Tuesday, June 19, 2018

Ziara ya Waziri Mahiga katika picha

KIKAO CHA KAZI CHA UJUMBE WA WAZIRI MAHIGA NA MHE. DKT. WILBROAD SLAA, BALOZI WA TANZANIA NCHINI NORWAY MWENYE MAKAZI YAKE NCHINI SWEDEN

Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akipokea taarifa ya kazi kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Norway mwenye makazi yake Stockholm Sweden, Mhe. Dkt. Wilbroad Slaa, katika Hoteli ya Grand Oslo iliyopo kwenye mji wa Oslo, Norway.  


Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akiwa kwenye kikao cha kazi na ujumbe wake mara baada ya kuwasili Mjini Oslo, Norway kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Kwenye ziara hiyo Waziri Mahiga ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara Prof. Adolf Mkenda (kulia kwa Waziri), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani Bw. Jestus Nyamanga, Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati Bw. Adamu Zuberi, pamoja na maafisa waandamizi wa Mambo ya Nje. 



KIKAO CHA KAZI CHA UJUMBE WA WAZIRI MAHIGA KWENYE KAMPUNI YA STATOIL (EQUINOR) NA WATENDAJI WA KAMPUNI HIYO YENYE MAKAO YAKE MAKUU MJINI OSLO, NORWAY.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda akisalimiana na Makamu wa Rais Mtendaji wa STATOIL Bw. Lars Christian Bacher mara baada ya ujumbe wa Waziri Mahiga kuwasili kwenye makao makuu ya kampuni hiyo Oslo, Norway. Wengine kwenye picha ni Mhe. Dkt. Wilbroad Slaa, Balozi wa Tanzania nchini humo, na Bw. Adamu Zuberi, mtaalam wa Wizara ya Nishati.

Balozi wa Tanzania nchini Norway, Mhe. Dkt. Slaa akisalimiana na Watanzania wawili Nyarobi na Eunice, wanaofanya mafunzo ya vitendo kwenye kampuni hiyo, baada ya kumaliza mafunzo ya shahada ya uzamili kwenye Chuo Kikuu Norway. 

Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Hanne Marie Kaarstad akizungumza kwenye kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo. Pichani chini Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho. 


Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje akipokea zawadi kutoka kwa Bw. Lars Christian Bacher, Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya Statoil. Pichani chini, Mkurugenzi Bacher akimkabidhi zawadi Mhe. Dkt. Wilbroad Slaa, Balozi wa Tanzania nchini Norway baada ya kikao hicho kumalizika kwa mafanikio makubwa. 


Picha ya pamoja 
Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa kwenye picha na Mtanzania Nyarobi aayefanya mafunzo ya vitendo kwenye kampuni ya Statoil akiwa na mmoja wa Wakurugenzi watendaji wa kampuni hiyo.



Waheshimiwa Balozi Dkt. Slaa na mwenzake Balozi Kaarstad wanaowakilisha nchi zao Tanzania na Norway wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa kitanzania Eunice na Nyarobi walionufaika na ufadhili wa kampuni ya Statoil kwenye masomo ya shahada ya uzamili ambao wanaendelea kupata mafunzo ya vitendo.


KIKAO CHA KAZI CHA UJUMBE WA WAZIRI MAHIGA NA UONGOZI WA SHIRIKA LA MAENDELEO LA NORWAY, NORAD MJINI OSLO NORWAY

Ujumbe wa Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukiwa kwenye kikao cha kazi na Ujumbe wa Mkurugenzi wa Norad Bw. Jon Lamoy. Norad ni Shirika la Maendeleo ya Norway linalofadhili miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Norway. Shirika hilo lipo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo. 


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani kwenye Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania Bw. Jestus Nyamanga akiwa na ujumbe wa Mhe. Waziri Mahiga, wakati wa kikao cha kazi na Shirika la Maendeleo la Norad la Serikali ya Norway.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.