Wednesday, May 15, 2024

TANZANIA NA UFARANSA ZASAINI TAMKO LA PARIS

Tanzania na Ufaransa zimesaini Tamko la Paris (Paris Declaration) katika kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi uliopo baina ya nchi hizo mbili.

Tamko hilo limesainiwa leo tarehe 14 Mei, 2024 jijini Paris Ufaransa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba na Waziri wa Ufaransa anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa, Mhe. Chrysoula Zacharopoulou.

Maeneo ya ushirikiano yaliyosainiwa ni pamoja na Nishati na mabadiliko ya tabianchi, usafirishaji na maendeleo ya miundombinu, usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake.

Hafla ya utiaji saini imeshuhudiwa na Mabalozi wanaowakilisha katika hizo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Ali Jabir Mwadini, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Nabil Hajlaoui, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda na Maafisa wengine Waandamizi walioambatana na Viongozi hao wawili.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (kushoto) pamoja na Waziri wa Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa ufaransa, Mhe. Chrysoula Zacharopoulou wakisaini Tamko la Paris tarehe 14 Mei, 2024.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Ali Jabir Mwadini (kati), Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Athuman Kikwete wakishuhudia utiaji saini wa Tamko la Paris.

Hafla ya utiaji saini Tamko la Paris.

Picha ya Pamoja 

Waheshimiwa Mawaziri wakibadilisha Hati za Tamko baada ya kutia saini.

Picha ya pamoja waheshimiwa Mawaziri na Waheshimiwa Mabalozi waoawakilisha nchini Ufaransa na Tanzania.

Mhe. Waziri Makamba na Mhe. Chrysoula Zacharopoulou wakiteta baada ya kukamilisha zoezi la utiaji saini.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.