Friday, January 15, 2021

BALOZI MBUNDI AONGOZA MAJADILIANO BAINA YA TANZANIA NA POLAND


Mheshimiwa Balozi Stephene P. Mbundi (kulia), Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa na Balozi wa Poland nchini Tanzania  wa kwanza kulia)walipokutana kwa mazungumzo kwenye ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Mheshimiwa Balozi  Mbundi, leo tarehe 15 Januari, 2021, ameongoza majadiliano baina ya Poland na Tanzania.

Mjadiliano hayo yaliyolenga kuimarisha ushirikiano hususan katika masuala ya biashara na  uwekezaji. Kwa upande wa Tanzania washiriki walikuwa ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo; Mjumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango; Watendaji wa NFRA; na Watendaji wa TBA.

Kwa upande wa Poland, walioshiriki ni pamoja na  Mheshimiwa Krzysztof Buzalski Balozi wa Poland nchini Tanzania na Wawakilishi wa makampuni kutoka Poland ya Feerum S.A na Unia Spzo.o.

Mheshimiwa Balozi Stephene P. Mbundi, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa patika picha ya pamoja na Balozi wa Poland nchini Mheshimiwa Krzysztof Buzalski 
Mheshimiwa Balozi Stephene P. Mbundi, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifafanua jambo alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa Poland nchini Mheshimiwa Krzysztof Buzalski 
Sehemu ya wajumbe wakifuatilia mazungumo

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.