Thursday, December 10, 2020

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE ALA KIAPO CHA UTII BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Olenasha, ameapa kiapo cha Utii cha Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mhe. Olenasha ameapa kiapo hicho na kushuhudiwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Martin Ngoga pamoja na wabunge wengine wanaounda Bunge hilo ili kumwezesha kushiriki kwenye Bunge hilo kama Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mhe. Olenasha ameapa kiapo hicho akiwa katika Ofisi za Wizara zilizopo kwenye Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma wakati wa kikao kilichofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 10 Desemba 2020.

Aidha, kikao hicho kimehudhuriwa na Wabunge wa Bunge hilo ambao wengi wameshiriki kutokea kwenye nchi zao wakati Mhe. Spika akiwa Makao Makuu ya Bunge hilo jijini Arusha.

Kikao hicho, pamoja na mambo mengine kimejadili Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Afrika Mashariki ya Masuala Mtambuka

 



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Olenasha akiapa kiapo cha utii na uadilifu mbele ya Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Ngoga Martin   


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Olenasha akiapa kiapo cha utii na uadilifu mbele ya Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Ngoga Martin   

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Mhe. Josephine Sebastian Lemoyan akimtambulisha Mhe. Olenasha kwenye Bunge hilo kama Mjumbe mpya

Mhe. Olenasha akisaini Hati ya Kiapo baada ya kula kiapo cha utaii cha kushiriki Bunge la Afrika Mashariki


Mhe. Olenasha kwa pamoja na Mhe. Josephine wakifuatilia mjadala uliokuwa ukiendelea wakati wa kikao cha Bunge la EALA


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Olenasha akichangia jambo wakati wa kikao  


Mhe. Olenasha na Mhe. Josephine wakifuatilia mjadala wakati wa kikao hicho



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.