|
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe aliyeongoza ujumbe wa Tanzania
katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji
Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu akizungumza katika Mkutano huo uliofanyika tarehe 19, Aprili jijini
Kampala, Uganda. |
|
Makatibu Wakuu ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Uratibu ya Mkutano wa Tano wa Baraza
la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya
Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ngazi ya Makatibu Wakuu
uliofanyika tarehe 19, Aprili jijini Kampala, Uganda. |
|
Ujumbe wa Tanzania
katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji
Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu ukifuatilia Mkutano huo |
|
Ujumbe wa Uganda
(kushoto) na ujumbe wa Tanzania (kulia) katika Mkutano wa Tano wa Baraza
la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji
Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya
Afrika
Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu ukifuatilia Mkutano huo |
|
Washiriki wa Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji
Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu wakifuatilia Mkutano huo. | |
|
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe aliyeongoza ujumbe wa Tanzania
katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji
Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu akipongezana na Kaimu Mkurugenzi Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Judith Ngoda baada ya kumalizika kwa Mkutano huo uliofanyika tarehe 19, Aprili jijini
Kampala, Uganda. |
|
Katibu
Mkuu wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe aliyeongoza ujumbe wa
Tanzania
katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na
Ukuzaji
Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya
Afrika
Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu baada ya
kumalizika kwa Mkutano huo uliofanyika tarehe 19, Aprili jijini
Kampala, Uganda. |
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
itaendelea kushirikiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
kuhakikisha rasilimali za uvuvi katika Ziwa Victoria zinalindwa ili zinufaishe
jamii zinazozunguka ziwa hilo na mataifa husika kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe aliyeongoza ujumbe wa Tanzania
katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji
Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika tarehe 19, Aprili jijini
Kampala, Uganda.
Prof. Shemdoe aliuhakikishia mkutano
huo kuwa, Tanzania itaendelea kuchukua hatua madhubuti za kusimamia ziwa hilo
kama nchi wanachama wa wa LVFO zilivyokubaliana. Alisisitiza pia kuwa Tanzania inaendelea
kudhibiti matumizi ya zana haramu za uvuvi, kupiga marufuku uvuvi wa samaki wachanga,
kudhibiti utoroshaji wa mazao ya uvuvi na kuhamasisha ufugaji wa samaki kwa
vizimba katika Ziwa Victoria bila kuathiri mazingira.
Amesema pia, Tanzania imeimarisha
udhibiti wa uingizaji wa zana za kuvulia samaki ili kuzuia uingizaji wa zana
haramu nchini na kuendesha ukaguzi wa kina ili kuhakikisha uvuvi endelevu
unafanyika kwa tija.
Pia Profesa Shemdoe alitanabaisha kuwa
mchango wa Sekta za Uvuvi katika uchumi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
ni mdogo sana kwakuwa mchango wake unahesabiwa katika maeneo ya uvuvi na
ukuzaji bila kujumuisha mapato yanayotokana na shughuli zote zinazofanyika
katika minyororo yake ya thamani.
“Mchango wa Sekta za Uvuvi katika uchumi
wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ni mdogo sana kwakuwa mchango wake
unahesabiwa katika maeneo ya uvuvi na ukuzaji bila kujumuisha mapato
yanayotokana na shughuli zote zinazofanyika katika minyororo yake ya thamaniBadala
yake thamani hiyo inajumuishwa katika sekta zingine na hivyo kutokutoa picha
halisi ya Sekta ya Uvuvi,” alisema.
Katika mkutano huo, Balozi wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda, Dkt. Aziz Mlima, alimwakilisha Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt.
Samwel Shelukindo.
Kikao hiki kimehudhuriwa na nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zilizopo katika Taasisi ya Uvuvi
ya Ziwa
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.