|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mhe. January Makamba (Mb.) akipokea Hati za Utambulisho za mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara
katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mhe. January Makamba (Mb.) akipeana mikono na Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara
baada ya kupokea Hati za Utambulisho za mwakilishi huyo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mhe. January Makamba (Mb.) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara
baada ya kupokea Hati za Utambulisho za mwakilishi huyo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. |
|
Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mhe. January Makamba (Mb.) baada ya kukabidhi Hati zake za Utambulisho katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mhe. January Makamba (Mb.) katika picha na Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara
baada ya kupokea Hati za Utambulisho za mwakilishi huyo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mhe. January Makamba (Mb.) na ujumbe wake (kulia) katika picha na Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara
na ujumbe wake (kushoto) baada ya kupokea Hati za Utambulisho za mwakilishi huyo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mhe. January Makamba (Mb.) amepokea Hati za Utambulisho za mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Shigeki Komatsubara
katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kupokea nakala za hati hizo, Mhe. Waziri
Makamba amemhakikishia Bw. Komatsubara kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na
UNDP ili kusogeza mbele agenda yake ya maendeleo na hivyo kuinua maisha ya
watanzania kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Mhe. Waziri amesema Tanzania na UNDP zimekuwa zikishirikiana
kutekeleza mipango ya maendeleo kwa kuwa zina lengo la kuboresha maisha ya watu
kupitia maeneo ya utawala wa demokrasia, ukuaji uchumi, maendeleo endelevu mazingira endelevu na uhimilivu wa mabadiliko
ya tabia nchi.
Waziri Makamba ameongeza kuwa Tanzania inathmini na kutambua
jitihada za UNDP katika kukabiliana na madhara yaliyotokana na janga la UVIKO
19
Kwa upande wake Mwakilishi wa UNDP nchini, Bw. Komatsubara
ameahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuendeleza jitihada za UNDP nchini na
kuongeza kuwa atakuwa sio tu Balozi mzuri wa Tanzania bali pia atakuwa mtangaza
mazuri ya Tanzania kupitia kazi zake.
Bw. Komatsubara ameongeza kuwa ofisi yake ina nia ya
kusaidia Tanzania kujenga uwezo kwa
watu wake ili kutekeleza kwa ufanisi mipango ya maendeleo na kwamba
atahakikisha UNDP inaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha kuwa
ajenda ya maendeleo
inafanikishwa.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.