|
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen
Byabato
(Mb.) (wa tatu kutoka kushoto) akizungumza na vijana wa Kitanzania
waliorejeshwa nyumbani na Serikali kutoka nchini Israel kufuatia
changamoto za kiusalama nchini humo wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.
Samwel Shelukindo |
|
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen
Byabato
(Mb.) (wa pili kushoto) akizungumza na vijana wa Kitanzania
waliorejeshwa nyumbani na Serikali kutoka nchini Israel kufuatia
changamoto za kiusalama nchini humo wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.
Samwel Shelukindo |
|
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen
Byabato
(Mb.) akizungumza na vijana wa Kitanzania waliorejeshwa nyumbani na
Serikali kutoka nchini Israel kufuatia changamoto za kiusalama zilizoikumba nchini hiyo katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuwapokea vijana hao |
|
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen
Byabato
(Mb.) akisalimiana na Bw. Lucas Malaki ambaye ni mmoja wa vijana wa Kitanzania waliorejeshwa nyumbani na
Serikali kutoka nchini Israel kufuatia changamoto za kiusalama zilizoikumba nchini
hiyo |
|
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen
Byabato
(Mb.) akizungumza na vijana wa Kitanzania (hawapo pichani ) ambao
wamerejeshwa nyumbani na
Serikali kutoka nchini Israel kufuatia changamoto za kiusalama
zilizoikumba nchini
hiyo, nyuma yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo na Mkurugenzi wa Idara
ya Mashariki ya Kati wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Abdallah Kilima walipofika uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam kuwapokea vijana hao
|
|
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen
Byabato
(Mb.) akimsikiliza kijana Lucas Malaki aliyerejea nchini kutoka Israel kufuatia changamoto za kiusalama zilizoikumba nchini
hiyo |
Watanzania 9 waliokuwa nchini Israel wamerejea nyumbani leo tarehe 18
Oktoba 2023 na kulakiwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato
(Mb.) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza katika mapokezi ya Watanzania hao Naibu Waziri Byabato amesema
kurejea nyumbani kwa Watanzania hao kunatokana na utekelezaji wa uamuzi wa
Serikali ya Tanzania wa kuwarejesha nyumbani raia wake walioko nchini Israel
ili waendelee kuwa salama.
Amesema Serikali kupitia Ubalozi wake wa nchini Israel iliweka utaratibu wa
kuwarejesha Watanzania wote ambao wangetaka kurudi nyumbani na kuongeza kuwa
Serikali itaendelea kuwashawishi Watanzania walioko nchini humo ili waone haja
ya kurudi nyumbani hadi pale hali itakapotengemaa.
Amesema Serikali imefarijika kwa Watanzania hao kuitikia wito wa kuokoa
maisha yao na anaamini kuwa Watanzania waliobaki nchini humo busara zao
zitawaongoza na kuamua kurejea nyumbani ili wawe salama na kuongeza kuwa
Serikali itawarejesha nyumbani watakapokuwa tayari kufanya hivyo.
Akizungumza baada ya mapokezi hayo mmoja wa Watanzania hao Bw. Lucas Malaki
ameishukuru Serikali kwa kitendo cha kuwarejesha nyumbani na kusema kuwa
kitendo hicho kimewafanya wajisikie fahari kuwa watanzania na kuwaondolea
unyonge na kuongeza kuwa wanakichukulia kitendo hicho kuwa ni cha upendo na cha
kizalendo na kuahidi kuwa wataendelea kuwa raia wema.
Watanzania hao wamerejeshwa nyumbani na Serikali kufuatia kuendelea
kuzorota kwa hali ya amani na usalama
nchini Israel na maeneo mengine ya jirani tangu kikundi cha HAMAS
kilipoishambulia Israel tarehe 7 Oktoba, 2023.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.