Monday, April 24, 2023

NJE SPORTS HOI MBELE YA WAKUSANYA MAPATO


Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuingia dimbani kuwakabili wapinzani wao timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) kwa mara nyingine jana tarehe 23 Aprili 2023 ilishuka dimbani kucheza na timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika hatua ya timu 16 bora kwenye michuano ya kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) yanayoendelea mjini Morogoro 

Katika mtanange huo ulionza majira ya saa 10.30 jioni kwenye uwanja uliopo Solomon Mahlangu Kampas – Mazimbu, Nje Sports ambayo ilipewa nafasi kubwa ya ushindi kabla mchezo ilipoteza kwa goli 1-0 liliofungwa na mshambuliaji Erick Mwita katika dakika ya 20 ya kipindi cha kwanza, na kudumu hadi dakika ya mwisho wa mchezo. 

Katika hatua hiyo ya mashindano ya timu 16 bora ilihusisha timu ya TAMISEMI, Morogoro DC, Uchukuzi, Afya, Mahakama, TANROADS, HAZINA, Maliasili, TRA, Nje Sports, TANESCO, Kilimo, CRDB, Mambo ya Ndani, Wizara ya Ulinzi na TPDC.

Baada ya kufungwa katika mchezo huo Nje Sports imepoteza nafasi ya kuendelea kushiriki katika mashindano ya mpira wa miguu, hivyo wanamichezo wake wataendelea kushiriki katika mashindano ya michezo mingine ikiwemo kuvuta kamba, bao na drafti.

Mashindano hayo yanayohusisha michezo mbalimbali kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Dunia (Mei Mosi), itakayo adhimishwa kitaifa mjini Morogoro tarehe 1 Mei 2023.

Wachezaji wa Nje Sports na TRA wakiwania mpira katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja uliopo Solomon Mahlangu Kampas – Mazimbu.
                                           Mchezo ukiendelea
Safu ya ulinzi ya Nje Sports ikiwa imejipanga kuzima moja ya shambulizi lililofanywa na TRA 
Mshambuliaji wa Nje Sports akiwatoka walinzi wa TRA katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja uliopo Solomon Mahlangu Kampas – Mazimbu

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.