|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe. Naimi Aziz (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Balozi Samwel Shelukindo mara baada ya kukabidhiwa tuzo za Tanzania. |
|
Balozi Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akipokeza tuzo za Tanzania kutoka kwa afisa wa Umoja wa Afrika wakati wa Mkutano wa Umoja wa Afrika. |
Na. Immaculate
Makilika – MAELEZO
Serikali ya
Tanzania imepewa tuzo 2 za masuala ya Ustawi wa Jamii pamoja na ushirikishwaji
wa wanawake katika ngazi ya maamuzi ya Serikali na Taasisi mbalimbali katika
Mkutano wa 27 wa Umoja wa Nchi za Afrika (AU) uliofanyika hivi karibuni Kigali
nchini Rwanda.
Hayo yamesemwa
leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi, Augustine Mahiga, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi
wa habari kuhusu mambo yaliyojadiliwa katika mkutano wa 27 wa Umoja wa nchi za
Afrika uliofanyika hivi karibuni Kigali nchini Rwanda.
“Tanzania
imetambuliwa na AU kama nchi ambayo kwa miaka 15 sasa imekua na mikakati
mbalimbali ya kitaifa ya kuzingatia haki za wanawake na kutimiza malengo ya
Milenia,” alisema Balozi Mahiga
Aliongeza kuwa
Tanzania ni kati ya nchi tano bora katika bara la Afrika ambazo zimepewa tuzo
hizo.
Katika hatua
nyingine, Balozi Mahiga amasema kuwa katika mkutano huo wa 27 viongozi wa
Afrika walizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo hati ya kusafiria Afrika (passport),
ambayo itawezesha watu wa bara hilo kusafiri katika nchi zote za Afrika.
Balozi Mahiga
aliongeza kuwa, lengo la kuanza kutumia hati hiyo ya kusafiria kwa nchi za
Afrika ni kutoa vikwazo vilivyokuwepo wakati wa kutembelea na kusafiri ndani ya
nchi hizo.
Aidha, Balozi
Maiga amesema kwamba, kutolewa kwa hati ya kusafiria ya Afrika ni ishara ya
Umoja na mshikamano, hati hizo zimeanza kutolewa kwa marais na viongozi wa
Serikali wa nchi ambazo zilihudhuria mkutano huo. Hati hizo zitatumika kwa
kuzingatia sheria za kila nchi.
Hali kadhalika,
mkutano huo ulijadili migogoro ya nchi za Burundi na Sudani Kusini ambapo
viongozi hao walikubaliana kupeleka Jeshi la Umoja wa Afrika nchini Sudani
Kusini ili kutenganisha majeshi ya pande mbili zinazoendelea kupigana nchini
humo.
Aidha, mgogoro
wa Burundi bado unaendelea kupatiwa ufumbuzi kutokana na jitihada mbalimbali
zinazoendelea kufanywa na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye aliteuliwa na
mapema mwaka huu na viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkutano wa 27
wa Umoja wa nchi za Afrika wenye wanachama 54 ulifanyika Kigali nchini Rwanda
tarehe 18 mwezi huu, ukiwa ni mkutano wa pili kwa mwaka huu ulikua na kauli
mbiu inayosema mwaka wa haki za binadamu.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.