Tuesday, April 25, 2023

UJUMBE WA TANZANIA ULIVYOSHIRIKI MAANDALIZI YA MKUTANO MAALUM WA 48 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA EAC

Mkutano Maalum wa 48 wa Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki kwa ngazi ya Makatibu Wakuu umefanyika kwa njia ya mtandao tarehe 25 Aprili 2023 huku ujumbe wa Tanzania ukishiriki kutokea Dodoma.

 

Mkutano huo  ambao ulianza  kwa ngazi ya Wataalam tarehe 24 Aprili 2023 umejadili pamoja na mambo mengine Taarifa ya Mkutano wa Kamati ya Fedha na Utawala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika mwezi Machi 2023 pamoja na  Taarifa ya Kamisheni ya Ukaguzi wa Fedha za Jumuiya kwa kipindi kilichoishia tarehe 30 Juni 2022.

 

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Mkatibu Wakuu umeongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi.

 

Vilevile, mkutano huo umehudhuriwa na Wajumbe kutoka nchi zote Wanachama wa Jumuiya ambazo ni Burundi, Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na Sekretarieti ya Jumuiya hiyo.

Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo kwenye Mkutano wa Makatibu Wakuu uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 25 Aprili 2023 kuandaa Mkutano Maalum wa 48 wa Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki.
Mkutano ukiendelea
Balozi Mbumdi akiwa na Wajumbe wengine wa Tanzania kwenye Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mkutano ukiendelea

Wajumbe kutoka Tanzania katika Mkutano wa Makatibu Wakuu

Mkutano ukiendelea

Makatibu Wakuu kutoka Nchi wanachama wakishiriki Mkutano kwa njia ya mtandao

 

 

 


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.