Tuesday, March 17, 2015

Waziri Mkuu akutana na Watanzania waishio nchini Japan

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Bibi wa Kijapan, Midori Uno,machi 17, 2015 kwenye hoteli ya New Otani jijini New York , ambaye aliishi Tanzania miaka ya 60 baada ya Uhuru wa Tanganyika akifanya kazi kwa kujitolea. Hisasa Bibi Uno ni bingwa wa lugha ya kiswahili na amekwishaandika Kamusi ya Kijapan na Kiswahili pamoja na vitabu kadhaa.
Waziri mkuu, Mizengo Pinda na mkewe wakitia saini kitabu cha wageni kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Tokyo nchini Japan baada ya kuwasili ubalozini hapo kuzungumza na Watanzania waishio Japan Machi 17, 2015. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Japan aliyemaliza muda wake, Salome Sijaona na Wapili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Abood Mohamed. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Batilda Buriani na wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Mahadh Maalim.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania waishio nchini Japan.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.