![]() |
Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akipanda mti alipotembelea Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam |
![]() |
Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akiwa ndani ya nyumba iliyohifadhiwa katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam alipotembelea makumbusho hiyo |
![]() |
Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhifadhi wa makumbusho alipotembelea Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam |
![]() |
Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akiangalia ngoma ya utamaduni alipotembelea Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam |
![]() |
Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhifadhi wa makumbusho alipotembelea Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam |
![]() |
Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi katika picha ya pamoja na ujumbe wake walipotembelea Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam |
Ujumbe kutoka Makumbusho ya Taifa ya Oman ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho hiyo Mheshimiwa Jamal al-Moosawi umetembelea Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujifunza na kujionea historia, mila na tamaduni za makabila mbalimbali ya Tanzania.
Ujumbe
huo kutoka nchini Oman ambao uko nchini umeambatana na Mkurugenzi wa
Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Balozi Abdallah Kilima na Balozi wa Oman nchini
Tanzania Mheshimiwa Saud bin Hilal Alshaidani.
Ujumbe huo pia
uliambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa Dkt. Oswald
Masebo na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Noel Lwoga.
Akiongea
baaada ya kutembelea Kijiji cha Makumbusho Mhe. Al Moosawi alielezea
kuridhishwa kwake na uhifadhi wa historia ya makabila ya Tanzania ambayo
ameisikia na kuona jinsi nyumba za makabila hayo kama zilivyooneshwa
katika eneo hilo na kupongeza jitihada za kuhifadhi historia hiyo kwa
ajili ya vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.
Kijiji cha makumbusho
ni eneo linalohifadhi mifano ya nyumba na vifaa vya makabila na
tamaduni mbalimbali zinazopatikana Tanzania.
Eneo hilo lilianzishwa
mwaka 1966 kwa ajili ya kuonyesha na kutunza tamaduni za asili, ngoma na
tamaduni za makabila mbalimbali kama Wanyakyusa, Wamakonde, Wamasai,
Wachagga, Wahaya, Wangoni, Wayao na mengine mengi.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.