Tuesday, October 10, 2023

DKT. MWINYI AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA MAKUMBUSHO YA TAIFA YA OMAN

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akipokea vitabu kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi aliyemtembelea Ikulu Zanzibar na kuzungumza naye

  

Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi alipomtembelea Ikulu Zanzibar


Ujumbe ulioshiriki kikao kati ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi aliyemtembelea Ikulu Zanzibar  kuzungumza naye


Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati -Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Abdallah Kilima akaiwa na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar Balozi Silima Kombo Haji waliposhiriki kikao kati ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi aliyemtembelea Ikulu Zanzibar 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (katikati) katika picha ya pmoja na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi na ujumbe wake alipomtembelea Ikulu Zanzibar na kuzungumza naye


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi alipomtembelea Ikulu Zanzibar na kuzungumza naye

 

 

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.
Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na kuzungumza na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi na ujumbe wake Ikulu Zanzibar.

Katika mazungumzo yao Mhe. Rais Dkt.Mwinyi amemkaribisha Mhe. Jamal al-Moosawi Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwa kuzingatia kuwa nchi hizo zina historia maalum na kuongeza kuwa kupitia historia hiyo nchi hizo zinaweza kunufaika na fursa za kubadilisha taarifa za kihistoria, uzoefu wa kutunza na kuhifadhi mali kale na kujengeana uwezo katika eneo la uendeshaji wa Makumbusho za Taifa.

“Ni kweli kuwa Tanzania na hasa Zanzibar tuna historia maalum na Oman, tunaweza kutumia kigezo hicho kama fursa za kuendeleza ushirikiano kati yetu katika nyanja tofauti za historia, uhifadhi wa mali kale na ni wahakikishie kuwa Serikali iko tayari kuendeleza ushirikiano wetu,” alisema Dkt . Mwinyi.

Akizungumza katika kikao hicho Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi ameelezea nia ya Serikali ya Oman katika kushirikiana na Tanzania katika eneo la uhifadhi na ulinzi wa malikale, usimamizi wa Makumbusho za Taifa, uandaaji wa taarifa katika makumbusho na uwasilishaji wa taarifa kwa watalii na wageni mbalimbali na kuiwezesha sekta ya Malikale na Makumbusho za Taifa kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi.

Mhe. Jamal alisema hii ni mara ya kwanza kwa taaisisi yao kuja Tanzania kwa lengo la kujifunza na kuona jinsi historia kati ya Tanzania na Oman ilivyotunzwa na kuhifadhiwa nchini.

Amesema ni matarajio yao kuwa ujio wao utawawezesha kuelewa jinsi wanavyoweza kushirikiana na Tanzania katika eneo hilo la makumbusho na uhifadhi wa malikale na namna wanavyoweza saidia na kuwekeza katika eneo hilo.

Aliongeza kuwa ziara yao hiyo itawawezesha kujua aina ya msaada wanaoweza kutoa ikiwa ni pamoja na kuona maeneo mapya ya ushirikiano ambayo wanaweza kuanzisha na kushirikiana na Tanzania.

Ukiwa nchini ujumbe huo kutoka Makumbusho ya Taifa ya Oman ulishiriki Mkutano wa Kwanza wa Pamoja wa Wataalamu kati ya Tanzania na Oman uliofanyika jijini Dar es Salaam, ulitembelea Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam, Makumbusho ya Kijiji cha Makumbusho, Makumbusho ya Kunduchi na Mji Mkongwe wa Bagamoyo na kujionea historia na malikale zilizopo katika makumbusho hayo.

Ukiwa Zanzibar ujumbe huo umekutana na kuzungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bi. Fatma Mbarouk na watendaji wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale.

 

Ujumbe huo pia umetembelea Mji Mkongwe, Makumbusho ya amani na historia ya Mnazi Mmoja, Jumba la Kibweni na Magofu ya Mtoni, Pango la Kuumbi la Jambiani, Makumbusho ya Unguja Kuu na kujifunza na kujionea historia na mali kale zilizopo Zanzibar.


Ujio wa ujumbe huo ni matunda ya ziara zilizofanywa na viongozi wa Tanzania nchini Oman katika miaka ya hivi karibuni ina lenga kuendelea kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Oman.

 

Ujumbe huo unatarajiwa kuondoka nchini tarehe 12 Oktoba 2023 kupitia Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.