Monday, March 30, 2015

Picha na Matukio ya Ufunguzi wa Jengo la Tanzania Jijini New York


Jengo la ghorofa sita la Ofisi za Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Jengo hilo lipo karibu na Ofisi za Umoja wa Mataifa anuani namba 307 East 53rd Street, 4th Floor, New York, N.Y. 10022. 

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akifurahia jambo baada ya kuwatambulisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Mahadhi Juma Maalim na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue kwa mabalozi wa nchi za Kiafrika waliohudhuria uzinduzi wa jengo hilo.

Balozi Ombeni Sefue akisalimiana na baadhi ya Watanzania waishio Jijini New York wakati wa uzinduzi wa jengo. Balozi Sefue aliwahi pia kuwa Balozi wa Tanzania hapa New York kwenye Umoja wa Mataifa na pia Washington DC. 
Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiangalia picha ya utalii wa Tanzania iliyopo kwenye eneo la mapokezi la jengo jipya la Tanzania jijini New York Marekani wakati wa ufunguzi.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bw. Alfred Swere, Mhasibu wa Ubalozi wa Tanzania Washington D.C. ambaye pia alikuwa mhasibu wa Ubalozi wa NY wakati jengo hilo likinunuliwa. Wengine pichani ni baadhi ya watumishi wa Serikali Bw. Noel Kaganda, Bw. Lucas Suka, Mkurugenzi wa Ugavi na Manunuzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Watanzania waliofika kwenye uzinduzi huo.


Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bi. Roselinda Mkapa mfanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mindi Kasiga. 

Mhe. Rais Jakaya Kikwete kwenye picha na wana diaspora waishio New York. (kutoka kushoto) Bw. Meck Khalfan aliyebuni power bank PUKU, mwanamitindo Flaviana Matata na Rosemary Kokuhilwa pia mwanamitindo wa Kitanzania anayefanya shuguli za ujasiriamali jijini New York, Marekani. 
Baadhi ya Maafisa wa Ubalozi ambao walishiriki kwenye uzinduzi huo. (kushoto-Kulia) Noel Kaganda, Justin Kisoka na Alfred Swere. 

Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (kutoka kushoto) Noel Kaganda (kwa sasa ni Mshauri wa Mhe. Sam Kutesa, Rais wa Kikao cha 69 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ), Baraka Luvanda (kwa sasa ni msaidizi wa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Ikulu Dar es salaam), Mindi Kasiga (kwa sasa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa) na Togolani Mavura (kwa sasa ni Msaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu).

Maafisa Mambo ya Nje na Wasaidizi wa Viongozi wa Serikali,  Bw. Togolani Mavura ; Msaidizi wa Rais Hotuba na Bw. Adam Issara; Msaidizi wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakipitia hotuba za viongozi wakati wa uzinduzi wa jengo la Tanzania jijini New York, Marekani.   

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.