Na
Mwandishi wetu, Dar
Watanzania wamepewa changamoto ya kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana Nje ya Nchi ili waweze kuinua uchumi wao pamoja na uchumi wa Taifa kwa ujumla.
Changamoto hiyo imetokewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati alipofanya ziara ya kutembelea Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd leo Jijini Dar es Salaam.
Balozi
Mulamula amewasihi watanzania kuchangamkia fursa za masomo, masoko pamoja na
biashara na uwekezaji na endapo kuna mtanzania anakwama basi asisite
kuwasiliana na Wizara ili asaidiwe kupata ufumbuzi wa changamoto inayomkabili
na kumwezesha kupata fursa husika.
“Fursa
mbalimbali zimekuwa zikitangazwa katika Mashirika na Asasi za Kimataifa lakini
watanzania wamekuwa wazito kiasi flani kuchangamkia fursa hizo, mfano fursa ya
kufundisha lugha ya Kiswahili nje ya nchi, fursa ya kuuza bidhaa za kilimo nje
ya nchi na nyingine nyingi………rai yangu kwa watanzania tuchangamkie fursa hizi
ili tuweze kuinua kipato na uchumi wetu na taifa kwa ujumla,” amesema Balozi
Mulamula
Pia
Balozi Mulamula amewahakikishia ‘Diaspora’ kuwa serikali inatambua na kuthamini
mchango wao na kwa sasa inaendelea kuandaa Sera ya Mambo ya Nje ili kuwawekea
mazingira bora na salama ya uwekezaji nchini.
Pamoja na mambo mengine, Balozi Mulamula ameipongeza Kampuni ya Mwananchi kwa kuhabarisha na kuelimisha jamii kwa weledi wa taaluma ambao umekuwa ukiwawezesha wananchi kufahamu mambo mbalimbali yanayoendela nchini.
“Vyombo
vya habari vya Mwananchi ni mdau muhimu sana kwani vimekuwa vikihabarisha na
kuelimisha wadau mbalimbali mambo mazuri yanayotekelezwa na Serikali ya
Tanzania,” amesema Balozi Mulamula
Balozi
Mulamula ameongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki itaendelea kushirikiana kwa karibu na vyombo vya habari katika
kuhakikisha kuwa vinaitambulisha vyema Serikali ya Tanzania vyema katika
mataifa mbalimbali.
Balozi
Mulamula ametembelea Kampuni ya Mwananchi Communications Limited wachapishaji
wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti na kujionea shughuli
zinavyofanyika pamoja na kuongea na wahariri wa Magazeti hayo.
Tarehe
04 Juni, 2021 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Liberata Mulamula alifanya ziara yake ya kwanza katika vyombo vya habari vya
habari vya IPP ambavyo ni ‘The Guardian Ltd’ inayozalisha magazeti ya The
Guardian na Nipashe, Radio One, Capital radio, East Africa radio, ITV, Capital
TV pamoja na East Africa TV.
1. Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications
Limited Bw. Bakari Machumu akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi za Mwananchi
Communications Ltd Jijini Dar es Salaam. Mwingine ni Naibu Mhariri Mtendaji
Mkuu wa Mwananchi, Bw. Rashid Kejo
1. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwaelezea jambo Mhariri
Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications Limited Bw. Bakari Machumu pamoja na Naibu
Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi, Bw. Rashid Kejo
1. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiangalia gazeti la Mwananchi wakati wa kikao
1. Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications
Limited Bw. Bakari Machumu akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki nakala za Magazeti ya Mwananchi, The Citizen pamoja na
Mwanaspoti
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza
mmoja kati ya wafanyakazi wa mwananchi
1. Naibu Mhariri Mtendaji Mkuu wa
Mwananchi, Bw. Rashid Kejo akimuonesha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula namna magazeti yanavyohifadhiwa
katika jalada maalum
Kikao cha Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na
wahariri wa Mwananchi Communications Limited kikiendelea
1. Kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na wahariri wa
Mwananchi Communications Limited kikiendelea
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.