Sunday, October 8, 2023

MTENDAJI MKUU WA MAKUMBUSHO YA TAIFA YA OMAN ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA KAOLE- BAGAMOYO



Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mheshimiwa Jamal al-Moosawi akiangalia mabaki ya vitu mbalimbali vilivyohifadhiwa katika  Makumbusho ya Kaole mjini Bagamoyo Mkoani Pwani alipotembelea kujionea historia ya mabaki ya mawe ya zamani, magofu na vitu vingi vya kale yakiwemo makaburikatika makumbusho hiyo


Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal Al-Moosawi akiangalia mabaki ya vitu mbalimbali vilivyohifadhiwa katika makumbusho ya Kaole mjini Bagamoyo


Mhifadhi wa makumbusho katika Makulbusho ya Kaole mjini Bagamoyo akimuelezea Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal Al-Moosawi historia ya vitu vivyohifadhiwa katika Makumbusho hiyo


Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akiangalia gofu lenye mnara mrefu alipotembelea Makumbusho ya Kaole mjini Bagamoyo


Balozi wa Oman nchini Mhe. Saud bin Hilal Alshaidani akisoma  historia ya watu na mabaki ya vitu mbalimbali vilivyohifadhiwa katika Makumbusho ya Kaole mjini Bagamoyo alipotembelea makumbusho hiyo

Balozi wa oman nchini Mhe. Saud bin Hilal Alshaidani akinawa maji maarufu yanayopatikana katika kisima kinachoaminika kuchimbwa katika karne ya 13 mjini Bagamoyo katika Makumbusho ya Kaole  alipotembelea makumbusho hiyo

Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akiangalia Kisima cha maji maarufu yanayopatikana katika kisima kinachoaminika kuchimbwa na kutumika katika karne ya 13 mjini Bagamoyo katika Makumbusho ya Kaole  alipotembelea makumbusho hiyo


Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akinawa maji ya kisima maarufu ya kaole alipotembelea makumbusho hayo
Mmoja wa wageni kutoka Makumbusho ya Taifa ya Oman akinawa maji maarufu yanayopatikana katika makumbusho ya kaole mjini Bagamoyo walipotembelea makumbusho hayo mjini Bagamoyo mkoani Pwani

 

Ujumbe wa Makumbusho ya Taifa ya Oman ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mheshimiwa Jamal al-Moosawi umetembelea Makumbusho ya Kaole yaliyoko Bagamoyo Mkoani Pwani na kujionea mabaki ya mawe ya zamani, magofu na vitu vingi vya kale yakiwemo makaburiambayo ni sehemu ya historia ya kale vilivyotumiwa na Waarabu katika karne ya 13 mpaka karne ya 16.
 

Ujumbe huo kutoka Oman ambao uko nchini kukutana na wenzao wa Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Oman ulihudhuria Mkutano wa Kwanza wa Pamoja wa Wataalamu kati ya Makumbusho ya Taifa ya Tanzania na Makumbusho ya Taifa ya Oman.
 

Ujumbe huo uliambatana na Balozi wa Oman nchini Tanzania Mheshimiwa Saud bin Hilal Alshaidani Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa Dkt. Oswald Masebo na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Noel Lwoga.

Ujumbe huo kutoka Makumbusho ya Taifa ya Oman unatarajia kwenda katika Visiwa vya Zanzibar ambako utatembelea Mji Mkongwe, Makumbusho ya amani na historia ya Mnazi Mmoja, Jumba la Kibweni na Magofu ya Mtoni. 

Ujumbe huo pia utatembelea Pango la Kuumbi la Jambiani na Makumbusho ya Unguja Kuu kwa ajili ya kujifunza na kujionea historia ya Zanzibar. 


Ujumbe huo kutoka nchini Oman uliwasili nchini tarehe 05 Oktoba, 2023 unatarajiwa kuondoka nchini tarehe 12 Oktoba 2023 kupitia Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.