Saturday, May 25, 2013

Matukio mbalimbali kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (OAU/AU)

Msemaji wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50  ya Uhuru wa Umoja wa Afrika (AU) Bw. Emmanuel Luangisa ambaye ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akimkaribisha Mgeni Rasmi, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kutoa hotuba wakati wa maadhimisho hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Membe akitoa hotuba wakati wa kuadhimisha miaka 50 ya AU-OAU. Wengine katika picha ni Mhe. Balozi Juma Khalfan Mpango (kulia), Mkuu wa Mabalozi, Mhe. Ambrosio Lukoki (kulia kwa Waziri), Mkuu wa Mabalozi wa Nchi za Afrika na Balozi wa Angola hapa nchini na Bw. John Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa


Mhe. Membe akiendelea na hotuba yake.

Mabalozi wa nchi mbalimbali waliopo hapa nchini wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)

Sehemu nyingine ya Mabalozi wakimsikiliza Mhe. Membe.

Mabalozi na wageni waalikwa wakimsikiliza Mhe. Membe.

Balozi Walidi Mangachi akiwasilisha mada kuhusu "Pan-Africanism and African Renaissance" wakati wa maadhimisho hayo huku Mhe. Membe, Mabalozi na Wageni waalikwa wakimsikiliza.

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bi. Tonia Kandiero akiwasilisha mada kuhusu mchango wa benki hiyo katika maendeleo ya Afrika.

Wageni waalikwa wakisikiliza mada mbalimbali zilizowasilishwa.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.