Wednesday, July 19, 2017

Chungulia Fursa Boda to Boda

Kituo Kikuu cha Mabasi, Dodoma
Bw. Justin Kisoka, Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye amebobea katika masuala ya uchumi akitoa somo namna vijana wa Kitanzania watakavyoweza kuuza bidhaa zao ndani ya soko la Afrika Mashariki lenye nchi sita na idadi ya watu wanaofikia milioni 165. 
Mfanyabiashara akielezwa namna bidhaa zake ambazo amezibeba kichwani atakavyoweza kuziuza katika nchi za Afrika Mashariki na kupata faida kubwa.

Ujumbe wa kutaka vijana na Watanzania kwa ujumla wazinduke ili wanufaike na soko la Afrika Mashariki ulifikishwa kwa njia tofauti ikiwemo sanaa ya maigizo.

Baadhi ya watu waliojitokeza kupata mbinu za kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hapa ilikuwa Kituo Kikuu cha Mabasi mjini Dodoma.


Gandhi Hall , Mwanza 

Bw. Justin Kisoka akiwa kwenye bustani ya Gandhi Hall mjini Mwanza akitoa somo namna Wanamwanza watakavyoweza kuuza Sato, Sangara na bidhaa nyingine katika soko la Afrika Mashariki.

Wanamwanza acheni woga, vukeni mipaka ya Tanzania kuuza bidhaa zenu, ni baadhi ya maneno aliyokuwa anayatumia Mchumi huyo katika kuwashajihisha vijana wachangamke kuvuka mipaka ya Tanzania kuuza bidhaa zao.

Dada somo limemkolea anapata maelezo zaidi kutoka kwa wataalamu wa Wizara ili shughuli ya kuvuka mipaka ianze mara moja.


Viwanja vya Furahisha, Mwanza
Bw. Abel Maganya, Mtaalamu wa Masuala ya Afrika Mashariki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje akitoa somo kwenye viwanja vya  furahisha. 

Serikali za Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinatimiza majukumu yake kwa kuweka mazingira mazuri ikiwemo sheria, kanuni na miundombimu ili wanajumuiya mfanye biashara katika nchi unayopenda bila bugdha. Msijifungie ndani vukeni mipaka kupeleka bidhaa mbalimbali.

Baadhi ya Wananchi waliojitokeza katika viwanja vya furahisha.

Mzee anasema somo limengia barabara hivyo na  uzee wangu nawahimiza wajukuu zangu kufanya biashara ya kuvuka mipaka. Anafikisha ujumbe wake kwa kushiriki kusakata dance linalohimiza biashara za kuvuka boda.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.