Wednesday, May 22, 2024

WAZIRI MAKAMBA AAGANA NA BALOZI WA ITALIA NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba ameagana na Balozi wa Italia nchini ambaye amemaliza muda wake wa utumishi nchini hapa nchini.

Akizungumza katika kikao hicho Waziri Makamba amemtakia kila la heri Balozi Lambardi na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Italia.

“Uliukuta uhusiano wa Tanzania na Italia ukiwa katika hali nzuri lakini kwa nguvu, jitihada na weledi wako umeufanya uhusiano wetu kuwa katika kiwango cha juu kabisa, tunakupongeza na kukushukuru sana,” alisema Waziri Makamba.

Naye Balozi Lambardi ameishukuru Wizara na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano mkubwa iliyompatia wakati wote ambao amekuwa kitekeleza majukumu yake nchini.

“Mhe. Waziri niwashukuru sana Wizara na hasa Idara ya Ulaya na Amerika kwa kushirikiana nami na kufanya utendaji wangu kukamilika bila kukwama, asanteni sana” alisema Balozi Lambardi.

Amesema ana amani kuwa anaondoka nchini huku akiuacha mpango wa Matei ukiwa katika hatua nzuri ya utekelezaji.










 


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.