Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amefungua rasmi Jukwaa la Uwekezaji kati ya Tanzania na India lililofanyika jijini New Delhi tarehe 10 Oktoba 2023.
Akifungua Kongamano hilo lenye kaulimbiu isemayo “Strong, Togerher ," Mhe. Rais Dkt. Samia amewakaribisha
wawekezaji wa India kuja nchini kuwekeza kwenye sekta mbalimbali zikiwemo
kilimo, afya, Tehama, Utalii na Miundombinu na kuwahakikishia mazingira
mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara.
Amesema Tanzania imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji
biashara kwa kurekebisha baadhi ya sheria za usimamizi wa biashara,
kuboresha huduma na miundombinu, teknolojia pamoja na kuishirikisha
kikamilifu sekta binafsi.
Ameongeza kuwa kutokana na jitihada hizo, viwango vya biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na India vimeongezeka mwaka ha ambapo kwa
takwimu za Tanzania za mwaka 2021/2022 India ni miongoni mwa nchi
tano zinazoongoza kwa uwekezaji nchini kwa kuwekeza miradi 630 yenye thamani ya
Dola za Marekani 3.7 ambayo imetengeneza ajira kwa watanzania 60,000.
Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara wa India Mhe. Shri Piyush
Goyal amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika
kuboresha mazingira yabuwekezaji na kwamba ziara ya Mhe. Dkt. Samia inafungua
ukurasa mpya wa ushirikiano kwenye sekta muhimu ikiwemo biashara na uwekezaji.
Awali akizungumza kwenye kongamano hilo Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi
Tanzania, Bi. Angelina Ngalula amepongeza jitihada zinazofanywa na
Serikali hizi mbili katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara.
Amesema kutokana na jitihada hizo jukwaa hilo limehudhuriwa na zaidi ya
wafanyabiashara na wawekezaji 250 kutoka Tanzania na India ambapo kati
yao 80 wanatoka Tanzania katika sekta za Benki, Uchukuzi,
Uzalishaji viwandani, TEHAMA, Burudani na Ubunifu wa mitindo.
Kongamano hilo ambalo limebeba mada isemayo " Nafasi ya Sekta Binafsi
katika kuimarisha Biashara kati ya Tanzanaia na India litahitimishwa kwa
kupitisha Azimio na Mapendekezo mbalimbali yanayolenga kuboresha sekta ya
biashara na uwekezaji kati ya nchi hizi mbili.
Sehemu ya wawekezaji kutoka Inida pamoja jumbe wa Tanzania wakifuatilia Mkutano wa Jukwaa la Uwekezaji kati ya Tanzania na India |
Mkutano wa Jukwaa la Uwekezaji kati ya Tanzania na India ukiendelea |
Mhe. Rais Dkt. Samia akishuhudia ubadlishanaji wa Hati za Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India kwenye sekta ya uwekezaji |
Mhe. Rais Dkt. Samia akishuhudia ubadlishanaji wa Hati za Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India kwenye sekta ya biashara |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.