMA

The Acting Permanent Secretary in the Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation Ambassador Stephen Mbundi has met with the Vietnamese Ambassador to Tanzania Hon Nguyen Nam Tien in the capital Dodoma.

The two leaders were discussing on ways to strengthening diplomatic relations existing between the two nations as well as attracting investors from Vietnam to come and invest in Tanzania.

Speaking at the meeting, the Acting Permanent Secretary Ambassador Mbundi expressed his appreciations over the role played by Vietnamese investor who are complying with the Tanzanian laws and paying the required taxes which contributes to the country’s economic development and its people.

He said he is optimistic that Tanzania and Vietnam will continue to prosper their cooperation for the mutual benefits of the two nations as well as Tanzania will continue learning and adopting technological advancement and skills from Vietnam in the areas of Agriculture and fishing.

On his side Hon. Ambassador Tien said Vietnam is eager to honour the diplomatic relations which has 55 years and will continue to support Tanzania especially in investing in the area of processing Tanzanian cashewnuts since Vietnam is the second country which buys Tanzanian cashewnuts