Thursday, April 20, 2023

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI YASHIRIKI UFUNGUZI WA MICHEZO YA MAADHIMISHO YA MEI MOSI


Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wanaoshiriki katika michezo inayoendelea mjini Morogoro wameungana na maelfu ya wafanyakazi wenzao kushiriki katika sherehe ya ufunguzi wa tamasha la michezo kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) yatakayofanyika Kitaifa mjini Morogoro.

Ufunguzi huo uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro umefanywa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Fatma Abubakar Mwassa na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Wafanyakazi nchini.

Mhe. Mwassa akihutubua wafanyakazi waliojitokeza katika uwanja wa Jamhuri ametoa wito kwa Watumishi kuendeleza utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuongeza ukakamavu na kupunguza uwezekano wa kuugua magonjwa yasiyo ambukizwa kama inavyoshauriwa na Wataalamu wa Afya. 

“Michezo ni afya, michezo ni furaha, michezo ni urafiki hivyo naendelea kusisitiza Wafanyakazi kuendeleza utamaduni wa kufanya mazoezi kama ambavyo sera inavyohimiza ilikuongeza utimamu wa mwili na akili. Mfanyakazi anayezingatia michezo au mazoezi hata ufanisi wake kazini huwa nimzuri zaidi” ameeleza Mhe. Mwassa

Sherehe za ufunguzi wa tamasha hilo lilishindikizwa na michezo na burudani mbalimbali ambapo Viongozi waliohudhuria uwanjani hapo akiwemo Mhe. Prof. Joyce Ndalichako Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu walipata nafasi ya kujionea ujuzi, ukakamavu na umahiri wa watumishi katika michezo.

Kwa upande wake Timu ya Wanawake ya mpira wa pete ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) ilicheza dhidi ya timu ya Mahakama ya Tanzania mbapo Timu ya Mahakama imeibuka na ushindi wa magoli 37 dhidi 3 

Timu ya mpira wa pete ya Nje Sports imeendelea kuwa na mwenendo wa kusua sua katika mashindano hayo ambapo Kiongozi wake Bi. Pili Rajabu ameeleza kuwa uwepo kwa majeruhi wengi katika kikosi chake kinaifanya timu hiyo kutokuwa katika nafasi nzuri ya ushindani hivyo kupoteza michenzo mingi wanayoshiriki.
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye maandamano wakati wa sherehe za ufunguzi wa michezo kuelekea maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wafanyakazi duniani yatakayofanyika Kitaifa mjini Morogoro

Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye maandamano yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuelekea maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wafanyakazi duniani yatakayofanyika Kitaifa mjini Morogoro



Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Abubakar Mwassa akihutubia watumishi waliojitokeza katika uwanja wa Jamhuri mkoani humo kwenye sherehe za ufunguzi wa michezo kuelekea maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi).
Bi. Pili Rajab (mwenye mpira) mchezaji wa Nje Sports akiwatoka walinzi wa  Time ya Mahakama ya Tanzania katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri.  Timu ya Mahakama iliibuka na ushindi wa magoli 37 - 3 katika mchezo huo.




Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakila kiapo cha utiifu katika michezo ya kuelekea maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wafanyakazi duniani yatakayofanyika Kitaifa mjini Morogoro 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.