Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) leo tarehe 21 Aprili 2023 imeshuka dimbani kucheza mchezo wake wa wanne dhidi ya timu ya Wizara ya Fedha na Mipango (Hazina FC) ambapo imepoteza kwa goli 1-0.
Mchezo huo ulioanza majira ya saa 3.00 asubuhi katika uwanja wa Ujenzi uliopo mjini Morogoro, Nje Sports iliruhusu goli la mapema katika dakika ya 2’ ya kipindi cha kwanza cha mchezo ambapo lilidumu hadi mwishoni mwa mchezo.
Baada ya kupoteza mchezo huo Nje Sports inasalia na alama zake 7 katika kundi C huku ikishika nafasi ya pili katika kindi hilo nyuma ya Ulinzi FC yenye alama 9.
Nje Sports kesho tarehe 22 Aprili 2023 inatarajiwa kushuka dimbani kucheza mchezo wake wa tano (5) dhidi ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Michezo hii ni muendelezo wa mashindano yanayoendelea mjini Morogoro kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) yatakayo adhimishwa Kitaifa mjini humo tarehe 1 Mei 2023.
Katika hutua nyingine timu ya kuvuta kamba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeibuka na ushindi dhidi ya TAMISEMI katika mchezo uliochezwa saa 12.30 asuhuhi katika uwanja wa Jumhuri mjini Morogoro.
Wakati huohuo timu ya Wanawake inayoshiriki mashindano ya mpira wa pete ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki saa 1.00 asubuhi ilishuka dimbani kucheza dhidi ya mpinzani wake Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambapo imepoteza kwa magoli 47-5 kwenye mchezo iliochezwa Jamhuri mjini Morogoro.
Mshambuliaji machachari wa Nje Sports Bw. Mikidadi Magola akiwatoka walinzi wa Hazina FC katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Ujenzi mjini Morogoro |
Moja ya goli lililofungwa kwenye mchezo kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari |
Moja ya goli lililofungwa kwenye mchezo kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari |
Mchezo kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mawasiliano ukiendelea |
Winga machachari wa Nje Sports akipiga shuti baada ya kuwatoka walinzi wa Hazina FC katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Ujenzi mjini Morogoro |
Mechi kati ya Nje na Hazina FC ikiendelea katika uwanja wa Ujenzi mjini Morogoro |
Wachezaji wa Nje FC wakipata nasaha za kocha Bw. Shaaban Maganga wakati wa mapunziko |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.