Mkutano huo umefunguliwa na Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Maafisa Waandamizi/ Makatibu Wakuu, Balozi Kanali
Wilbert Ibuge Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki.
Wajumbe wengine ni waliohudhuria
ni Katibu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Prof. Abel
Makubi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utaii Dkt. Aloyce Nzuki pamoja
na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipago, Bi Amina K. Shaaban.
Mkutano wa Baraza la Mawaziri utafanyika
Mei 29, 2020 baada ya kukamilika kwa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Maafisa Waandamizi/Makatibu Wakuu ambapo
pamoja na mambo menine, Kikao cha Maafisa waandamizi kimejadili masuala
mbalimbali ndani ya Jumuiya ikiwemo Mlipuko wa Virusi vya Corona ndani ya SADC.
Mkutano huo utaangalia
utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri kilichofanyika mwezi
Aprili 2020 kuhusu COVID 19 na athari zake katika utekelezaji wa programu za SADC, athari za kijamii na kiuchumi za COVID
-19 na madhara yake ndani ya Jumuiya.
Aidha, Mkutano huu pia umejadili
Hali ya kifedha ndani ya Jumuiya, Utekelezaji wa Maazimio yaliyotokana na kikao
cha Baraza la Mawaziri wa SADC ambayo ni Menejimenti ya Maafa, utekelezaji wa
kaulimbiu ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC isemayo "Mazingira Wezeshi kwa ajili ya
Maendeleo Endelevu na Jumuishi ya Viwanda,
Kukuza Biashara na Ajira ndani ya SADC" na mapitio ya hali halisi ya biashara baina
ya nchi, maendeleo ya viwanda ndani ya Jumuiya na taarifa ya utekelezaji wa Mkakati wa Maendeleo ya Viwanda wa Jumuiya na
Mpango kazi wake.
Mkutano
huo umehusisha wataalamu kutoka nchi wanachama 12 wa SADC kutoka sekta za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Fedha na Mipango, Uchukuzi na Mawasiliano, Viwanda na Biashara, Maliasili
na Utalii pamoja na Afya.
Nchi zilizoshiriki Mkutano huo
ni Angola, Afrika Kusini, Comoro, Eswatini, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia,
Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Zimbabwe na Mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Baadhi ya Makatibu Wakuu wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam |
Baadhi ya
Maafisa waandamizi wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika
kwa njia ya (Video Conference) leo
Jijini Dar es Salaam
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.