Serikali
kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imesema kuwa
dawa ambayo nchi ya Madagascar imeitoa kama msaada kwa Serikali ya Tanzania ni
kwa ajili ya utafiti kwanza.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) amewaambia waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuwa dawa
hiyo inayojulikana kaitaalamu kama "COVIDORGANICS" ni kwa ajili ya
utafiti na siyo kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
"Huu
mzigo (dawa) ni kwaajili ya kufanyiwa utafiti…….na kazi kubwa tunayoianza leo
ni na wataalamu wetu wa afya ni kufanya utafiti," Amesema Prof. Kabudi
Prof.
Kabudi ameongeza kuwa dawa hiyo siyo kwa ajili ya kugawa kwa wananchi, bali ni
kwa ajili ya utafiti na mara baada ya utafiti kukamilika wataalamu wa afya
watatoa maelekezo ya jinsi ya utumiaji wa dawa hiyo.
Aidha,
dawa hiyo imegawanyika katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza la dawa ni
kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya COVID 19 kwa wale ambao hawajaambukizwa
ugonjwa wa Corona. Kundi la pili ni kwa ajili ya matibabu kwa wananchi ambao
tayari wameathirika na COVID 19.
"Dawa
hii tuliyokuja nayo jana kutoka Madagascar mara baada ya utafiti kukamilika na
kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wetu wa afya itatumika kukinga
wananchi ambao hawajaathirika na kutibu wale walioathirika," Prof. Kabudi
Kwa
upande wake Mganga
Mkuu wa serikali Prof. Abel Makubi amesema kuwa mara baada ya kupokea dawa hiyo
kazi ya kwanza ya ni kuanza utafiti ambao utaonesha kama dawa hiyo ni salama na
haina madara kwa wananchi na pili utafiti wa kuangalia ubora wa kutibu au
kupunguza makali ya COVID 19.
"Mara
baada ya utafiti wa dawa hii kukamilika itatumika katika makundi matatu ambayo
kundi la kwanza ni wagonjwa kutumia dawa ya kawaida, kundi la pili watapata
dawa ya kawaida na hii iliyotoka Madagascar na kundi la tatu wagonjwa watatumia
dawa ya kawaida na ile inayozalishwa na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu (Nimr)," Amesema Prof. Makubi
Prof.
Makubi pamoja na mambo mengine, ametoa wito kwa watanzania kuchukua tahadhari
katika kujikinga na ugonjwa wa COVID 19 na wasibweteke na lolote.
Nae
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimr) Prof. Yunus
Mgaya amesema kuwa Nimr imejipanga kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali
hasa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika kuhakikisha inafanya utafiti wa
kina juu ya matumizi ya dawa hiyo.
"Nimr
inafanya tafiti mbalimbali za kupambana na ugonjwa huu wa COVID 19 na
itaendelea kufanya tafiti hizo ili kuwasaidia watanzania," amesema Prof. Mgaya
Kwa
upande wake Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko amesema kuwa Ofisi
ya Mkemia Mkuu inalo jukumu lakuchunguza dawa au sumu zozote kwenye sampuli, kukadiria
kwa usahihi kiasi cha dawa, umetaboli au sumu.
Drkt.
Mafumiko ameongeza kuwa, kupitia utafiti wa dawa hiyo, ofissi yake kwa
kushirikiana na wataalamu wa afya watatafsiri matokeo ya uchunguzi katika dawa
hiyo kutoa maelekezo sahihi juu ya matumizi yake kwa mwananchi.
Mkutano
huu ulihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Mganga Mkuu wa serikali Prof. Abel Makubi, Mkurugenzi
wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimr) Prof. Yunus Mgaya, Mkemia
Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Tiba za
Asili Dkt. Paul Mkama.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) dawa ambayo
imetolewa na Madagascar leo Jijini Dae es Salaam
Mganga
Mkuu wa serikali Prof. Abel Makubi akiongea na waandishi wa habari (hawapo
pichani) wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dae es Salaam
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Yunus Mgaya akiongea
na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika leo
Jijini Dae es Salaam
Mkemia
Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati wa mkutano
Mkuu
wa Kitengo cha Tiba za Asili Dkt. Paul Mkama akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati mkutano ukiendelea
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.